Duru za siasa: Mbinu za ccm kuingiza katiba yao ya mafichoni

Duru za siasa: Mbinu za ccm kuingiza katiba yao ya mafichoni

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
15,773
Reaction score
32,431
RASIMU YA WARIOBA IMEANDIKWA KWA MFUMO WA SERIKALI 3
KUIFUMUA NI KUBADILISHA KILA KITU
MAMLAKA YA KUANDIKA RASIMU MBADALA YAMETOKA WAPI?

Bunge la katiba limeanza kuijadili rasimu kupitia kamati. Kamati hizo zimepewa vifungu viwili, cha kwanza na cha sita vinavyozungumzia muundo wa serikali.

Katika mazingira ya kawaida hiyo ingekuwa kazi ya kujadili na kupiga kura.
Kwa mbinu za Samwel Sitta na CCM, wameamua kuanza na vifungu hivyo ili wafumue rasimu ya tume kwa kupendekeza mfumo wa serikali 2 wanaoutaka.

CCM na Rais Kikwete wamehoji uhalali wa 'sample size' ya tume, wakisema watu 20,000 hawawakilisha maoni ya watu milioni 41. Upotoshaji huu haukuzingatia ukweli, hiyo ilikuwa sample size na kitaalamu inakubalika. Milioni 41 ni pamoja na vichanga na watoto.

Baada ya kuona kitaalamu hilo limeshindikana, CCM wamekuja na mbinu wakiwa wamejipanga ionekane maoni ya tume hayafai.

Kitu wasichoelewa ni kuwa tume ilipewa uhalali wa kisheria na maoni yake yamejengwa kwa msingi huo. Je, watakapobadilisha na kuweka kifungu cha serikali 2, nani amewapa mandate hiyo?

Kitaalamu wanataka kutuambia kuwa sample size ya watu 600 ni kubwa sana kuliko 20,000 na hivyo wana haki ya kuandika rasimu mbadala.

CCM wameshindwa kuelewa kuwa rasimu nzima ipo katika mfumo wa serikali 3, sehemu kubwa ikiwa ni ile ya shirikisho zaidi kuliko washirika wa muungano.

Mambo ya kawaida kama haki za binadamu, ukisoma yapo kulingana na mfumo uliotarajiwa.

Jaribio la kufumua rasimu litazua tatizo la rasimu nyingine ya watu 600 au chini ya hapo.

Mpango wa kuingiza rasimu ya CCM upo mbioni. Lakini je;

1. CCM itaweza kuingiza mfumo wao wa serikali 2 zikiwa na mabunge 3 bila tatizo?
CCM wanasema kutakuwa na bunge la Tanganyika kwa mambo ya Tanganyika.

Swali la kujiuliza hilo bunge la Tanganyika litasimamia serikali ipi?
Litaongozwa na kiongozi gani wa serikali asiye na uhusiano na serikali kuu?
Litahudumiwa na gharama za serikali ipi ikiwa tuna serikali ya JMT na SMZ?

2. Kwa kuangalia mabadiliko ya 10 ya katiba ya znz ya mwaka 2010, mapendekezo ya CCM yatafanyikaje? znz ni nchi, je, CCM itakuwa na uwezo wa kuwalazimisha wznz wakubaliane na kufumua katiba yao ili ikidhi mahitaji ya uwepo wa bunge la Tanganyika.
Je, kisiasa hilo litakubalika znz?

3. Malalamiko ya zanzibar ni hali ya Tanganyika kuvaa koti la Tanzania.
Kwa muundo wa CCM kuna uwezkano gani wa kuondoa hisia hizo iwapo kuna bunge la Tanganyika linalohudumiwa na JMT?
Hoja ya bunge la Tanganyika inajirudia hapa kwa kuangalia malalamiko ya wazanzibar pia

4. Malalamiko ya Tanganyika ni kubeba gharama kubwa za muungano.
Tume ya Warioba imepunguza mambo hayo kutoka 22 hadi mambo 7.

Hilo pia ni dai la znz kuwa mambo yameongezwa kinyemela. Kwa muundo uliokusudiwa na CCM, gharama za serikali ya JMT zitachangiwaje?
Na je mapendekezo ya CCM yatapunguza mambo chini ya yale 7 . Endapo haitawezekana, vipi suala la gharama kwa tume ya Warioba lionekane kubwa kuliko mapendekezo ya CCM

5. Rasimu ya Warioba inasisitiza uwepo wa chombo cha tatu cha sheria.
Endapo CCM watafumua rasimu ya Warioba, chombo hicho cha tatu watakiweka katika sehemu gani ya rasimu yao, na je huo si mwanzo wa kuandika rasimu mpya kabisa nje ya utaratibu?

6. CCM inapendekeza yawepo mambo ya muungano na yasiyo ya muungano.
Katika rasimu ya Warioba mambo hayo yametengwa kwa kuzingatia uwepo wa serikali 3, za washirika na ile ya pamoja.

Je, kwa muundo wa serikali 2 na bunge la Tanganyika, mambo yanayoihusu Tanganyika yatahudumiwa na serikali ipi? Na ni vipi mambo hayo yanaweza kutengwa iwapo hakuna serikali ya kushughulikia.

Hoja ya kuwepo kwa bunge la Tanganyika bila serikali ni uwepo wa mhimili mmoja ukiwa hauna washirika wake ambao ni serikali na mfumo wa sheria.

Vipi mambo yasiyo ya muungano yanaweza kushughulikiwa na bunge la Tanganyika bila uwepo wa serikali ya Tanganyika.

7. Kwa vile bunge la katiba linataka kufumua rasimu ya Warioba, ni vipi mambo yaiyoshindikana miaka 50 yanaweza kupatiwa ufumbuzi na watu 600 kwa siku 60?

