SoC01 Dunia inakwenda kasi, tusibaki nyuma

SoC01 Dunia inakwenda kasi, tusibaki nyuma

Stories of Change - 2021 Competition

IoT

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2014
Posts
1,057
Reaction score
1,402
Maisha yetu huwa na thamani pale tunapoona uwezo wetu wa kutatua changamoto ni mkubwa. Maisha yetu hukosa thamani pale tunapojihisi hatuna kile kinachoweza kuongeza thamani katika maisha yetu.

Uwezo wa kutatua changamoto katika maisha hujengwa ili kutoa matokeo kusudiwa. Leo katika Story of Change, ningependa kuzungumzia namna gani mitaala na sera ya elimu inavyopaswa kubadilika ili kuleta maendeleo makubwa ya kiuchumi na kifikra miongoni mwetu Watanzania.

Ukweli mchungu ni kwamba soko la ajira kwa sasa ni changamoto kubwa, sio Tanzania tu bali duniani kote. Hivyo basi mitaala ya elimu yetu inapaswa kutujenga katika kutatua changamoto na matatizo ya kijamii ili kutengeneza ajira. Maelfu ya watu uhitimu shule n avyuo mbalimbali kila leo. Pamoja na hilo, ukweli mchungu ni kwamba wahitimu hao wamekosa ujuzi na maarifa yanayopaswa kuwa kichocheo kikubwa cha wao kutengerneza ama kupata ajira.

Uwezo wa kuelewa na kutenda kile walichohitimu imekuwa ni changamoto, hali inayofanya waajiri wengi kuona kuna haja ya kubadili mitaala.

Mambo kadhaa yanayoonesha kuwa ubora wa elimu yetu ni hafifu ni haya:
  • Uwezo wa kujenga hoja na kuwasiliana baina ya watu umekuwa na changamoto kubwa, sio tu kwa Lugha ya Kiingereza pia Lugha ya Kiswahili.
  • Uwezo wa kujisimamia katika utendaji kazi.
  • Wemejawa na hofu na hali ya kutokujiamini.
  • Uoga wa kuchangamkia fursa, hali inayofanya hali ya utegemezi kuendelea kukua siku hadi siku.
  • Kutokuwa na malengo ya muda mfupi au mrefu. Mipango ni ramani ya kumsaidia mtu namna bora ya kupata hitimisho katika malengo aliyojiwekea.
Kuthibitisha hayo, ikiwa utafanya observation kwa wahitimu wa shule binafsi zenye mitaala ya kimataifa au vyuo vya nje hasa kwa mataifa yaliyoendelea. Utaona ni kwa kiasi gani wahitimu wao wana uwezo mzuri wa kuwasiliana na kujenga hoja, pia kusimamia kile wanachokiamini.

Ukweli mchungu sio Watanzania wengi wenye kipato hiko cha kuwawezesha kupeleka watoto wao katika vyuo na shule hizo.

Hivyo basi kuna haja ya serikali na umma wa Watanzania wenye nia ya kuona Taifa letu linakuwa katika nyanja za kiuchumi na kijamii, kuona ipo haja ya elimu itolewayo iendane na wakati wa sasa na ujao.

Baadhi ya mambo ya kuzingatia ili kuendana na nyakati tulizopo nah apo baadae ni haya:
  • Serikali ione ipo haja ya kuweka mazingira mazuri ya kufundishia, yanayomwandaa na kumwezesha mtoro na kijana wa Kitanzania kuona fursa na kuchukua hatua. Kutengeneza mitaala itakayochochea ubunifu baina ya wahitimu. Mimi binafsi sioni kama na haja ya kusoma vitu vingi kuanzia Elimu ya Msingi, tunaweza kuanza kutengeneza umahiri kwa wanafunzi kusoma kwa tija (kutengeneza specialization mapema).
  • Serikali iendelee kutoa elimu kwa wananchi wake, kuwa ipo haja ya wao pia kushiriki katika suala la maendeleo. Mfano, elimu ya uzazi wa mpango ni muhimu zaidi nyakati hizi. Ipo haja ya jamii kuzaa Watoto inaoweza kuwahudumia kikamilifu kwa mahitaji muhimu.
  • Jamii kuelimishwa juu ya namna bora ya malezi, yatakayotoa nafasi kwa Watoto wao kuwa na mitazamo mikubwa ya kifkra.
Kwa kufanya haya, tutakuwa tumeisaidia Jamii ya Kitanzania kwa sehemu kubwa. Hivyo basi kutengeneza jamii iliyo salama katika nyanja zote za kiuchumi, kijamii, kiafya, nk.

Pia, tutapunguza wimbi la vijana kuwa na elimu isiyoweza kuwasaidia kutatua changamoto walizonazo. Ni ukweli usipingika kwa takwimu mbalimbali zilizopo ni kuwa vijana ni wengi zaidi. Na miongoni mwa kundi hili, wengi hawana vipato vya uhakika katika kuendesha maisha yao.

Pia, tutapunguza misongo ya mawazo, inayopelekea vifo wakati mwingine. Pia tutangeneza jamii iliyostaarabika kimawasiliano, kiafya, nk.

Hivyo basi, ni rai yangu kuwa ipo haja ya serikali kuweka msisitizo wa vitendo katika hayo na mengine mengi. Asanteni sana, na hii ndo Story of Change kutoka kwangu. Karibuni kwa mawazo yenu, ushauri na nyongeza zaidi.
 
Upvote 2
Of course that's big problems that face Africa continent.
But come to Tanzania is too worse, and Solutions of this issues is poor institutions tulizo nazo .
Na nature of leaders wanao tuongoza wanataka wazidi kutawala wao kwa wao mpaka mwisho na kurhithisha vizazi vyao at end.
 
Back
Top Bottom