Dunia inaniadhibu, nahitaji kuchukua maamuzi magumu

Pole sana Mkuu,Tambua kwamba nyakati ngumu marshani zipo. Husiikimbie familiya yako katika kipindi hiki. Nakushauri geukia masokoni tafuta pahali palipochangamka Anna kuchukua matunda uza na mengine kata uza ya vipande. Nyakati ngumu hazidumu mkuu.
Husilipie kodi hapo kwenye flemu, hiyo milioni moja sokoni ni kubwa.
 
Uwakala si lazima ukakae kwenye jengo hilo la kodi yote hiyo. Ondoka hapo kwanza tafuta mahala oengine ambapo hata kama ni meza utaweka utaendelea na mishe.

Kama umepanga nyumba, rudisha chumha ongea nanmzee kama vipi akuhifadhi kwenu (kama space ipo) wewe na mkeo. Mna mtoto mmoja hiyo fanilia hata sio kubwa kihivyo.

Ikishindikana , mwambie wife arud kwanza home kwao uangalie ustaarabu.

NAfasi ya mkeo kwenye maisha yenu ni ipi? Au yeye ni mama wa nyumbani? ????
 
Ndiyo mkuu yeye ni mama WA nyumbani darasa la Saba
 
Hiyo laki unusuulilewa ukaifata kwenda kujimwagia maji mengine hapo bar. Kama hiyo hela ni tatizo basi suluhu lake ni wewe Kukumbuka vizuri ukitumia na dem gan hapo bar akurudishie nusu
 
Pole sana ,.
Nimekusoma vizuri hayo ni mambo ya kawaida kwenye biashara sijasoma kuona una ishu ngumu ambayo ikufanye ufikirie kujuzuru ndugu cha msingi endelea kupambana.
Mara nyingi mwanzo ni mgumu sana
 
Mimi sioni hapo kama unatatizo saana zaidi ya kupoteza hiyo 150k. As long as ni mzima wa afya unaweza pata zaidi na zaidi ya ulichokipoteza.
Kikubwa tu usikubali pressure kutoka kwa huyo mkee wako ndio anakuharibu ujione kama umefeli sometimes wanawake ni wajinga wenyewe wanaropoka tu hawajui wanaume tunapitia nini.
 
Mzee naumia sana nakuonea huruma unachopitia miaka mitano iliyopita nilipitia hali kama yako.

Mimi mwenyewe nilitamani kukimbia familia lakini nilikaa na wife nikamwambia ukweli wa maisha.

Akakubaliana na hali akakubali kufunga mkanda. Tukavuka japo kwa mtiti na machungu makubwa.

Kwahiyo mimi nikushauri kaa na shemeji yangu( mke wako). Mueleze ukweli wote na anatakiwa akubaliane na hali na akubali kufunga mkanda .

Jamaa yangu maisha yako hivyo usikatetamaa na usiwaze kujiua. Ndugu matatizo tumeumbiwa sisi binadamu

Pole sana Mungu akupe nguvu na busara katika wakati huu mgumu unaopitia.
 
Hiyo laki unusuulilewa ukaifata kwenda kujimwagia maji mengine hapo bar. Kama hiyo hela ni tatizo basi suluhu lake ni wewe Kukumbuka vizuri ukitumia na dem gan hapo bar akurudishie nusu
Hapana mkuu jumapili sikurudi ofisini baada tofauti na mda ule asubuhi na Wala sikunywa pombe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…