8. Suala la mapato na mgawanyo wake litashughulikiwa vipi iwapo kuna Tanzania ambayo znz inadai imo ! Watanganyika watakuwa na amani gani juu ya mchango wa znz katika muungano, ikiwa miaka 20 hawajachangia chochote.

9. Masuala ya ulinzi na usalama ambayo Tanganyika iimeyabeba yatatafutiwa ufumbuzi gani ili Znz nayo ichangie bila kumtupia mzigo huo Mtanganyika?

10. Mfumo wa CCM unaopendekezwa umelenga nini? Kumaliza tatizo la malalamiko ya wazanzibar kwa kuwapa mamlaka zaidi, au kumaliza tatizo la Tanganyika kwa kubeba muungano peke yake au kuridhisha pande zote.

Kwa mfumo wa serikali 2 ni kwa njia gani hilo linawezekana bila upande mmoja kulalamika ima kwa kuonewa au kuumizwa.

11. Kama znz wana fiscal autonomy, mwisho wa autonomy yao ni upi ikiwa katiba yao ni juu ya katiba ya JMT. Na je, znz wapo tayari kurekebisha katiba yao ili kukidhi haja ya mfumo wa CCM. Ni kwanini tudhani znz inapaswa kuwa na fiscal autonomy na wala si Tanganyika.

Je, haki ya Mtanganyika kuwa na fiscal autonomy yao ipo wapi na kwanini Tanganyika isipewa autonomy kama mshirika wa muungano znz alivyopewa.

12 Endapo znz inadai historia na ulinzi wa rasilimali zake, hizi za Tanganyika nani ni custodian wake na kwanini historia na rasilimali za Tanganyika ziwe za Tanzania.

Wanaduru haya ni baadhi ya mambo tunayotakiwa tuyajadili kwa pamoja.
Rasimu ya CCM inayoingizwa kinyemela na Samwel Sitta si tu ni hatari kwa kustakabali wa taifa bali ni catalyst ya vurugu katika miezi michache ijayo.

Tafadhali pitia nyuzi zifuatazo kama sehemu ya mjadala huu.

https://www.jamiiforums.com/great-t...shaji-na-kiwewe-cha-kuzinduka-tanganyika.html
https://www.jamiiforums.com/great-t...a-katiba-je-katiba-itatokana-na-wananchi.html
https://www.jamiiforums.com/great-t...-gharama-za-muungano-siri-isiyozungumzwa.html
https://www.jamiiforums.com/great-t...ba-ya-jk-kuzindua-bunge-maalum-la-katiba.html
https://www.jamiiforums.com/great-t...asa-vijana-katiba-mpya-na-kiu-ya-uongozi.html

Tusemezane

cc JokaKuu Mwigulu Nchemba John Mnyika Mchambuzi Mzee Mwanakijiji Bongolander Mag3 Ngongo zumbemkuu Mkandara Mtanganyika Nape Nnauye Zakumi Mimi baba HKigwangalla Dr F. Ndugulile Anna Tibaijuka AshaDii Barubaru GHIBUU Pasco Ben Saanane Ritz
 
Last edited by a moderator:
Asante mkuu Nguruvi3 kwa kutufahamisha. lakini mpaka sasa bado sijaona hatua zozote zenye akili zinazoweza kuchukuliwa na kuacha serikali mbili zinazoweza kuzjibu malalamiko yaliyofanyiwa kazi na rasimu ya tume ya jaji Warioba.

Kama kweli CCM inataka kuleta serikali mbili tofauti na za sasa, basi zitakuwa ni serikali mbili ya Tanganyika na ya Zanzibar, ambayo itakuwa ni kunyume na spirit ya Muungano. Ina maana wanataka kuweka mazingira ambayo ni non accomodating na magumu zaidi.

Kama kweli kuna dosari za kiufundi za tume ya Warioba, kwamba haikufanya kazi ya kukusanya maoni ya wananchi kitaalamu, Mh Sitta amepewa uwezo gani wa kufanya kazi ya kukusanya maoni kitaalamu? au ndio itakuwa anapika facts ofisini na kusema ndio maoni ya watanzania? Sioni kama itakuwa ni jambo la busara Sitta na wenzake kubadilisha na kubananga maoni yaliyokusanywa kitaalamu, na kuleta mapendekezo ambayo yanalinda maslahi ya CCM na nradi wao wa serikali mbili.
 
Ahsantum Nguruvi3.

Hakika huo ni mtihani mkubwa sio tu kwa CCM bali kwa wananchi wa TGK katika kudai haki yenu ya kimsingi ya Nchi yenu. Tukumbuke kuwa HATIMA YA TGK YENU IPO MIKONONI MWENU NA SIO CCM. Inataka wananchi wawe na hari, moyo, uzalendo na Utaifa kudai haki ya nchi yao iliyyopotezwa kiainaaina na wanasiasa wachache. Ijulikane kuwa wengi watarubuniwa na hata kuhongwa sana kuikana TGK. Lakin uzalendo na utaifa ndio dawa pakee kwa wananchi.

Tukirejea kwa Upande wa Znz, mimi naamini wazi HAKUNA HATA KIONGOZI MMOJA WA KISIASA ATAKAYEWEZA NA KUTHUBUTU KUSIMAMA KATIKA MKUTANO WOWOTE ULE UWE WA NDANI AU HADHWARA NA KUSEMA ZNZ IBADILI KATIBA YAKE WANDIKE KUWA ZNZ SI NCHI BALI NI SEHEMU YA JMTz. Hilo haliwezekani as'lan abadan.

