Dunia ya kufikirika, wanayoishi Yanga na GSM

Dunia ya kufikirika, wanayoishi Yanga na GSM

Johnny Sins

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2019
Posts
2,537
Reaction score
3,873
SAFARI ya kutoka Tabata, Mwananchi, hadi kufika maeneo ya Mbagala Rangi Tatu, ilichukua jumla ya saa mbili, hii ni kutokana na foleni za hapa na pale, nafanikiwa kufika mahali ninapoishi huku nikiwa nimechoka hadi unyayo, sikutamani kufanya chochote zaidi ya kuupumzisha mwili wangu.

Baada ya pilika pilika za mchana kutwa, nilijitupa kitandani na haikuchukua hata duru, tayari usingizi ukawa umetawala machoni mwangu. Nikiwa kwenye lindi hilo zito la usingizi nilijikuta nipo kwenye ulimwengu wa kufikirika, ulimwengu wa watu wa ajabu ambao sikuwahi kuwaona hapo kabla.

Mmoja wa watu hao ambao sikuwa nimfahamu. Nilimshuhudia akitoa kidaftari kidogo kisha akaanza kukisoma, baada ya kuanza kukisoma, nikagundua kuwa kilichoandikwa pale kilikuwa ni shairi moja ambalo lilihitaji ufikirivu wa hali ya juu, ili kuelewa kile ambacho kiliimbwa kwenye shairi hilo. Kwani lilikuwa ni shairi lililobeba mamilioni ya dhamira ndani ya herufi zake.

Alisikika akiimba hivi.

“Bora ningejua, yangu nisingekupa
Nimechomwa najua, nimekata yangu malapa
Nilipigana mchana, usiku nikakupa
Bora ningejua, yangu nisingekupa.”


Huyu aliyekuwa anaimba shairi hili tena kwa sauti ya kwanza anaonekana kuwa na wadhifa wa hali ya juu, lakini kwenye jezi aliyovaa kulikuwa na muhuri wa moto wa kampuni ya GSM.

Napata tabu kwenye kumtafsiri mtu huyu, juu ya mashairi aliyo yamwaga, lakini baadae nikaja kugundua kuwa huyu alikuwa ni mdhamini wa klabu ya Yanga ambaye sasa anajutia kwa kile alicho kitoa hapo mwanzo, sikukaa sawa mara likawasili kundi kubwa watu walio valia jezi za Yanga, macho yao yakiwa na rangi nyekundu kutokana na vilio walivyo angusha baada ya kumsikia mdhamini huyo katoka kaimba shairi hilo.

Walimsogelea na kuanza kumipigia magoti, wakimuomba kuwa asikate tamaa na kuchukua maamuzi ya kuwaacha pekee yao, kwani hawataweza kuhudumia timu yao bila yeye.

Baada ya kusikia kauli zile kutoka kwa mashabiki wale, moyo uliripukwa kwa mshangao, nikawa naanza kujiuliza maswali ambayo yalikuwa yanagoma kuleta majibu. Nilijiuliza hali hii itaendelea mpaka lini? Kwanini klabu zetu, zinaendelea kukubali tiba isiyotibu?

Nilichokiona kwa klabu zetu ni kuwa bado hazitaki kukubali hii ni 2020 na sio 1970, hawataki kukubali kwamba umefikia muda wa wao kuwa na uchumi imara na usio yumbishwa na mtu yeyote, hawataki kukubali kuwa kuna njia nyingi za mapato wanazoweza kuzitengeneza ukiacha kodi za majengo wanazozigombania.

Simba na Yanga ni miongoni mwa klabu kubwa kabisa kwenye Bara la Afrika, ni aibu sana kusikia timu hizi zinasujudia mtu mmoja au zinaishi kwa tabasamu la mtu mmoja.

GSM kama kweli alikuwa anataka aisaidie Yanga, kwanza angeanza kuwafanya Yanga wawe tayari kuishi bila uwepo wake, leo ameimba shairi tu imekuwa hivi je angepoteza maisha, wana Yanga mngemlilia nani, au mngeenda kulia juu ya kaburi lake?

Ifikie mahala, nyie mliopewa nafasi ya kuziongoza hizi klabu mjitafakari mara mbili mbili, kuwa mnatosha kuziongoza klabu hizi?

Kwa sasa hamuhitaji tena kuishi kwa kutegemea mfuko wa mtu, bali mnahitaji kuishi kwa kujitegemea wenyewe, na njia rahisi ya kuishi hivyo ni kukubali tu mabadiliko ya kiuendeshaji, mtoke hapa mlipo, mhamie sehemu nyingine, sidhani kama GSM ingekuwa imeweka pesa kama mwekezaji, mngekuwa kwenye hali hii kwa sasa.

Lakini hali hii inatokea kwakuwa mmekubali kuwa ili muishi lazima, mdhamini atoke na tabasamu nyumbani kwake.
Ghafla nikakurupuka kutoka usingizini, huku kijasho chembamba kikinitoka, nafungua dirisha naona tayari kumekucha nikajiandaa halafu huyoo, nikatimkia kwenye mizunguko yangu ya kila siku. Na nikaachan na hii ndoto ya GSM na Yanga.

Credit: Mwanaspoti

Rudi Nyumbani Kumenoga.
 
Vitu, vyote umevichanganya pamoja, GSM yupo Yanga Kama alivyo Taifa gas , sportpesa na maji ya afya.

Kila mdhamini kaweka pesa yake pale kwa mikataba tofauti huku Sportpesa wakiwa na fungu kubwa.

Jiulize kwann GSM , ndo anasikika zaidi yy kausogelea mpira wenyewe kawasogelea wachezaji, kawasogelea Makocha na matabibu.

Kakaa mbali na viongozi, haulizi mapato Wala nn? Yy anataka Brand yake ikue soko lake lipanuke kikwazo alichokiona ni timu iko legelege anatakiwa aiimarishe.

Viongozi wa kamati ya usajili wanajisikia vibaya , anaposajili bila kuwashirikisha. Sasa tupo Tanzania timu imechoka nauwezo wangu nasajili nyie pokeeni. Imewashinda jiuzuluni siyo kuanza majungu.

Mpira wetu mgumu Sana , mtu anayejitoa kuusaidia mpira wetu anapaswa kuungwa Mkono, sio kukatishwaa tamaa .

Ili mpira wetu ulipe inapaswa Serikali iuingilie mazima. Kama Sasa CAG alivyoingia, Logo za klabu ziheshimiwe.

Ili Mwekezaji naye arudishe kwa faida ya wazi, siyo Sasa hakuna faida ya wazi , anawekeza ili aibe .

Nakubaliana wawekezaji hawa wanapaswa wavisaidie vilabu hivi kwenda kwenye Mabadiliko, na ni kitu ambacho GSM anafanya . Hapo ndipo anapobidi kuungwa Mkono kwa nguvu zote.

Msingi mkuu wa Mabadiliko ni pamoja na kuwa na timu Imara.
 
OOOOOH WANGAA WABAYAAAA HAOOOO
AAAAAAHJHJ OOOOH .,..WABAYA HAOOO
 
Back
Top Bottom