Saved Souls
New Member
- Feb 27, 2019
- 3
- 3
DUNIA NA VIPINDI VYAKE, ILIPOANZIA, ILIPO NA INAPOELEKEA.
SEHEMU YA PILI
DUNIA NA MAHALI ILIPOANZIA
BWANA alipomuumba Adamu alimweka kuwa mtawala na msimamizi wa dunia na viumbe vyote vyenye mwili lakini mamlaka kuu ilikuwa ni ya BWANA kwa kuwa utawala wake ni juu mbinguni na chini duniani na ndani ya bahari. (Dan 4:25 b).
Na Adamu alikuwa ni mfano wa ufalme wa Mungu katika mambo yaonekanayo kwa sababu aliumbwa kwa mfano wa Mungu ili kutawala vyote vyenye miili (Mwa 1: 26)
Adamu aliasi sheria za BWANA mbele ya macho ya BWANA katika bustani na utawala wa BWANA, na BWANA akamfukuza katika umiliki wa Edeni (Mwa 3).
Adamu alipata watoto lakini wote hawakumfanania wote walikuwa na asili ya uovu uliowafanya kuwa tofauti kabisa na Adamu. Alimzaa kaini, akamzaa Habili, lakini wote hata kwa rangi na sura na tabia na mioyo haikumfanania Adamu.
Na ndipo Adamu akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi (Mwa 5:3)
Ukimtoa Kaini na habili kwa sababu ya tukio Adamu alizaa wana wengi lakini wote walielekea njia zao zilizokuwa machukizo mbele za BWANA nao waliabudu miungu wakijisimamishia kila mmoja muungu wake mbele za BWANA (Mwa 5: 4)
Vizazi vya Sethi na hivyo vizazi vingine vya Adamu viliingiliana katika shughuri mbali mbali japo ni mara chache vilipopata vibari vya kuoana, mfano wake ni,pale Lameki mwana wa Methushaeli mjukuu wa mbali wa Kaini alipopata kibali cha kuoa wana wawili wa Keinani kijukuu cha Sethi. Na hiyo tafsiri yake inaweza kuwa ni kuelekea ule utimilifu wa Laana ya Kaini juu ya damu ya nduguye (Mwa 4: 9-15 hakuna neno la BWANA lipotealo), kwa sababu mtoto wa Lameki (Tubal-Kaini) inaelezwa kuna sehemu alichangia katika lile tukio la Kaini kupigwa mshale na Lameki japo Lameki alipojua amemuua babu yake alimshambulia mwanaye kwa ngumi hadi alimuua.Na hapo aliondoka mbali na wakeze kwa sababu walinuia kumuua kwa sababu aliua mtoto wao, na baaada ya kujificha mbali na wakeze kwa muda mrefu nao hasira yao ilipotulia ndipo alipowaendea na utasoma kujieleza kwake katika (Mwa 4:23)
Tamati ya vizazi vingine vya Adamu ukiachia uzao wa Sethi kwa mfuatano wa Henoko (Enock) hadi Nuhu na kizazi chake ilifikiwa baada ya kuingiliwa na kuchanganyika na uzao wa malaika walioasi makao yao ya kimbingu.
UKWELI KUHUSU ILE GHARIKA KUU, MANEFILI/MAJITU NA KIBALI KATIKA KIZAZI CHA SABA CHA ADAMU (HENOKO) MALAIKA WAASI, UKAMILIFU WA NUHU NA UWEPO WA MABAKI YA MANEFILI/MAJITU KATIKA DUNIA HII YA LEO.
"Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na WANA WA KIKE wakazaliwa kwao, WANA WA MUNGU waliwaona hao BINTI ZA WANADAMU ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua" ( Mwa 6:1-2)
"Ikawa wanadamu walipoongezeka, katika siku hizo walizaliwa MABINTI WAZURI. Na MALAIKA WANA WA MBINGU waliwaona na wakawatamani, nao wakaambiana "twende na tuchague WAKE katika binti za Adamu na tujizalie wana"
Basi malaika wale wakiongozwa na Semyaza ambaye ni kiongozi wao aliwapa sharti la kiapo na kujifungamanisha kwa pamoja katika laana ambayo ingewakuta kwa dhambi ile waliyokuwa wanakwenda kuifanya. Wakashuka juu ya kilele cha Ardis cha mlima Hermon na wakafanya kiapo kile huku wakijua ni dhambi kuu wanayokwenda kuitenda lakini wakadhamiria kuitenda kwa ufanisi mkuu (efectively). Walikuwa mia mbili wenye viongozi Ishirini waliokaa juu ya kila kumi kwa makumi ishirini. Na mlima ule uliitwa Hermon kwa sababu kwa uovu ule walifanya kiapo juu ya mlima huo.