Na cha kufurahisha sasa katika mapendekezo yyaliyotolewa na kamati nyingi kwa upande wa Znz, wamesema ZNZ IRUHUSIWE KUJIUNGA NA TAASISI AU JUMUIYA YOYOTE ILE NDANI AU NJE BILA KUINGILIWA NA JMTz NA IMETAKIWA JMTz ITOE USHIRIKIANO katika kufanikisha. Hilo ni kuhalalisha kile kilio cha ZNZ CHA KUPATA MAMLAKA KAMILI NDANI YA MUUNGANO.

Tukumbuke kuwa hatima ya TGK ipo mikononi mwa waTGK na sio CCM.

L'jumaa kareem
 
Ulikuwa wapi muda wote huu? Hizi nondo za kutosha kabisa! Matumain yangu CCM wanaotembelea hapa watasoma na kutafakari na kisha kuwapasha wenzao. Hii mada umeiweka vizuri na ninaweza tu kusema HONGERA na ASANTE
 
Asante mkuu Nguruvi3 kwa kutufahamisha. lakini mpaka sasa bado sijaona hatua zozote zenye akili zinazoweza kuchukuliwa na kuacha serikali mbili zinazoweza kuzjibu malalamiko yaliyofanyiwa kazi na rasimu ya tume ya jaji Warioba.

Kama kweli CCM inataka kuleta serikali mbili tofauti na za sasa, basi zitakuwa ni serikali mbili ya Tanganyika na ya Zanzibar, ambayo itakuwa ni kunyume na spirit ya Muungano. Ina maana wanataka kuweka mazingira ambayo ni non accomodating na magumu zaidi.

Kama kweli kuna dosari za kiufundi za tume ya Warioba, kwamba haikufanya kazi ya kukusanya maoni ya wananchi kitaalamu, Mh Sitta amepewa uwezo gani wa kufanya kazi ya kukusanya maoni kitaalamu? au ndio itakuwa anapika facts ofisini na kusema ndio maoni ya watanzania? Sioni kama itakuwa ni jambo la busara Sitta na wenzake kubadilisha na kubananga maoni yaliyokusanywa kitaalamu, na kuleta mapendekezo ambayo yanalinda maslahi ya CCM na nradi wao wa serikali mbili.
Jambo la kushangaza ni kuwa CCM wanasema sample size ya Warioba haikutosha.
Tulitegemea wajadili uhalali wa sample size kabla ya kuanza mjadala.

Kwasasa kamati zinajadili sura ya kwanza na ya sita ya muundo wa muungano.
Wanajadili sura za rasimu ile ile wanayosema sample size haikutosha.
Kwamba, wanatumia udhaifu ule ule wanaousema kutengeneza kitu wanachodhani ni strong

Wanapaswa waamue kwanza kama sample size inakidhi uwakilishi wa wananchi.
Wakiona haitoshi hatua inayofuata ni kuvunjilia mbali maoni ya tume ya Warioba, kuomba serikali iunde tume nyingine na mchakato uanze upya.

Kitendo cha kutumia maoni ya sample size iliyopo na kubadilisha kwa kutumia watu 600 kama sample size ni uvivu mkubwa sana wa kufikiri. Sample size ya watu 600 imepata wapi mandate ya kuandika rasimu.
 
''MAONI YA WENGI, MAONI YA WACHACHE''
MBINU CHAFU ZA UPOTOSHAJI

Katika bunge la katiba linaloendelea, kamati mbali mbali zinatoa maoni kuhusu mitazamo yao.
Hadi majuzi ni kamati mbili tu zilizokuwa zimepata muafaka wa 2/3 kutoka pande zote.

Ni pande zote kwasababu Tanganyika haina mwakilishi, inawakilishwa na Tanzania ambayo znz ipo, huku Zanzibar ikiwa na uwakilishi wake.
Kwa mtazamo huo tu utaona jinsi ambavyo Watanganyika hawana mahali pa kushika au utetezi.
Muhimu hapa ni kuwa pamoja na mazingaombwe hayo 2/3 haikupatikana.

Kutopatikana kwa 2/3 kuna maana moja, suala la vifungu 'cha kwanza na sita' hayana ufumbuzi'
Katika kuliendesha bunge kibubusa busa Mh Sitta ameamua kamati zianze kuwakilisha maoni yao.

Kuna jambo watu wengi hawalioni kama upotoshaji. Kila anayesimama na kuwakilisha mawazo husema ''maoni ya wengi au maoni ya wachache'
Hii ni hila na mbinu ya CCM kuwalaghai wananchi kuwa kuna majority na minority.

Kwa taratibu za upigaji wa kura huwezi kusema maoni ya wengi ikiwa huna 2/3 kutoka pande zote. Kamati ambazo hazina 2/3 ya pande zote hazifai kabisa kusema kuna maoni ya wengi. Utakuwaje na maoni ya wengi wakati huna 2/3?

Mfano kama wajumbe wa 'Tanzania' wakiwa 30 na wakapiga kura na kupata 2/3 hiyo maana yake ni 20 kati ya 30.

Hawa hawatoshi kupitisha vifungu hadi wajumbe wa znz waridhie kwa 2/3.
Kama wajumbe wa znz ni 24, 2/3 yao ni 16 na hao lazima wapatikane ili kusema 'wengi'.

Hata kama wajumbe wote wa 'Tanzania wakikubali kwa ''3/3'' idadi yao ambayo ni 30 haiwezi kupitisha vifungu hivyo endapo ile ya znz ni 15 au chini ya hapo.

Kwa muonekano wa haraka 2/3 ya Tanzania inaweza kuwa nyingi, hiyo haifanyi 2/3 ya znz kuwa wachache.

Kinachoangaliwa ni 2/3, hata kama wznz katika kamati ni 9, 2/3 yao ni 6.
Hao wznz 6 wanaweza kukwamisha vifungu vilivyopitishwa na 3/3 ya 'Tanzania' ambao ni 30.

