Baada ya mgonjwa wetu kurudishwa hospitali kutokana na kushindwa, ikatulazimu kujaribu upande mwingine, sasa zunguka weeee bila bila, afadhali hakuna.
Jana tukatonywa juu ya uwepo wa mtaalamu mwingine kijiji fulani, tukaondoka huko tulikokuwa na leo asubuhi tumefika kwa huyo 'mtaalamu'.............dah!
Sura ya 'kitaalamu' kweli kweli, inatisha akikuangalia. Mazingira ya kitaalamu pia, zagazaga za kila aina na kila sehemu. Masharti sasa, hilo la kwanza tu sielewielewi mpaka sasa; eti yeye kwake wito wake unaitikwa kwa sauti ya 'beeeee'. Hiyo ni kwa yeyote (awe mgonjwa au muuguzi; awe me au ke) na wakati wowote utakaokuwa hapo.
Nipo hapa nje natafakari haya maisha wakati wengine wapo huko wanaendelea kusikiliza yaliyobaki!