Dunia yaenda kombo

Tamu3

Member
Joined
Feb 17, 2023
Posts
28
Reaction score
18
Ndimi mimi Kitumbika, mtunzi wa mashairi,
moyoni nafadhaika, kuitunza hii siri,
leo ndiyo natamka, nitasema sighairi,
dunia yaenda kombo, zichukuliwe hatua.

kuna vita kila kona, watoto wawa yatima,
kwa wakubwa na vijana, majumbani wamehama,
duniani wauwana, wanayumbishwa na vyama,
dunia yaenda kombo, zichukuliwe hatua.

inarindima mitutu, hofu imeongezeka,
imefanya hawa watu, wazidi kuhangaika,
na vita vikome katu, utulivu kujengeka,
dunia yaenda kombo, zichukuliwe hatua.

Denny Jeremias Kitumbika
mtunzi wa mashairi na ngano za Kiafrika
Mufindi Tanzania 19/11/2023

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…