Siyo sahihi na ni upotoshaji wa makusudi kabisa wa kutumia lugha kwa kusema maoni ya wengi na maoni ya wachache.

Mkakati huu umelenga kuvunja nguvu za kisheria za 2/3 kwa neno 'wengi na wachache'.
Wananchi na wabunge wakatae hila hizo.

Kinachopaswa kusemwa ni hivi ' maoni ya kundi moja yanasema ABCD, maoni ya kundi la pili yanasema ABCD'

Nashangaa sana hata wale wenye hoja wanakubali kuitwa wachache wakati hakuna uchache.
Kwa kwamisha vifungu kwa 2/3 ni nguvu na wingi.

Narudia hata kama wachache wapo 6, 2/3 yao ni 4, hao ni sawa na 100 ambayo 2/3 yao ni 66. Hatuwezi kudharau hao 4 kwasababu kanuni zinasema lazima kupatikane 2/3 ya pande zote.

Hata katiba na ndani ya bunge la JMT, wznz ni 81 na 'Watanzania' ni takribani 240.
Sheria na kanuni zinasema, jambo la muungano lazima lipate 2/3 ya pande zote.
Haisemi wengi au wachache.

Sitta akiwa Spika hakuwahi kutumia neno wachache kwa wazanzibar ndani ya bunge la JMT, leo anaanzia wapi kama si ulaghai na hila zake akitumiwa na CCM.

Huu ni mtego wa kuonyesha umma kuna wengi na wachache wakati ukweli si hivyo.
Wajumbe kuweni macho.
 
RASIMU MBADALA YA CCM
TUELEZENI UNAFUU WA GHARAMA
KWANINI HAMKUWEZA MIAKA 50 NA SASA MNADHANI MNAWEZA
FUTENI RASIMU YA WARIOBA, MALIZENI MCHAKATO.
MAONI YENU YA WATU 300 KWANINI YAKIDHI TAKWIMU

Majadiliano yanayoendelea yamejikita katika kujibu rasimu ya Warioba. Majibu ni mepesi hayatoshelezi kina cha rasimu iliyopo. CCM wanachomeka rasimu yao, hatua za mwanzo ni kunyofoa kifungu cha 1 na 6.

Wazungumzaji waupande mmoja wametoa takwimu za maoni ya wananchi na gharama husika.
Tume inasema uwezekano wa kutenga mambo ya muungano na yasiyo ya muungano ni kupitia serikali 3

CCM wanasema wanataka serikali 2. Wasichotueleza katika rasimu yao inayoingizwa bungeni kinyemela ni mambo muhimu na mazito;

1. Onyesheni jinsi ambavyo serikali 2 zinapunguza gharama.
2. Tuelezeni vyanzo vya mapato vya serikali ya muungano, tofauti na vile vya Warioba
3. Tuelezeni, mumefikiaje hatima ya kusema wananchi wanataka serikali 2 (takwimu)
4. Tuelezeni katika malalamiko ya pande zote ni njia zipi mnashauri( yataje malalamiko na solution)
6. Ni namna gani katiba ya JMT itakuwa juu, ikiwa wznz hawataki katiba yao iguswe tena.
7. Tuelezeni 'wengi na wachache' wanawakilisha sehemu gani ya wananchi, takwimu zipi zinahalalisha hilo.
8. Tuelezeni bunge la Tanganyika linachaguliwaje, linagharamiwa na nani na linaongozwa na serikali ipi
9. Tuelezeni jinsi rasimu yenu inavyoondoa malalamiko kwa Tanganyika kubeba zigo, znz kuonewa
10. Tuelezeni hatari ya kuvunjika muungano inatoka wapi na kwasababu gani ambazo serikali 2 itazizuia.

Kwa vile mumeamua kufuta rasimu ya Warioba kinyemela, mtakimbia, hamtaweza kujificha
1. Kuitumia kwa namna yoyote ni kukubali takwimu zake na maoni ya wananchi
2. Kubadilisha ni kudharau maoni ya wananchi mliyoyakubali kwa kuanzia
3. Fungeni bunge, anzisheni mchakato upya. Watu 600 hawana mandate yoyote kutoka kwa wananchi.

CCM watueleze wapi tume ya Warioba ilikwenda kinyume na hadidu rejea zilizotolewa na Mwenyekiti wa CCM ambaye ni rais wa JMT.

CCM hii iliyopo madarakani iliamua mfumo wa vyama vingi in favor ya 21% ya waliotaka.
Tuambieni kipi kinapelekea leo CCM iwe na 'wengi wanasema, wachache wanasema'

Haiwezekani kukawa na bunge lisilogharamiwa. Bunge la Tanganyika linalokusudiwa na CCM litahudumiwa kwa vyanzo gani vya mapato na kutoka wapi. Nani atasimamia shughuli za bunge hilo lisilo na serikali na kisheria hiyo itawezaje kuingizwa katika katiba ya JMT.

Hao wabunge wa Tanganyika kupitia bunge la CCM wanapatikana kwa utaratibu gani. Gharama za kuchaguliwa kwao anazibeba nani. Uwakilishi wao ni kiasi gani, mambo gani wanapaswa kuzungumza ambayo ni nje ya muungano.

cc Nape Nnauye Mwigulu Nchemba Anna Tibaijuka @Dr F. Nsugulile

Last edited by a moderator:
Ahsantum Nguruvi3.

Hakika huo ni mtihani mkubwa sio tu kwa CCM bali kwa wananchi wa TGK katika kudai haki yenu ya kimsingi ya Nchi yenu. Tukumbuke kuwa HATIMA YA TGK YENU IPO MIKONONI MWENU NA SIO CCM. Inataka wananchi wawe na hari, moyo, uzalendo na Utaifa kudai haki ya nchi yao iliyyopotezwa kiainaaina na wanasiasa wachache. Ijulikane kuwa wengi watarubuniwa na hata kuhongwa sana kuikana TGK. Lakin uzalendo na utaifa ndio dawa pakee kwa wananchi.

