Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 51,303
- 40,190
Mkuu wangu JokaKuu, msome hapa chini kiongozi wenu Lema anawatoa wasiwasi kuhusu Zitto Kabwe...Zitto alipaswa kuwaeleza wana-Shinyanga ni jinsi gani ACT itaboresha sekta ya pamba.
..alitakiwa awaeleze ni jinsi gani ACT itawawezesha wachimbaji wadogo-wadogo wa madini tofauti na CCM inavyowakandamiza.
..angewaeleza ni jinsi gani ataboresha sekta ya ufugaji, ili wafugaji waweze kufaidika zaidi na mifugo yao.
..badala ya kufanya hayo Zitto anajielekeza kwenye siasa za chuki, fitina, na uchonganishi.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimewatoa hofu wanachama wake mkoani Shinyanga kikidai propaganda zinazoenezwa na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Bw. Zitto Kabwe, anayedai chama hicho kimepoteza mwelekeo si za kweli bali ni uongo.Mbunge wa Arusha Mjini ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa, Bw. Godbless Lema, aliyasema hayo hivi karibuni mkoani Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Mahakama ya Mwanzo.Alisema chama chao bado kipo imara na hakitagawanyika kama inavyodaiwa na Bw. Kabwe ambaye CHADEMA kilimfukuza katika chama baada ya kukisaliti hivyo kukiuka Katiba ya chama hicho."Ndugu zangu wana Shinyanga, CHADEMA tupo imara na tutaendelea kuwa imara hadi tukamate dola na kuwakomboa Watanzania ambao wanateseka tangu tupate uhuru."Zitto hana ubavu wa kukigawa chama chetu kama anavyofikiri na kuamini...anahangaika bure, alitaka kukiua tukamshtukia na mimi ndiye mtu wa kwanza kubaini njama zake na wenzake akiwemo Samson Mwigamba na Profesa Kitila Mkumbo; hivyo hawatubabaishi kwa lolote,"-alisema.Bw. Lema aliongeza kuwa, Bw. Kabwe alikuwa chanzo cha kufifisha ushindi wa CHADEMA katika baadhi ya majimbo katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 baada ya kutoa taarifa za uongo kwa wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo ya Katavi, Musoma Vijijini na Singida Mjini na kusababisha wagombea wa CCM wapite bila kupingwa.