Duru za siasa: Hotuba ya Jakaya Kikwete mwisho wa mwaka 2013

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
15,773
Reaction score
32,431
Wanajamvi,
Ifuatayo ni hotuba ya rais Jakaya Kikwete tarehe 31 December 2013
Yapo aliyoyajadili na tumekuwa na mijadala mingi kabla ya hapo.

Moja ya ijadala hiyo ni huu wa Mchambuzi na mingine mingi iliyopita kutoka kwa wanajamvi mbali mbali

https://www.jamiiforums.com/great-t...i-mazingaombwe-kwa-maskini-7.html#post7869284


Na ifautayo ni hotuba ya rais kama ilivyowekwa jamvini na @JF-forums ambayo ni text
Tuangalie hotuba hiyo kwa pamoja hasa maeneo yanayogusa maisha ya watanzania kama uchumi na kisha tuijadili
.


Katika hotuba hiyo sehemu inayozungumzia ujangili wa wanayamapori tumeijadili katika uzi ufuatao

https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/572764-duru-za-siasa-sakata-la-mawaziri.html


Hotuba inahitaji kuangaliwa kwa ujumla wake

Uhalifu:
Mh Rais amesema yapo mafanikio yanayotia moyo yaliyopatikana katika eneo hilo.
Tunafahamu kuwa uhalifu wa silaha, kumwagiwa tindikali, kulipuka kwa mabomu, kuteswa watu na kuuawawa kwa waandishi wa habari yamekithiri. Kibaya ni kuwa waliotenda hayo kama kulipua mabomu na kuumiza raia wengine hakuna aliyefikishwa mbele ya mkono wa sheria.

Rais amesema ''anaanda kikosi maalum cha kupambana na uhalaifu wa madawa ya kulevya''
Kwasasa kipo kikosi kama hicho ambacho kimeonekana kushindwa kazi, sijui kuanzishwa kwa kikosi kingine kutaleta utofauti gani na kile cha zamani.

Mh alipewa majina ya wauza unga hadi leo hakuna hatua, kikosi kingine kitafanya nini zaidi.

Rais ameonyesha takwimu za mwaka 2013 kuhusu madawa ya kulevya, hakueleza takwimu za mwaka 2012 kuhusu tatizo hilo kama alivyofanya sehemu nyingine kwa kulinganisha mafanikio.

Takwimu za mwaka 2013 ni kubwa kuliko za 2012 na hivyo kusema yapo mafanikio ni maneno ya kisiasa kwasababu takwimu zinapingana na kauli hizo ndiyo maana hakutaka kuzisema.

Mh Rais sijui ametumia kigezo gani kutenganisha uhalifu wa kuvunja milango na wa kalamu.
Wizi katika taasisi za umma ni wa kiwango kikubwa kama taarifa zinavyoonyesha.
Rais anaposema kuna mafanikio najiuliza ni yapi hayo.

Rasimu ya Katiba
Rais ameonya kuwa kama haitakubalika basi iliyopo itaendelea hadi tutakapopata mpya kwa muda mwingine.

Ninashawishika kusema kuwa anachojaribu kukisema ni kuwapa watu wasiotaka katiba mpya yenye masilahi yao kama CCM kupinga ili iliyopo iendelee.
Alichokisema ni ukweli lakini kwa kukisema ni kutoa 'mbinu' kwa wasiotaka.

Rais amesema, wajumbe wa bunge la katiba waweke masilahi ya taifa mbele na si yao.
Nadhani Rais angejiuliza mchakato wa kupatikana kwake uliwashirikisha wananchi?

Tuliwahi kujadiliana na kusema hatua muhimu ilikuwa kwa mchakato kupitia wananchi na serikali iweke mazingira mazauri ya shughuli na mshirika na isiwe ndiyo inaandaa katiba

Uwezekano wa wananchi au wajumbe kuikataa ni mkubwa kwa kuzingatia kuwa mchakato huo ilikuwa wazo katika jamii alilolichukua kama yeye binafsi tena bila kushirikisha chama chake.