Tukirejea kwa Upande wa Znz, mimi naamini wazi HAKUNA HATA KIONGOZI MMOJA WA KISIASA ATAKAYEWEZA NA KUTHUBUTU KUSIMAMA KATIKA MKUTANO WOWOTE ULE UWE WA NDANI AU HADHWARA NA KUSEMA ZNZ IBADILI KATIBA YAKE WANDIKE KUWA ZNZ SI NCHI BALI NI SEHEMU YA JMTz. Hilo haliwezekani as'lan abadan.

Na cha kufurahisha sasa katika mapendekezo yyaliyotolewa na kamati nyingi kwa upande wa Znz, wamesema ZNZ IRUHUSIWE KUJIUNGA NA TAASISI AU JUMUIYA YOYOTE ILE NDANI AU NJE BILA KUINGILIWA NA JMTz NA IMETAKIWA JMTz ITOE USHIRIKIANO katika kufanikisha. Hilo ni kuhalalisha kile kilio cha ZNZ CHA KUPATA MAMLAKA KAMILI NDANI YA MUUNGANO.

Tukumbuke kuwa hatima ya TGK ipo mikononi mwa waTGK na sio CCM.

L'jumaa kareem
http://www.habarileo.co.tz/index.ph...marekani-serikali-2-wazee-z-bar-wamfagilia-jk
 
KAMATI ZIMEKOSA 2/3, RASIMU INAINGIZWA KINYEMELA

Mbinu ya CCM ya kuunda kamati na kuwajaza CCM inaonekana kutokidhi mahitaji tarajiwa.
Mbinu hiyo ililenga kujaza viongozi wa kamati ili waingize maoni ya rasimu ya CCM kutoka mafichoni.

Kilichosahaulika ni uwepo wa factor mbili
1. Wale wanaotaka Tanganyika izinduke
2. Wale wana CCM wanaoutaka ukweli utamalaki
3. Wajumbe kutoka Zanzibar wanaotaka Tanganyika irudi.

Makundi hayo yameweza kuwa na ushawishi katika kamati na hata kufanya kamati zaidi ya 9 kati ya 12 kutokuwa na muafaka, kwa maana ya kukosa 2/3.
Lengo la CCM kwa kumtumia Samwel Sitta lilikuwa kutengeneza kamati ili zije ndani ya bunge zikiwa na 2/3 ya rasimu ya CCM na kurahisha kazi ya kuingiza rasimu hiyo bungeni rasmi.

Ukisikiliza maoni ya kamati zote, kile kinachoitwa 'wengi' ambacho ni propaganda za kuonyesha wengi wanakubaliana na serikali 2, yanafanana. Maana yake ni kuwa kamati zilikuwa na wajumbe wa CCM waliofundishwa namna ya kusema.

Tumemsikia mbunge kijana HKigwangalla akiwasilisha maoni ya kamati yake. Alichokisema cha kanza ni kuhusu mfumo dume na kutumia muda huo kuinanga kamati zingine kwa hoja hiyo.
Baada ya hapo akaanza kusoma maoni ya kamati ambayo basically ni maoni ya rasimu ya CCM ya mafichoni. Ndio maana tunjiuliza katika uzi huu
https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/637631-duru-za-siasa-vijana-katiba-mpya-na-kiu-ya-uongozi.html
kama vijana tuliona nao wanakidhi haja na tafsiri ya ujana kuliko wazee kama kina Warioba.

Kushindikana kupatikana kwa 2/3 kumemlazimu Samwel Sitta aruhusu kamati hizo zifikishe maoni yao kichovu chovu zikisaidiwa na hoja iliyobuniwa na CCM ya 'walio wengi' dhidi ya walio wachache.

Hii maana yake nini! Ina maana moja kubwa kuwa baada ya kamati hizo kuwakilisha maoni yao kitakachofuata ni kupiga kura ya wazi na siri. CCM wanataka kutumia kura ya wazi kuwaziba midomo wale wabunge wa CCM (kundi namba 2 hapo juu)

Na katika kuhakikisha wanawatia adabu wabunge wa CCM kabla mambo hayajaharibika, CCM na Samwel Sitta wataahirisha bunge kwa kile kinachosemwa ni kupisha bunge la katiba.

Ni wakati huo wa 'break' tutashuhudia wabunge wengi wa CCM wakipewa maonyo na vitisho ili wakati wa kura za wazi kuamua vifungu 1 na 6 wajirudi na kukubaliana na CCM.

Mbinu hii itafanikiwa kwa muda na kushindwa mbele ya safari kwasababu kuu mbili
1. Kitendo cha kuwatukana wazee akina Warioba na Salimu kinawagawa CCM katika makundi makubwa ambapo uasi wa wazi utatokea 'rebelion'

Uasi huo utawaunga mkono akina Warioba na wale wasiogopa CCM kama akina Lugola watapata kuungwa mkono. Kura ya wazi inaweza isitoe matokeo CCM inayotarajia.

Matatizo ndani ya CCM yanaonekana kwa sasa. Mitandaoni kumezuka kundi la watu wanaoleta uchonganisha kwa tume ya Warioba. Watu hao wametumwa na wazee ambao wapo nyuma yao.
Kwa kiasi fulani nii ni 'blessing in disguise' kwasababu mkakati utakufa kutokana na mtafaruku

2. Kundi la wabunge kutoka ZNZ litapata joto ya jiwe litakaporudi visiwani. Akina Shamsi Vuai Nahodha watapambana na nguvu ya wananchi.

