Dunia ijifunze nini kutoka demokrasia ya Marekani? Mgombea aliyekuwa na mashtaka ya uhaini na ubakaji kurudi madarakani

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Ni kawaida uongozi wa Marekani kuwafanyia nongwa viongozi wa nchi nyengine duniani wanaposhutumiwa kwa makosa mbali mbali hata yasiyothibitishwa na mahakama.

Kinyume chake raisi Donald Trump aliyeapishwa leo kurudi ikulu ya Marekani ni kiongozi ambaye kwa miaka minne aliyokuwa nje ya Ikulu alikabiliwa na mashtaka kadhaa na ambaye hatimae yaliyotolewa hukumu.

Pamoja na hivyo kiongozi huyo amerudi madarakani kama kwamba aliyotenda hayakutokea.

Suala jengine katika uchaguzi huo uliopita inaonekana kulikuwa na rushwa kubwa iliyotolewa na mabilionea wa nchi hiyo kubadili matokea. Vitita vya dola zilizotolewa na watu kama Ellon Musk lilikuwa ni jambo ambalo halikufichwa.

Kitendo kama hicho daima Marekani imekuwa ikielekeza kuwa vyama vya kisiasa vipokee ruzuku pekee kutoka serikalini. Akitokea tajiri akafadhili vyama vya siasa basi serikali za nchi hizo nazo humfanyia vitimbi vya wazi tajiri huyo mpaka atakasalimu amri.

Kwa ufupi kuna lipi la kujifunza katika kurudi madarakani Donald Trump.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…