Walishuka (wakaigiza maumbo ya wanadamu) wakachukua wake kwa kila mmoja, nao wakafanya uovu ule mkuu, nao wanawake wakapata mimba wakazaa majitu (manefili) inaelezwa urefu wao hao majitu ulikuwa dhiraa Elfu tatu (3,000) "nao wanefili/majitu walikuwako duniani siku zile.... " Mwa 6:4
Majitu hao walikula vyakula vyote vya wanadamu wakamaliza, hadi wanadamu wakashindwa kuwahimili. Hao majitu wakageuka na kuanza kuwala wanadamu, wakatenda maovu kwa wanyama, ndege, samaki na wadudu na mijusi (reptiles) ikapelekea interbleedings, na kutokea viumbe wa ajabu. Wakala wanyama na kunywa damu. Dunia ikalalamika.
MATOKEO YA MUINGILIANO ULE WA MALAIKA NA WANADAMU.
AZAZEL kiongozi mkuu, akawafundisha wanadamu kutengeneza panga/upanga, visu, nyembe na ngao na ngao zifunikazo vifua.
Akawaonesha mengi yazidiyo hayo, akawaonesha jinsi ya kutengeneza ; vikuku (blacelets) , vidani, mapambo na jinsi ya kutengeneza macho na jinsi ya kulemba kope akawaonesha mawe ya thamani, na kila aina ya rangi za kupaka. Wakaweka shepu za viuno vyao. Na dunia ilibadilika.
Palikuwa na UASI MKUBWA, na UZINZI MWINGI URIKITHIRI, na wanadamu waiingia katika uovu na njia zao zote zikaharibika.
Wakawafunza uandishi, wakajifunza ulozi, wakawafunza uchawi, wakawafunza UNAJIMU NA NJIA ZA MWEZI, wakawafunza kutamka laana na mengine mengi yaliyo machukizo makuu.
Na kwa matendo ya majitu wana wa malaika wale walifanya uharibifu mkubwa, na katika uharibifu huo na mauaji, SAUTI ZA VILIO VYA NAFSI ZA WANADAMU ZILIZOKATILIWA ZIKAFIKA MBINGUNI.
Na Michael, Gabriel, Suriel na Uriel wakatazama chini kutoka mbinguni wakaona umwagaji wa damu na uovu uliokuwa Duniani. Wakaambiana "Basi dunia iharibiwayo ilie na sauti ziliazo zifikie lango la mbinguni"
(Palifuatia malalamiko mengi ya malaika wakimueleza BWANA Mungu juu ya wale malaika walioasi na kwamba yeye alijua lakini hakuzuia. Naye MFALME wa Wafalme akaongea ( fuatisha andiko la Biblia ; BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. " BWANA akasema_nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemuumba usoni pa nchi;mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi kwamba nimewafanya". Lakini NUHU akapata Neema machoni pa BWANA. Mwa 6:6-8) na kumtuma Arsyalalyur kwa mwana wa Lameck(Nuhu) akimwambia (hili lilikuwa ni agizo la mbele kuelekea uharibifu, hivyo agizo lilianza kutimizwa mapema kwa sababu huyo malaika ilibidi amfundishe Nuhu njia ili yeye na uzao wake waokolewe na uharibifu ule uliokuwa unaijia dunia). Akamwambia
"kamwambie kwa jina langu; jifiche wewe, na umuoneshe ule mwisho ambao unakuja kwa sababu dunia yote na vyote vilivyomo vitaharibiwa, kwa hiyo sasa mfundishe ili kwamba aepuke uharibifu ule na uzao wake utaishi/utaokoka juu ya dunia yote".
BWANA aliitamka hukumu yote ambayo utimilifu wake ulianza mapema kabla ya kuzaliwa Nuhu na kabla ya Henoko hajachukuliwa na kabla ya gharika ile kuu.