Hoja zao za kutaka seikali 2 zina maana kuu moja, kuwa znz ibadili katiba yake ili kukidhi mahitaji ya serikali 2. Hilo litazusha mtafaruku mkuu si kati ya CUF na CCM bali CCM yenyewe kwa yenyewe.

3. Mparaganyiko wa makundi hayo mawili utaleta usaidizi kwa kundi namba 1 hapo juu.
Kura iwe ya wazi au ya siri bado 2/3 itakuwa mbali.

Option ya mwisho ni CCM kukubali rasimu ya serikali 3. Baada ya hapo watakimbilia kwenda kuwaghilibu wananchi wapige kura ya maoni ya kuzuia serikali 3 kwa kukataa.

Mbinu hii nayo inaweza kuwa na matatizo kama wale wanaotaka serikali 3 watasimama kidete kuitetea. Hoja kubwa ni kuwa ni hawa hawa CCM walisema vyama vingi vitaleta tabu, leo ni mwaka wa 20 hakuna tatizo. Hoja za fiscal autonomy itasaidia sana kujenga hoja zao hasa katika gharama,, mapato na matumizi

Hili suala la serikali ni jinamizi linaloishi nchini Tanzania. Inachokifanya serikali ya CCM ni kupulizia ubani kila linapoibuka. Lilianza na akina Jumbe, tume tano za Nyalali, Kisanga, Amina, Warioba na sasa Warioba tena. Kundi la G55 nalo lilikuwa na hoja hiyo hiyo.

Kubadili katiba ya znz 2010 ni matokeo ya jinamizi la serikali 3. Kushindwa kwa serikali ya Kikwete kutoa suluhu ni ushahidi jinamizi si tu kuwa lipo bali linazidi kuzaa watoto.

Ilipofika mahali suala hili linaongelewa wazi wazi tayari kuna sensitivityna kinachofuata ni curiosity. Mbinu za kuzima TV ya TBC haitasaidi katika zama hizi za mitandao. Tena zinazidi kujenga curiosity. Leo watu wanaitafuta hotuba ya Lissu wakiwa na shaka, nini serikali inaficha.

All in all serikali 3 ni jinamizi linalopaswa kukabliwa kwa hoja na si mbinu. Hadi sasa mbinu zinaelekea kugonga mwamba. Kinyume na hekima muungano utaifia mikononi mwa Kikwete si kwa hiari yake bali itabidi.

Tusemezane
Anna Tibaijuka Dr F. Ndugulile Mwigulu Nchemba Nape Nnauye HKigwangalla Bongolander Mag3 Mchambuzi zumbemkuu JokaKuu Ritz GHIBUU

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 07.04.2014
CCM MKOA WA SHINYANGA YA LAANI KAULI YA
MBUNGE WA JIMBO LA KAHAMA JAMES LEMBELI
KUWA "CCM SIYO MAMA YANGU"
Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga KIMELAANI vikali kauli ya Mbunge James Lembeli Mbunge wa Jimbo la Kahama aliyoitoa kwenye vyombo ya habari hivi karibuni iliyosema "CCM SIYO MAMA YANGU".
Kwa hiyo Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga na wana CCM wote kwa ujumla wamestushwa na kauli ya Mbunge Lembeli anayetokana na CCM kwani kauli hii hatukutegemea sote kama ingeweza kutolewa na Mwanachama ambaye tena ni Kiongozi ndani ya Chama.
Tunaomba ieleweke na tunautaarifu Umma na wana CCM wote kuwa CCM haina tatizo kabisa na msimamo wa Mbunge James Lembeli kuhusu msimamo wake wa serikali moja, mbili, tatu au nne na hata serikali ya Tanganyika kwani huo ni uhuru wake binafsi. Tatizo letu kubwa kwake ni kauli aliyoitoa kuwa "CCM SIYO MAMA YANGU" kwani kauli hiyo ameitoa sio mahali pake na haihusiki na utashi wake binafsi katika msimamo alionao katika BUNGE LA KATIBA. Kauli hii inaukakasi na ni sawa na kukinajisi Chama.

Taarifa hii imeandaliwa na Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga na imesomwa na:-

Ndugu Emmanuel S. Mlimandago
Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM
Mkoa wa Shinyanga
Kwa hisani ya AL truth (JF)

Bandiko la hapo juu tumezungumzia kutishwa kwa viongozi. Haya ndiyo yameanza.
 
1. Onyesheni jinsi ambavyo serikali 2 zinapunguza gharama.
2. Tuelezeni vyanzo vya mapato vya serikali ya muungano, tofauti na vile vya Warioba
3. Tuelezeni, mumefikiaje hatima ya kusema wananchi wanataka serikali 2 (takwimu)
4. Tuelezeni katika malalamiko ya pande zote ni njia zipi mnashauri( yataje malalamiko na solution)

Mkuu so far suala la Muungano ni gharama, ni gharama za idi kwa bara na kama kweli suala ni kupunguza gharama kuwepo kwa serikali tatu, kwa staili ya mapendekezo ya tume ya Warioba kutapunguza gharama. LAKINI inaonekana kuwa CCM wanataka kucheza na suala la gharama, hata kama kweli serikali 3 ni gharama ni sisi wananchi na sio CCM wanaogharamia, why worry? Ina maana mapesa tunayopoteza bara sasa kutokana na kuwa kwenye muungano sio gharama? Mamilioni tunayowalipa wabunge wanaohudhuria tu Dodoma, na wengine wenye vyeo vikubwa ambao kimsingi kazi yao ni kujaza nafasi na sio kufanya kazi?? Kwa hiyo ukiangalia utaona kuwa si suala la Gharama, it is much more than that.

