Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Katiba imepindishwa na na sheria imekiukwa,basi acha iendelee tumezowea kwa hilo ktk ccm ili kuhakikisha yao yanakwenda,siwezi kubishana na wewe wakati kitu kipo wazi kabisa... wa waendelee kupiga mabomu ile ndo sheria inavosema na katiba inavotaka. Mkuu haya yanauma wewe tuyaaache tu. kila la kheri..
Kila siku CUF wanalalamikia tume ya uchaguzi Zanzibar, hivi wao si ni sehemu ya tume hiyo? mbona wana makamishina kwenye tume hiyo? wanajilaumu wenyewe ama ni maigizo kwa wazanzibar?
Kila siku viongozi wa CUF wanalia juu ya ZEC sasa mbona hawawaambii makamishina wao wakajiuzulu?
Kwa hiyo Katiba inasema MARUFUKU kufanya SHUGHULI za kiserikali siku ya mapumziko? Tuonyesheni basi wapi inaposema hivyo! Mbona polisi wanafanyakazi siku za mapumziko. Mbona wanajeshi wanakuwa kazini siku za mapumziko. Mbona hospitali za serikali hazifungwi siku za mapumziko? Mbona bandari zinafanya kazi siku za mapumziko. Mbona zimamoto wako kazini siku za mapumziko? Mbona wakunga wanazalisha siku za mapumziko? Mbona vivuko vinafanya kazi siku za mapumziko? Unataka niendelee?
Acheni uongo. Na unafik.
Amandla......
Kweli wewe ni Fundi Mchundo. sasa mambo haya ya kihandisi mno uyawezi. Jiulize mbona huko Bara hamfanyi kazi siku za Jumapili na jumamosi?
Tofautisha kazi za huduma (service work)na kazi za kiofisi (Office work). Kazi za huduma huwa hazina ijumamosi wala ijumaapili wala sikukuu.Kweli wewe ni Hafif(u). Alikwambia nani kuwa bara hospitali, polisi, viwanja vya ndege, bandari, mahoteli, zimamoto zinafungwa siku ya jumapili na jumamosi? Umesikia wapi kuwa kufanya kazi siku ya mapumziko imekuwa kosa la jinai? Siku zote uandikishaji wa wananchi ( sensa n.k.) kunafanyika siku za mapumziko kwa sababu siku hizo ndiyo kuna uhakika zaidi wa kuwapata wengi wao. Leo mnataka kugeuza eti kuna 'hidden agenda'! kama nilivyosema awali, upuuzi mtupu.
Tofautisha kazi za huduma (service work)na kazi za kiofisi (Office work). Kazi za huduma huwa hazina ijumamosi wala ijumaapili wala sikukuu.
kazi za ofisini zinakuwa na mapumpumziko ya ijumaamosi na ijumaapili. kazi za Service zinakuwa na mapumziko ya mmoja mmoja na inaweza kuwa siku zozote.
Labda nikuulize mbona waalimu na wanafunzi ijumaamosi na ijumaapili wanapumzika?
Achana na ubishi wa kizembe. nimeshabainisha kuwa Kufanya hivi ni kosa kisheria.
Kila siku CUF wanalalamikia tume ya uchaguzi Zanzibar, hivi wao si ni sehemu ya tume hiyo? mbona wana makamishina kwenye tume hiyo? wanajilaumu wenyewe ama ni maigizo kwa wazanzibar?
Kila siku viongozi wa CUF wanalia juu ya ZEC sasa mbona hawawaambii makamishina wao wakajiuzulu?
Kuongezea tu. Tulikuwa tunafanya kazi nusu siku jumamosi. Lini katiba ilibadilishwa kusema kuwa jumamosi ni siku ya mapumziko? Mwinyi aliwahi kuanzisha mpango wa kufidia sikukuu. Lini katiba ilibadilishwa kuruhusu hiyo na kubadilishwa ilipobatilishwa? tumeongeza siku ya Nyerere katika siku za kupumzika. Lini katiba ilibadilishwa kuzungumzia hilo? Katiba ya nchi haiwezi kupanga muda wa mwananchi kupumzika bali inampa haki ya kupumzika. Sheria za nchi ndizo zinazopanga muda wa kupumzika na stahili za wafanyakazi watakaofanya kazi siku ambazo kisheria ni za kupumzika! Sheria inatafsiri katiba na sio katiba.
Christmas karibu inakuja tutaomba uandikishaji uendelee.Kuongezea tu. Tulikuwa tunafanya kazi nusu siku jumamosi. Lini katiba ilibadilishwa kusema kuwa jumamosi ni siku ya mapumziko? Mwinyi aliwahi kuanzisha mpango wa kufidia sikukuu. Lini katiba ilibadilishwa kuruhusu hiyo na kubadilishwa ilipobatilishwa? tumeongeza siku ya Nyerere katika siku za kupumzika. Lini katiba ilibadilishwa kuzungumzia hilo? Katiba ya nchi haiwezi kupanga muda wa mwananchi kupumzika bali inampa haki ya kupumzika. Sheria za nchi ndizo zinazopanga muda wa kupumzika na stahili za wafanyakazi watakaofanya kazi siku ambazo kisheria ni za kupumzika! Sheria inatafsiri katiba na sio katiba.
Amandla.......
Mkubwa, Huyo Hafif tatizo lake ni kuwa vituo vimefunguliwa ndani ya sikukuu ya kiislam, kama kawaida yao kulalamika... SIJUI INGEKUWAJE KAMA CHAGUZI ZOTE ZINGEFANYIKA IJUMAA.Kweli wewe ni Hafif(u). Alikwambia nani kuwa bara hospitali, polisi, viwanja vya ndege, bandari, mahoteli, zimamoto zinafungwa siku ya jumapili na jumamosi? Umesikia wapi kuwa kufanya kazi siku ya mapumziko imekuwa kosa la jinai? Siku zote uandikishaji wa wananchi ( sensa n.k.) kunafanyika siku za mapumziko kwa sababu siku hizo ndiyo kuna uhakika zaidi wa kuwapata wengi wao. Leo mnataka kugeuza eti kuna 'hidden agenda'! kama nilivyosema awali, upuuzi mtupu.
Amandla.......
Tatizo lako ni UDINI, VISASI, JINO KWA JINO etc. Mbona wenzio huwa tunaenda kusali halafu tunaelekea kupiga kura kila uchaguzi mkuu unapowadia???Christmas karibu inakuja tutaomba uandikishaji uendelee.