Duniani nzima imetetereka leo kutokana na hitilafu ya mtandao kwenye kampuni ya Microsoft, Tanzania tumejifunza nini?

Duniani nzima imetetereka leo kutokana na hitilafu ya mtandao kwenye kampuni ya Microsoft, Tanzania tumejifunza nini?

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Tunategemea mambe mengi toka kwa Wazungu, leo mifumo ya Microsoft imesumbua mambo mengi yamesimama, wote wanaotumia products za Microsoft wametikiswa na suala hili, swali ni je, sisi wategema wa Wazungu tumejifunza nini?

Tunafanyaje kupata ujuzi huo na kuanzisha vya kwetu? Tuna program kadha wa kadha kupeleka wanafunzi na wataalamu wengine kujifunza mambo mbalimbali kutoka nchi za nje zenye utaalamu huo, upande wa digitali tunafanya nini?

Pia soma: Mfumo wa TEHAMA watetereka dunia nzima baada ya Kampuni ya Microsoft kupata changamoto kwenye mifumo yako

Tunapeleka wataalamu wa kutosha kwenda kujifunza kwa wajuzi ili nasi tuanzishe mifumo ya kwetu inayoendana na mazingira yetu? Wazungu wakizima vyao tuna mbadala wa kuweza kuendesha shughuli zetu? Tuna wezi wa kutosha wa kuiba maarifa ili kuendeleza vyetu?

Tusikomae kupiga kelele kufungia mitandao sababu ya mambo madogo madogo ambayo tunaweza kurekebisha, kuna mambo muhimu kama haya ya kutupia macho.

Pia soma: Threads: "Uvccm Waitaka Serikali Kuifungia X Zamani Tittwer"

Hii ni kengele ya kutuamsha sisi ambao bado tunachechemea. Nape (najua utapita tu huku) fanya jambo ukumbukwe hata kwa moja zuri, TCRA na nyie muelewe Digitali siyo adui yetu, tuitumie kuboresha vya kwetu.

Narudisha mpira kwenu wakuu
 
Mimi nadunda tu kama mnavoona hapa nagonga comments na likes za kutosha...
 
Kesho saa kumi Yanga anacheza na Augsburg timu kutoka Bundesliga Germany.
 
Back
Top Bottom