Hiyo ya kukosoa sample ya tume ya Warioba naona ni kichekesho tu, kwa kuwa wanachofanya ni sample ambayo ni less representative kuliko ile ya tume ya Warioba, na ukiangalia upande wa vyama unaweza kuona kuwa CCM ndio iko represented zaidi kuliko vyama vingine.

Kwa maoni yangu ni kuwa malalamiko ya bara na ya Zanzibar hayatazingtaiwa hata kidogo kwenye hiyo rasimu ya CCM, isipokuwa malalamiko ya CCM will be well taken care of.

Mkuu hapa ni virugu tupu
 
Mkuu CCM wanazungumzia suala la gharama ili kuwatisha wananchi wasiojua.
1. Ukisoma maelezo au kuangalia video ya Ummy Mwalimu utacheka sana. Katika kamati yake (nadhani namba 2) anasema vifungu vyote vipo sawa sawa isipokuwa vile vyenye marginal note za shirikisho viwe muungano.
Halafu anakosa takwimu za Warioba kuwa zilikuwa na sample ndogo.
1. Kama takwimu zilikuwa na sample ndogo, iweje kamati hiyo isikatae rasimu yote bali penye neno shirikisho?
2. Kama sample ilikuwa ndogo, mbona kamati au CCM kwa ujumla haijaeleza kuhusu sample size inayotakiwa?
3. Kama gharama zitaongezeka, mbona CCM hawaonyeshi
a)Kwa muundo uliopo wenye wizara zinazoshughulikia muungano gharama zinapunguaje
b) Gharama kuongezeka kwa rasimu ya Warioba ni eneo gani na kwavipi zitaongezeka.

4, Wasichozungumzia ni kuhusu mambo 22 ambayo yakinyambuliwa ni zaidi ya 30. Mambo hayo yamepunguzwa, sasa gharama zinaongezeka kwa kupunguza mambo na si kuongeza?

Hili la gharama tuliwahi kuongea na Mkandara na Mtanganyika, tukawauliza watuonyeshe baada ya kuondoa mambo makubwa 15 gharama zitaongezeka vipi? Si wao wala Nape Nnauye au Mwigulu Nchemba wenye majibu.
Wanachokifanya ni kusema gharama zitaongezeka kwa asilimia 21 kwasababu tu wamesikia mtu akisema hivyo.

Well, kama zitaongezeka, hebu watuonyeshe ka mahesabu zinaongezeka vipi.

Katika kamati moja wamependekeza kuwa znz wapewe uhuru zaidi wa kukopa na misaada bila kupitia serikali ya muungano. CCM wanasema hilo liaondoa kero na kwamba znz ipewe fedha zaidi za maendeleo.

Wasichokisema ni kuwa fedha zinatoka wapi ikiwa znz haichangii muungano kwa miaka zaidi ya 20, inapewa pesa isizostahili kama msaada.

Kama kuna gharama basi kuongezeka kwakwe ni kwa upande wa znz ambao haukuwa na jukumu lolote katika mambo ya muungano. Utetezi wa kamati za CCM umelenga kuwapa pipi wznz ili wakubaliane na kile CCM inachokitaka.
Suala la gharama kalieleza vema Lipumba, na Kafulila kaeleza kwa upande wake.

Wasichokisema ni kuwa gharama za sasa zinahudumiwa na nani kiasi cha kudhani kuwa uwepo wa serikali 3 utaongeza gharama? Hawataki kukubali ukweli kuwa hilo ni zigo analobeba Mtanganyika na kwamba sasa ni wakati wa kulitua.
Kama wapo tayari znz kukopa na misaada, kwanini wadhani znz ambayo ni 'Hong Kong' ya Afrika inaweza kusimamia mambo yake kwa masuala 15 yaliyoondolewa

CCM ni wanafiki sana , hivi pesa zinazopotea kwa ufisaidi tena mafisadi wakiwa ndani ya bunge hilo ni kiasi gani kwamba haziwatii uchungu bali za serikali 3 zinaumiza wananchi kwa mujibu wao.

Kwa hesabu zozote za mtu aliyekwenda shule na shule ikamwelewa, serikali 3 zinapunguza gharama. Kwanini!
1. Tanganyika ikiwa na fiscal autonomy itaamua kila jambo bila kufungwa na uwepo wa znz
2. Znz ina fisacal autonomy ndio maana inaamua kuwa BLW liwe na watu 50, lakini wabunge wao watalii wanaokuja Dodoma wawe 81.

Hii ina maana moja, wao wana uchungu na mali yao, kwavile wanafahamu mazigo wa watalii 81 anaubeba Mtanganyika basi wapo tayari kuleta mabalozi wa nyumba kumi ili mradi kila mmoja apate ajira.
Mtanganyika ana disadavantage kwasababu analipia watalii na wala hana mahali pa kuhoji.

Utahoji vipi watalii wa bunge la JMT wakati nao ni Watanzania kama wewe?
Uyatima wa Tanganyika unasababishwa na kukosekana kwa mtetezi ambaye ni Tanganyika lakini amefungwa mikono na kamba za Tanzania. Leo tunaambiwa kulipia watalii 81 wanaokuja kupiga soga Dodoma siyo gharama.

Tunaaminishwa kuwa kulipia wanafunzi 1000 wa znz kwa jambo lisilo la muungano ni kupunguza gharama.
Tunaambiwa na CCM kuendesha muungano peke yetu kwa kodi yetu ni kupunguza gharama.