Naye Henoko (Enock) alikuwa mwandishi mkamilifu wa kipindi kile( scribe righteous) alikuwa ni mwenye haki na mwenye kuliita jina la BWANA, mtakatifu, aliyeziishi njia za BWANA. Na tazama malaika akamuita Henoko
"Henoko mwandishi mwadilifu, nenda uwataarifu wana wa mbingu ambao wameacha mbingu (Yud 1:6 inakili ujumbe huu) na makazi matakatifu ya milele na kujiharibu wenyewe kwa wanawake, na kufanya yote kama ambavyo WANA WA ADAMU hufanya, na kuchukua wake na kujikuta wameharibika moja kwa moja juu ya dunia; kwamba hawatakuwa na amani, wala dhambi zao hazitosameheka, na hawatafarijika kwa ajili ya watoto wao, watayaona mauaji ya wapendwa wao, na kwa kuharibiwa kwa wana wao watalalamika na kuomba kusamehewa milele lakini hawatohurumiwa wala hawatopata amani".
(" Nae Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya UNABII juu ya hao....Yud 1: 14.... Lakini kitu kibaya kilichopo kwenye biblia zetu ni kwamba, biblia imechanganywa sana isivyo kawaida, nitazungumza kuhusu hili pia hapo mbeleni)
Nae Honoko akaenda na kusema kwa Azazel "hutokuwa na Amani, hukumu nzito/kuu unakuja dhidi yako kwamba utafungwa (you will be bound)".
Henoko akawafuata wale malaika waasi wakiwa wamekusanyika wakitetemeka kwa hofu. Wakamuomba awaandikie maombi yao ya msamaha ili kwamba waweze kusamehewa naye ayachukue ayapeleke mbele za BWANA awaombee, kwa sababu wao hawakuweza kuongea, wala kuinua macho yao juu mbinguni kwa uovu walioutenda.
Kisha Henoko akaandika nukuu ya maombi yao kwa msamaha, na maombi ya kushuka kwa hali zao za kiroho na matendo ya kila mmoja. Henoko aliyaandika akaondoka KWENDA kukaa kwenye maji ya Dan (mto Dani) ambao uko magharibi-kusini mwa mlima Hermon. Akaisoma ile nukuu kwa sauti hadi aliposhikwa na usingizi.
Na tazama akapata NDOTO, na MAONO yakamjia, akaona maono ya ghadhabu (wrath), kwamba inampasa kwenda kuwarudi wale WANA WA MBINGU (reprove). Na alipoamka aliwaendea, nao walikuwa wamekusanyika pamoja Kama wanaomboleza na nyuso zao zimefunikwa. Na akaongea mbele za wote Yale maono aliyoyaona kwenye ndoto, akawarudi Kama BWANA alivyomwamuru kwenye maono.
Akasema
"Niliyoyaona nilipolala ndiyo nitakayokwenda kuyasema kwa ulimi wa nyama na pumzi yangu ambaye yule MKUU amenipa kwenye mdomo kwamba yatazungumzwa nao na kueleweka kwenye mioyo. Kama alivyomuumba mwanadamu na kumteua kuelewa neno la busara, hivyo ameniumba na kuniteua kuwarudi WANA WA MBINGU.
Niliandika nukuu ya maombi yenu ya msamaha, lakini ndani ya maono yangu ilikwisha onekana kwamba maombi yenu hayatojibiwa kwenu siku zote za umilele. Na hukumu kamili amekwishatangazwa dhidi yenu, na hamtopata Amani. NA KUANZIA SASA HAMTORUDI MBINGUNI MILELE YOTE, na imehitimishwa kwamba mtatiwa kifungoni duniani kwa siku zote za milele. Na kabla ya hili, mtauona uharibifu wa wana wenu wapendwa. Na hamtafarijika kwao, lakini wataanguka kabla yenu kwa upanga na maombi yenu hayatajibiwa kwa heshima yao au kwa heshima yenu (in respect of them or in respect of yourselves) "
Kisha Henoko alielezea jinsi Yale maono yalivyokuja, na mawingu yakamwita na ukungu (mist) ukamuita na njia za nyota na upepo ukamfanya apae na ukamnyanyua hadi mawinguni. Alipaa hadi alipojikuta Karibu na kuta iliyojengwa kwa mawe ya barafu (hailstones) na ndimi za moto zikiizunguka nayo ikamfanya aanze kuogopa.
Akaenda kwenye ndimi za moto na akajikuta yu karibu na nyumba kubwa ambayo imejengwa na mawe ya barafu (hailstones) na kuta za nyumba ile zilikuwa Kama mapambo ya barafu (mosaic) na sakafu yake ilikuwa theruji. Paa lake lilikuwa Kama njia za nyota (path of stars) na mmweko wa mianga (flashes of lightings) na kati yao walikuwa ni makerubi wawakao na anga lao lilikuwa Kama maji. Na kulikuwa na moto uchomao/uwakao kuzunguka kuta Zake na milango yake iliwaka ikitetemesha moto
Anasema.