Uwezekano wa wazo lake ambalo linaweza kuwa zuri lakini limefanywa vibaya kukataliwa upo na mwisho wa siku itabidi atawajibika na si suala la kusema atakuwa msoga

Uchumi
Mh kasema mapato yetu ya nje yamepungua mwaka huu kulinganisha na 2012 .
Hiyo imetokana na kupungua kwa bei ya mazao katika soko la dunia. Makakati anasema Rais ni kufufua viwanda ili kuongeza thamani za bidhaa

Hoja ya kufufua viwanda tumewahi kuizungumzia hapa ikiwashirikisha Mchambuzi na Zakumi kwa undani kabisa. Kinachoshangaza ni kusikia eti kuna mkakati wa kufufua viwanda.
Kwanza ujiulize viwanda vipi wakati ambapo Rais JK akiwa waziri na sasa Rais amesuhudia viwanda vikitolewa kama sadaka na kuwa maghala ya chumvi. Ina maana hakuona au hakujua!

Viwanda vyote vimebinafsishwa tena bila utaratibu na sasa ni magofu. Sababu zilikuwa kukaribisha wawekezaji ambao wamegeuza na kuwa maghala serikali ya JK ikishuhudia.

Sijui hili wazo la kufufua linalenga nini, je ni kuita wawekezaji au ni kuchukua maghala na kuyajaza mashine za kazi. Endapo ni hivyo, kwanini basi tulibinafsisha.

Je tunakwenda mbele au tunarudi nyuma? Kwanini miaka 10 tu tunakuwa na sera zinazotofautina katika jambo muhimu kama uchumi. Tatizo ni kukosa maono (vision) au kukosa wataalam au ni utashi wa kisiasa?

Mazingira ya uwekezaji


Itaendelea sehemu ya pili


 
Inaendelea..


MABADILIKO YA BARAZA LA MAWAZIRI

Ndugu wanajambi huu ni mwnedelezo wa hotuba ya mwisho wa mwaka. Tulisitisha majadiliano kutokana na matukio yaliyojitokeza tukisubiri pia mabadiliko yaliyotarajiwa ya baraza la mawaziri.

Mabadiliko yalitarajiwa kwa sababu kuu tatu
Kwanza, shinikizo la viongozi wa CCM kutaka mawaziri mizigo wapumzishwe
Pili, shinikizo la wabunge kutaka waziri mkuu aachie ngazi
Tatu, tukio la mawaziri 4 kujiuzulu kutokana na kashfa ya tokomeza.

Katika hatua isiyo ya kawaida mabadiliko ya mawaziri yametangazwa na katibu mkuu kiongozi ingawa rais amewaapisha siku iliyofuata.

Duru tunalitazama jambo hili kama woga wa rais kujibu maswali ya waandishi wa habari ikizingatiwa kuwa imekuwa ni kawaida yake panapokuwa na utata.

Rais anasema shinikizo la mawaziri kutoka kwa viongozi wa CCM akina Nape na Kinana halina maana kwasababu kushindwa majukumu ya uwaziri kunatokana na ufinyu wa bajeti.

Rais ambaye ni mwenyekiti wa CCM na CC ya alipaswa kuliona hilo na kulitolea majibu ndani ya vikao. Endapo huo ni ukweli kulikuwa hakuna sababu za kuita mawaziri na kuwahoji.

Kwasababu zozote atakazotoa ukweli unabaki kuwa Rais amewadhalilisha sana viongozi wenzake wa CCM. Leo Nape na Kinana wanonekana kama wanfiki na wambea mbele ya jamii.

Huko nyuma Rais alishawahi 'kumpiga' kibao Nape kwa hoja ya mafisadi.
Wakati Nape akitoa muda rais alisema hakuna muda hilo linashughulikiwa kichama.

