Dunia inaniadhibu, nahitaji kuchukua maamuzi magumu

Jamaa anaomba chochote kitu nyie mnakazana kumlisha maneno😎

Destiny is all.

Amina kaka acha tupambane
 
Pole,wajuzi wa mambo wanasema.kimfaacho mtu chake,uza ulivyo navyo nenda kapange mahali unapopamudu,pia biashara za fremu achana nazo kama huna mtaji wa kutosha fungua hata genge ujitafute kwanza.
 
chukua familia yako nenda nayo kwenu huku wakati unajitafuta kuporomoka kwenye maisha ni jambo la kawaida kwa mwanaume
 
"Man is born to suffer ".... Aliyesema huu msemo hakukosea kabisa.

Mkuu cha kwnz ZINGATIA utulivu wa Akili

Cha pili kaa chini weka au panga upya mikakati ya kuanza chini

Accept kwamba Life will no longer be the same kama awali.

Kuna vitu lazima vitabadilika ki mpangilio but we kubaliana na yote

Ungekuwa upo dsm tungeunda umoja wa watu wanaopitia msoto mkali. Tupo wengi mkuu tunatofautiana scenario tu.

Usione tupo nyuma ya 🎹..., ukweli ni kwamba tupo tunapitia mengi mkuu acha tu
 
Kwanza hiyo pesa ipo humo ndani na ukitaka uipate Ina bidi ulewe Tena Kama mwanzo

afu uingie Kama unaficha hela nyingine hutaamini akili yako itakapo kuambia ufiche pesa kwa Mara ya pili ukiwa umelewa ndipo itakuwa ulii ficha hiyo hela ya kwanza. No Sha kutana na Hilo tukio
 
Acha pombe anza upya kuyumba kibiashara wewe sio wa kwanza kuna watu wakina sisi tulifilisika mpaka wake zetu wakatukimbia tukahama mji tukaenda kujitqfuta kwa hasira now tunarudi kwa kasi kwenye peak na tumesimika ngome tusije rudi tena kwenye msoto
 
Kwanza pole sana kwa hali ilokukuta, ila tuu kaa ukijua ktk hii dunia kila binadamu ana mtihani wake ambao hatokufa ila mtihani huo uwe umemfika na ukimfika anaangaliwa na Mola wake kuwa atautumia kumkumbuka na kumshukuru ama kumkufuru?. Yanayokukuta amin kwamba sio wewe wa kwanza na sio wewe wa mwisho, na Mungu hakupi mtihani ambao huwez kuujibu,
Kaa chini, tuliza akili na uangalie ulipotoka kwamba, je ulishawahi kukosea wapi? Huenda Mungu alishakupaga sana faida ktk biashara zako lakin pengine hukuwahi kutoa ZAKA (Kama wew n Muislam/Fungu la kumi (kama ww n Mkristo)) sasa ikiwa hukuwah kufanya hvyo basi ukae ukijua kuwa Mungu anachukua kwanguvu.
Lakin pia kama ambavyo umefanya maamuzi ya kuja JF kushirikisha Wadau madhila ulonayo basi fanya hvyohvyo kuwashirikisha Wazazi wako, hao wapo duniani kabla yako na wameona na kupitia mengi basi naamin hawatokosa ushauri wa dhahabu watakaokupa ambao utakujenga na kukuimarisha na hata kuvuka mtihani ulonao.
Usiikimbie familia, kwani wao ndio baraka ya wewe kupata riziki, matatizo hayakimbiwi ila unatakiwa kuyakabili.
Ahsante
 
Ndio ukubwa pambana
 
Sasa mkuu hata kama unakimbia umeshajipanga kwamba unakimbilia wapi na unaenda kufanya nini? Je, mke unamwacha wapi na unamwachaachaje? Usije ukakurupuka fanya huko kukimbia kuwe kwa utaratibu! Na kama uko mjini tafuta fundi ujenzi mzuri upige hata saidia fundi kwa muda angalau upate cha kushika hapo mjini mpaka hali itakapotengamaa!
 
Ndiyo mkuu yeye ni mama WA nyumbani darasa la Saba
Hata kama ni darasa la 7 bado ana mchango mkubwa sana ndiyo maana anafika mahali anakulaumu kwa nini hujaenda kazini! Ana dalili za upambanaji!
 
Kama umefeli kabisa rudisha mpira Kwa kipa,Rudi home Kwa wazazi kajipange Tena kiume,weka ubishoo pembeni piga vibarua kama ni kulima Lima sana!Mwisho kama ni muislam nenda masjid toa zaka au Kwa watoto yatima.Huo usenge wa kukimbia familia achana nao kabisa.
 
Yaani Kodi milioni 1 Kwa mwezi afu mtaji ni laki 3, au mi ndo nmechanganyikiwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…