Nikaenda kwenye nyumba hiyo na ilikuwa ya moto Kama moto, na baridi Kama theruji, na hapakuwa na uhai wala maisha ndani yake. Hofu ikanivaa na kutetemeka kukanijaa. Na nilipokuwa nikitetemeka nilizama usingizini na nikaona kwenye njozi,
Na tazama, nyumba nyingine ambayo ilikuwa kubwa kuzidi ya mwanzo na milango yake ilifunguliwa mbele zangu, na lilijengwa kwa ndimi za moto. Na kila kitu kilikuwa kitukufu, na sakafu yake ilikuwa moto na juu njia za nyota na paa lake lilikuwa moto uwakao/uchomao.
Na nilipotazama ndani yake nikaona KITI CHA ENZI, na mwonekano wake ulikuwa Kama barafu(ice) na kilizungukwa na 'Kama jua linga'aalo' na sauti za makerubi. Na chini ya kiti cha Enzi kulitiririka moto ya moto kiasi kwamba ilikuwa ni vigumu kuiangalia.
Na yeye ambaye ni MKUU alikaa juu yake, na vazi lake liling'aa kuliko Jua na jeuoe kuliko theruji yoyote. Na hakuna malaika aliyeingia, na kwa muonekano wa sura yake yeye ambaye ametukuka na kuinuliwa hakuna kiumbe wa mwili ambaye angeweza kumuangalia.
Ziwa la moto liliwaka kumzunguka na moto mkuu ulisimama mbele Zake, Karibu nae. Makumi kwa makumi elf walisimama mbele Zake wala hakuhitaji mamlaka takatifu. Nao watakatifu ambao walikuwa Karibu nae hawakuondoka usiku na mchana.
Hadi hapo nilikuwa nimefunika uso wangu, nikitetemeka. Na BWANA akaniita kwa mdomo wake ananiambia " Njoo hapa Honoko (Enock) kwa neno langu takatifu". Na akaninyanyua akanileta Karibu na mlango. Na nilitazama uso wangu chini. Na akasema kuniambia kwa sauti yake "sikia, usiogope, Henoko, wewe ni mwenye haki, na mwandishi mwema, njoo hapa na sikia sauti yangu:
Nenda uwaambie waangalizi (watchers) wa mbingu ambao wamekutuma uwaombee msamaha; MLIKUWA NI WA KUWAOMBEA WANADAMU MSAMAHA, LAKINI SIO MWANADAMU KUWAOMBEA MSAMAHA NINYI. kwanini mmeondoka kwenye mbingu takatifu na kulala na wanawake, na kuwa nahisi kwa BINTI ZA WANADAMU, na kujichukulia wake, na kufanya Kama WANA WA DUNIA na kupata Wana majitu?.
Na mlikuwa wa kiroho, watakatifu, muishio maisha ya milele, lakini mmekuwa nahisi kwa kuingiliana na wanawake, na kupata watoto kupitia damu ya nyama, na tamaa imewawakia juu ya damu ya wanadamu na mmezalisha NYAMA NA DAMU KAMA WAFANYAVYO AMBAO HUFA NA KUHARIBIWA.
Na kwa sababu hii NILIWAPA WATU WAKE ILI KWAMBA WATAPANDA MBEGU KWAO, na kwamba WATOTO WATAZALIWA KWAO ili kwamba matendo yatendeke duniani.
Lakini ninyi, mwanzo mlikuwa wa roho muishio milele, maisha yasiyo na mwisho, kwa vizazi vyote vya Dunia. KWA SABABU HII NINYI SIKUWAANDALIA WAKE, KWA SABABU MAKAZI YA WALIO WA ROHO NI MBINGUNI.
Na sasa, majitu waliozaliwa Kutoka kwenye mwili na mnyama wataitwa "ROHO WAOVU/NAFSI OVU (EVIL SPIRITS) DUNIANI, NA DUNIANI PATAKUWA MAKAZI YAO". Na hizo nafsi ovu zitatoka kwenye miili yao, kwa sababu ni Kutoka kuu waliumbwa, Kutoka kwa wana watakatifu ulikuwa asili yao na msingi wao wa kwanza. Roho waovu watakuwa duniani na wataitwa "ROHO ZA UOVU"
Na makazi ya nafsi za mbingu ni mbingu, lakini makazi ya nafsi za Dunia, ambazo zimezaliwa duniani ni Dunia.
