Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,831
- 5,489
Kitendo cha HAMAS kuvamia Israel na kuua baadhi ya Raia, kumimina risasi uraiani, na kuteka watu ikiwemo watanzania wawili, icho tayari ni kitendo cha Kigaidi (Terrorism Act), rejea maana ya neno 'Terrorism' au 'Ugaidi'. Hata hivyo mwanzo watu walionekana kufurahishwa na vitendo vya Hamas.
Israel kujibu mapigo na kufanya patrol ya kuwatafuta Hamas ndani ya mji wa Gaza, ni hatua yoyote ambayo serikali yeyote Duniani ingefanya hili kulinda raia wake na mali zake dhidi ya maadui. Rejea kisa cha Vita ya Kagera baada ya Idd Amini kufanya mashambulizi dhidi ya Tanzania, ni kwamba Tanzania iliingia mpaka Uganda kuhakikisha inamuondoa Dada Idd Amini. Ndicho Israel inachokifanya dhidi ya Hamas mjini Gaza.
Hamas sio Nchi, Hamas sio Dini. Hivyo inashangaza kuona watu wanatetea uovu wa Hamas kwa kutumia neno "Free Palestine". Kwani nani kakuambia Palestina ndio imevamiwa, lililovamiwa ni eneo la gaza ambalo Hamas ndiko walikojificha na kuficha mateka. Palestina ina maeneo mawili ambayo hata hivyo nayo hayaelewani, kuna Gaza na West Bank. Raia wa West Bank hawana shida, wala hawashambuliwi. Hata serikali ya West Bank haiwakubali wanamgambo wa Hamas. Kutumia neno Palestina wakati wanaopigwa ni Hamas, ni matumizi mabaya ya neno palestina. Ingekuwa inayopigwa ni Nchi basi tungeona hata Ukanda wa West Bank nako kuna mashambulizi yanayorushwa na Wapalestina.
Mwisho kuweka Ukristo au Uislamu kwenye hii vita, huo ni utahira. Dini zenyewe umezaliwa umezikuta zimeletwa na wamishionari na Waarabu, wewe unazipaparukia. Unajiona huko radhi kumsaidia mpalestina au muisrael kuliko jirani yako Congo.
Watanzania na waafrika tuamkeni, tujenge nchi yetu na bara letu na sio kutukuza Dini na Nchi za ughaibuni wakati hali zetu za maisha zinadidimizwa na hao hao.