Kuhusu kumuondoa waziri mkuu kama bunge lilivyopendekeza, rais amewachapa kibao wabunge kama alivyowachapa kwa suala la Jairo na Blandina Nyoni ambao wote 'wamesafishwa' Blandina akirudi kazini na Jairo akipokea mafao licha ya kukamatwa akihonga watunga sheria kwa fedha za umma. Ni utaratibu ule ule wa kumuokoa Luhanjo na azimio la bunge.

Kuhusu mawaziri waliojiuzulu, hilo keshalisemea wamewajibika kisiasa waliochini yao ndio wenye makosa. Rais ameliangalia suala hilo kama la mfumo akiwa mfanyakazi nambari moja na anayepaswa kutenda na si kulaalaika.
Kama mfumo ni mbaya nani anawateua makatibu wakuu na wakurugenzi?

Mabadiliko ya baraza la mawaziri hayakuleta lolote jipya zaidi ya kubadili mvinyo mbovu kutoka chupa moja na kuweka chupa nyingine na kuiita mvinyo mpya.

Katika mabadiliko yaliyofanyika yapo mambo yanayoshangaza na kuhuzunisha.
Yanaacha umma ukijuliza kama ipo seriousness katika kushughulikia matatizo ya nchi hii.
Watu wanajiuliza kama kweli tutamudu ushindani wa dunia, bara au kikanda.

Kwa kuangalia changamoto za hotuba ya mwisho wa mwaka na baraza la mawaziri duru za siasa ina masikitiko makubwa na nchi yetu.

Tuangalie 'suprise' za baraza

Inaendelea
 
Inaendelea

Katika mawaziri na manaibu yapo mabadiliko yanayosumbua akili na kufikirisha.
Waziri Kawambwa ameonekana kupwaya katika wizara anazopangiwa.
Wizara aliyo nayo ni uhai wa taifa na inahitaji mtu makini.

Tatizo la elimu limeongezeka kila uchao nchi yetu ikishika mkia katika nchi za ukanda huu.
Hivi kulikuwa na sababu gani za kuendelea kuwa na waziri anayefikiri kuongeza division za ufaulu!

Naibu waziri wa fedha Adamu Malima hajaonyesha chochote kusema anaweza kupewa nafasi nyeti. Sifa yake ni madudu ya Morogoro na kushindwa kuueleza umma nini kilitokea.
Ukisoma rejea za bunge huwezi kuona kama ana mchango wowote wa fikra chanya za taifa hili.

Mwigulu Nchemba, huyu ni mpiga kelele, kuchaguliwa kwake ni kuandaa mazingira ya upatikanaji wa fedha za umma kwa uchaguzi wa mwaka 2015.

Naye kama alivyo Malima hana lolote la kuzungumziwa zaidi ya matusi na kejeli.
Ni ngumu kuamini anaweza kukaa meza moja na wasomi wengine akaiwakilisha nchi yetu vema.

Waziri Hussein Mwinyi.
Alikuwa waziri wakati wa mabomu mara mbili. Amerudishwa kama fadhila kwa mzee Mwinyi. Katika hali ya kawaida hakufaa kuwa waziri kwasababu ya kuwajibika kwa makosa.
Ni katika wakati wake ndege za jeshi zilitua kuchukua wanyama.
Kwa uchache ni kuwa uwaziri wake unategemea zaidi mahusiano binafsi kuliko sifa

Waziri wa fedha Saada Nkuya.
Wizara ya fedha ni wizara nyeti katika uhai wa taifa lolote. Mawaziri wa wizara hiyo huitwa waandamizi. Yanapotokea yasiyotarajiwa waziri wa fedha au waziri wa ulinzi huweza kuongoza nchi, ingawa si sheria lakini ki seniority hilo ndilo lililo mbele

kiangalia hotuba ya Rais ya kufunga mwaka hapo juu, matatizo yanayolikabili taifa ni kuvutia wawekezaji ambako ni kwa kiwango duni sana dunaiani licha ya ziara zsisizoisha, Upanuzi wa miundo mbinu kama reli, upanuzi wa nishati na utoaji bora wa elimu na maji.