Na nafsi za majitu ZITAFANYA MAOVU, WATAHARIBU, WATASHAMBULIA, WATAPIGANA, WATAVUNJA DUNIA NA KUSABABISHA HUDHUNI, HAZITOKULA, HAZITOONA KIU, WALA HAZITAONEKANA (ndicho kilichopo leo, nitakielezea vizuri mbeleni)
Na nafsi Hizi zitainuka dhidi ya wana wa Adamu, na dhidi ya wanawake kwa sababu ZILIIACHA MIILI YAO WAKATI WA MAUAJI NA UHARIBIFU.
Na vifo vya majitu, wakati nafsi zikiiacha miili yao, miili yao itaharibiwa kabla ya hukumu. Hivyo wao (nafsi) wataharibiwa ifikapo Ile siku iliyo kuu ya hukumu kuu.
Na sasa kwa nao waangalizi, ambao wamekutuma kuwaombea msamaha ambao mwanzo walikuwa mbinguni "Mlikuwa mbinguni LAKINI SIRI (SECRETS) ZA MBINGU ZILIKUWA HAZIJAFUNULIWA KWENU, NA MLIJUA UTATA/SIRI (MISTERY) ZISIZO NA THAMANI. HIZI MMEZIFANYA ZIJULIKANE KWA WANAWAKEKWA UGUMU WA MIOYO YENU. Na kwa siri hizi, wanawake na wanaume wamesababisha uovu uongezeke duniani" kawaambie "hamtopata amani"
NA HUKO NDIKO HUKUMU YA DUNIA ILE ILIYOINGILIWA NA MALAIKA NA UCHAFU MKUU WA MANEFILI/MAJITU ILIPOTIMIA,
HENOKO ALICHUKULIWA NA BWANA AKATOKA KWENYE DUNIA ILE PASIPO KUFA (Mwa 5:21-24) AKIIACHA FAMILIA ILIYOKUWA NA WATOTO AKIWEPO METHUSELA ALIYEMZAA LAMEKI
KIKAPITA KITAMBO KIDOGO, LAMEKI AKAMZAA NUHU (Na ndipo Ile kazi ya Arsyalalyur ilipoanzia kwa kumfundisha NUHU njia za BWANA)
HADI NUHU ALIOA AKAZAA WATOTO ( SHEMU, HAMU, YAFETHI Mwa 5:32) ule uharibifu ulikuwa haujatimia bado
Mungu alikipa kizazi kile cha wanadamu waovu muda wa Miaka Mia na Ishiriri (120 years) kama angalizo, kwamba ikiwa watamrudia ataghairi angamizo juu yao na dunia, lakini hawakugeuka.
KISHA MUNGU AKAMPA MAELEKEZO NUHU YA MWISHO WA DUNIA NA JINSI YA KUIJENGA SAFINA NA ILE GHARIKA KUU IKASHUKA JUU YA DUNIA (Mwa 6:13- Mwa8:19 .... IKUMBUKWE PIA KATIKA KUMUAGIZA YULE MALAIKA ALIMWAMBIA AENDE KWA JINA LA BWANA AFICHE SURA NA UHALISIA WAKE)
FAMILIA YA NUHU ILIANZA HISTORIA MPYA JUU YA DUNIA IKIWA HAINA WANA WA MALAIKA (MAJITU/MANEFILI) LAKINI IKIWA NA ROHO WAOVU WENYE HASIRA WALIOIACHA MIILI YAO KWA MAUMIVU NA KUIVUA KWA MAKOVU YA VISASI.
WALIKUWA NI WAZAWA WA DUNIA ASILI YA MBINGUNI, WALIOKATILIWA MBALI, WAKIACHWA NAFSI ZAO ZIKIWA HAI PASIPO MIILI, ZISIZOKULA, ZISIZOONA KIU, ZISIZOONEKANA NA ZENYE UCHUNGU.
FUATANA NAMI KWENYE KIPINDI CHA PILI CHA DUNIA YA MWANZO (DUNIA ILIPOANZIA)
AMANI YA BWANA IWE NAWE.
#Saved Souls
Nitaendelea sehemu ya tatu...
Adamu, na Sethi, na Enoshi, na Kenani, na Mahalaleli, na Yaredi; na Henoko, na Methusela, na Lameki, na Nuhu, na Shemu, na Hamu, na Yafethi ( 1 Nya 1:1-4).