Leo asubuhi nimekutana na huyu mtoto akanikumbusha hichi kisa, kinaweza kutusaidia pia kujifunza kitu. Ni cha kweli wapendwa msianze kuchakachua
Kuna jirani yetu alizaa na mwanaume watoto wawili hawakufunga ndoa ila waliishi pamoja kwa muda na kuachana maisha yakaendelea. Kuna kipindi wakaanza kugombania watoto mama anawataka na baba anawataka.
Baada ya muda baba alikua akamchukua mtoto mkubwa alikua na 10yrs, alipofika huko kwao akaanza kuumwa, mama alipopata taarifa ikabidi aende kumuona mwanae, kwa hali aliyomkuta nayo akaomba kuondoka nae, ndugu wa mume na mume mwenyewe wakakataa ila mama akamchukua kwa nguvu.
Baadae ilikuja kugundulika mtoto ana sickle cell, hivi wandugu sicle cell mtu huwa anazaliwa nayo au inaweza kujitokeza hata mtoto akiwa na miaka kumi? hiki kinanichanganya kidogo.
Mtoto yule aliumwa kwa muda wa miezi nane akaisha kuliko maelezo, na kipindi chote mtoto anaumwa yule baba hakuwahi kanyaga wala kutuma pesa za matibabu ya mtoto, baada ya miezi tisa yule mtoto akafariki dunia. Cha kushangaza yule baba hakukanyaga msibani tukazika yule mtoto.
Yule mama kifo cha mwanae kilimuumiza sana, alikua na vidonda vya tumbo vikaanza kumsumbua sana, hali ikawa mbaya baada ya wiki mbili toka mtoto wake afe na yeye akafa tukamzika. Cha kushangaza tena huyo baba hakuja kwa mazishi ya yule mama, na mpaka nazungumza hivi yule baba hajawahi kanyaga hata yule mtoto mwingine hajawahi leta matunzo yake, leo asubuhi nilivyomuona amenikumbusha na kuamua kuleta hichi kisa.
Ninachojiuliza hivi mtu unaweza gombana na mzazi mwenzio mpaka ukafikia maamuzi haya. Hata kama ni maudhi mmeudhiana mtu unaweza kufikia hatua ya kususa watoto wako na kususia mpaka mazishi?
Dunia hii ina mambo jamani. Poleni kwa maelezo mengi.
Maty, asante kutukumbusha dunia ina mambo.
Mambo ya watoto ayajuaye ni mama, tatizo la hawa wamama zetu, anabeba mimba ya fulani, na kumchagua fulani ndio kuwa baba wa watoto. Masikini huyo baba, aliwalea watoto hao mpaka huyo aliyepata hiyo sickle cell ndio ikatibua mambo. Hospital walimwambia wazi, Sicle cell ni ugonjwa wa genetic na unaambukizwa kwa heredity, baba akaulizwa kwenye familia yenu mnao, hakuna!, nadhani alipima damu akukuta kumbe alikuwa analea tuu, baba mwenyewe yupo!.
Mama alipomfuata mtoto mgonjwa, aliyemkatalia sio baba, itakuwa ni dugu tuu maana siri aijua baba peke yake, mama alipomchukua mtoto, huku baba akaufunga kabisa ukurasa bila hata haja ya kuthibitisha kama mtoto aliyebakia pia sio wake.
Pamoja na hayo, huyo mwanamume, hana huruma kabisa, mbona tuku wanaume wengi tuu tunalea watoto ambao sio wetu kwa mapenzi yote?, wako wanaotoa mapenzi kwa kutofahamu, lakini tuko sisi wengine, tumeshafahamu, DNA hatupimi ili kukwepa uthibitisho, na tunalea kwa mapenzi tena hata zaidi ya wale wa damu yetu wenyewe.
Haya ndio mambo nyie wanawake mnao tufanyia. Utaweza kulea kwa mapenzi yote, ukimhesabu tuu mtoto ni inocent victim na ulikubali kuwa baba, why let the innocent victim ateseke kwa kosa la mama yake?.
Ni kweli dunia, ina mambo tena sio machache ni mengi, na sio madogo ni makubwa!.
Pasco.