Yote yanategemea mapato ya taifa na wizara ya fedha ndiye mhusika mkuu.
Bajeti ya nchi inaandaliwa na wizara ya fedha pamoja na mipango yote ya nchi.

Ninaangalia huko nyuma nakuwaona watu kama akina Amir Jamal, CD Msuya, Kighoma Malima, Basili Mramba, Edwin Mtei halafu naangalia wasifu wa Saada Mkuya kama mmoja katika 'hall of fame'' nashindwa kuamini.

Naangalia CV za mwaziri wa fedha wa nchi za EAC pamoja na uzoefu wao na kuangalia CV ya Saada nashindwa kuamini kama kweli ninachikiona ndicho.

Saada hana wasifu wowote na pengine jana ndio wengine wameanza kumsikia.
Ni mchanga katika siasa, hana uzoefu wa kuongoza eneo kama wizara ya fedha na hata CV haionyeshi kuwa na mvuto wa aina yoyote kwa uchache wa kusema.

Sina uhakika na exposure yake katika mambo ya kimataifa, lakini nina uhakika huyu ndiye atatuwakilisha nje ya nchi iwe SADC, EAC Paris Club n.k.

Duru tukiangalia idadi ya wabunge hautuoni sababu za nafasi nyeti kama hiyo itolewe tu bila umakini wa aina yoyote. Ni dhahiri hakukuwa na vetting ya aina yoyote isipokuwa siasa tu.

Kuchaguliwa kwa Saada ni katika jitihada za kuwafurahisha waznz ili wajisikie kuwa wanauwakilishi katika JMT tukielekea bunge la katiba.

Kinachosahaulika ni kuwa JMT haigusi mambo ya znz ni hivyo uteuzi wa kisiasa namna hii unawaumiza Watanganyika kwa kutafuta tu umaarufu wa kisiasa.

Duru tunasema uteuzi wa waziri huu ni wa kusikitisha na kuhuzunisha.
Hakukuwa na kosefu wa watu wenye sifa wala uzoefu, kilichokosekana ni umakini na utayari ya kuyaangalia matatizo yanayolikabili taifa kama mifumuko ya bei, kupanda kwa gharama za maisha na kutafuta vyanzo vya mapato kwa umakini.

Hakuna ushahidi wa aina yoyote unaoonyesha utendaji wa Saada ambao ungeweza kumpa nafasi kubwa na nyeti katika taifa amsikini kama letu.

Hapa ndipo tunajiuliza kama kweli hotuba ya rais ilikuwa na maana ya kuzungumzia changamoto na suluhu au matarajio au ilikuwa porojo za kumaliza mwaka kama kawaida.

Endapo kungekuwa na umakini katika kuziangalia changamoto za hotuba ya rais, sidhani kama nafasi za uteuzi kisiasa kufurahisha watu zingepewa kipamumbele.

Duru tunasimama na kusema katika uteuzi wa waziri wa fedha, umasikini wetu si rasilimali au watu. Umasikini wetu ni kukosa uongozi. Ombwe la uongozi la serikali ya leo halina tiba.
Siyo tatizo la kimfumo au rasilimali, ni tatizo kubwa la uongozi wa nchi.

Katika nchi yenye maprofesa na wachumi waliobobea kama akina Mh Lipumba, kumchagua mtu asiye na sifa au uwezo ni kuliangamiza taifa licha ya ukweli kuwa kwa miaka 8 taifa limepoteza nuru, dira na uelekeo

Kwa mwendo huu wenzetu watazidi kusonga mbele sisi tukilalama wanatuonea.
Wanaduru, ningewasihi mpitie sifa na uzoefu wa mawaziri wa fedha wa Kenya, Uganda, Rwand, Burundi, Msumbiji, Malawi na Zambia kisha mje tujadiliane kama Saada alikuwa na nafasi yoyote hata ya unaibu.


Tusemezane
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…