Dunia tabu, duniani tabu haswa

Dunia tabu, duniani tabu haswa

Uwesutanzania

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2019
Posts
1,380
Reaction score
1,686
Ni mimi wako UWESUTANZANIA ✍️
Ngoja tuanze na Shahiri kwanza

Shahiri:
Dunia tabu,
Duniani tabu haswa,.
Ukiishi tabu,
Ukizeeka tabu haswa,.
Ukifa tabu,
Ukizaliwa tabu haswa,.
Ukiwa na mali tabu,
Ukiwa masikini tabu haswa,
Ukiwa wa kike tabu,
Ukiwa wa kiume tabu haswa,.
NA HATA USIPO ZALIWA TABU.

Mada yangu kwa siku ya leo ni
(NA HATA USIPO ZALIWA TABU)

Historia yangu fupi ni kuwa,

Baba yangu na mama yangu kabla ya kuzaliwa kwangu walikuwa ni wanandoa walioshindwa kupata mtoto kwa miaka mingi sana. Ni wastani wa miaka 17 na zaidi.

Jambo ambalo lililowakosesha amani kwa kipindi hiko.

Pamoja na kuendelea kudumu kwa kipindi kirefu chote hicho ila bado waliendelea kupambana kutafuta mtoto ''yaani mimi'', .

Basi waliendelea kupambana na kupambana mpaka walipopata MTAALAMU haswa wa maswala ya uzazi (NA HATA USIPO ZALIWA TABU),

Inaonekana ni kama vile nilianza kuona namna za tabu ya dunia zilivyo.

Basi mtaalamu akafanikiwa (KULETA TABU ) katika dunia (mimi), niliyokuja Kutana nao baada ya kuja sasa mh, Mungu mwenyewe anajua.

Mwisho wa hadithi fupi.

Ndugu yangu msomaji kama una matatizo ya uzazi basi nakuomba tafadhali usihangaike tena nakuomba sana kaa na kutulia upambane na tabu zako mpaka ufe peke yako.

Naongea kwa niaba ya UNAYETAKA KUMLETA TABUNI.

Asante
 
Back
Top Bottom