Haya yanaposemwa, wasomi akina Hkigwangalla wanapiga meza, masikini hawajui kuwa vyeo vyao ni vya muda lakini zigo la kulea znz ni la watoto wao. Hwajui kuwa huu ndio wakati wa kusaidia watoto wao, wanadhani watakuwa wabunge maisha yao yote.

cc Anna Tibaijuka , Dr F. Ndugulile HKigwangalla @Nape Nanuye Mwigulu Nchemba Mchambuzi Bongolander zumbemkuu @ Buchanan Pasco Chimunguru rev Kishoka
 
Last edited by a moderator:
MBINU YA HATI YA MUUNGANO YALETA WASI WASI KULIKO UKWELI
KWANINI ILIFICHWA HAPO AWALI?
KWANINI BUNGE LILILETEWA NYARAKA FEKI

Katibu mkuu kiongozi amezungumza na waandishi wa habari kuhusu hati ya muungano. Hii ni baada ya mjadala mzito ambao umeilemea serikali ya CCM.

Madai ya hati ya muungano ni ya siku nyingi. Yaliwahi kufikishwa katika mahakama kuu ya znz kudai nyaraka hiyo. Hili ni jambo zito ambalo serikali na Rais walipaswa kulitolea ufafanunuzi mapema.

Kwanini wamechelewa kiasi cha kutoa maelezo kupitia katibu mkuu baada ya shinikizo?

Kwanza kabisa, serikali ilipaswa iombe radhi wananchi kwa kitendo cha kupeleka hati feki na kughilibu umma.

Hata hivyo hati iliyopelekwa ilikuwa sheria na si hati na hivyo kuna jambo la kujiuliza, kwanini serikali kwa kupitia Samwel Sitta iliamua kufanya 'uhuni' wa aina hiyo. Nini kinafichwa.

Leo balozi Sifue hakuomba radhi na hivyo kubariki feki iliyopelekwa bungeni.

Samwel Sitta alidai waliofanya ni watumishi wa bunge akiataka kuitetea serikali.
Leo kama zilivyo siku nyingine amebaki 'uchi' kwasababu serikali ya JK imemruka kimanga.

Maelezo ya watumishi wa bunge yanatatanisha. Katibu wa bunge maalum alikaririwa akisema hati hiyo haipo umoja wa mataifa.

Waziri kiongozi wa znz Nahodha akasema hajawahi kuiona.
Akatokea kiongozi mwingine na kusema ipo Ikulu.

Kwa nyakati zote hizo serikali ilikuwa imekaa kimya, leo akina Lissu wamefumua bomu serikali imekurupuka na kuonyesha hati hiyo.

Swali linalokuja, je hati hiyo ni kweli ni ile iliyosainiwa?
Na kwa vipi wananchi waamini ikiwa serikali hiyo hiyo inayotoa hati ndio ilishiriki kupeleka hati feki bungeni?

Nani ana imani tena na hati hiyo ambayo inaonekana kufichwa na kuchezewa hovyo bila haya.

Swali linakuja, je wana ushahidi hati hiyo ilisajiliwa UN na lini ilifanyika hivyo?
Zaidi ya hapo, je waliwahi kujibu telex iliyoumwa kutoka UN kuhusu hati ya muungano?

Serikali imekurupuka baada ya kubaini mbinu zinazidi kuisha na uwezekano wa muungano kuvurugugia mikononi mwa JK ni mkubwa.

JK ajilaumu, haya ndiyo mambo alipaswa kuzungumza katika hotuba yake kwa unyeti na yanavyoligusa taifa.

Kitendo cha kumshambulia Warioba na kuacha mambo mazito sasa kinamrudi. Analipa gharama kubwa kwa jambo ambalo kama angekuwa makini lingeshamalizilka.

Hili ni jinamizi na sasa lipo mtaani. Itahitaji nguvu kuaminisha umma kuwa nyaraka hiyo ni halali, ilisajaliwa UN, na hakukuwa na kughushi kama ilivyokuwa ya kwanza.

Kwa hali ilivyo CCM wapo on defensive position, mbele ya safari mbinu zitakwisha utabaki ukweli.

Yes, watatumia tume na fojari wakisaidiwa na polisi, hata hivyo hawataweza kuuzuia ukweli.

Wata ahirisha matatizo tu kwa kuwatumia akina Sitta ili watakapokuwa wamestaafu mzigo huo ubaki na wanaotaka uongozi kama akina Sitta.
 
Kwa jinsi hali inavyoenda, bunge la katiba litaishia kurekebisha katiba ya JMT (1977) badala ya kulipatia taifa katiba mpya. Hii ni kwa sababu, msingi wa katiba ya JMT (1977) ni mfumo wa serikali mbili, baada ya msingi mwingine (mfumo wa chama kimoja) kubomolewa miaka ya tisini kufuatilia mabadiliko ya katiba yaliyotokana na kazi ya tume ya nyalali. Kitendo cha CCM kupangua Sehemu za Kwanza na Sita za ibara kwa nia ya kulinda serikali mbili, maana yake ni kwamba kinachofanyika ni maboresho ya katiba ya JMT (1977), katiba ambayo imekiuka mkataba wa muungano (1964). Katika mazingira haya ya maboresho ya katiba ya JMT (1977) badala ya katiba mpya, lengo la kuleta hati ya muungano ambayo imekiukwa na katiba inayolengwa kuboreshwa, lengo ni nini?

Na kwanini bunge la katiba limepoteza miezi miwili (milioni kumi na nane za posho kwa kila mjumbe, kwa wajumbe 600, trillioni moja?) Kufanya kazi za bunge la jamhuri ya muungano (constitutional amendments) badala ya kazi ya constituent assembly (kuandika katiba mpya)? Ni ccm hao hao ambao wanasema serikali tatu ni gharama. Shillingi bilioni nane pia zimepotea katika modifications za ukumbi wa bunge kukidhi matumizi ya BLK.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
........
Mchambuzi;9273912]..............

Mkuu Mchambuzi , CCM haina maadili ya kiroho ya kuzungumzia gharama.

Gharama zilizotumika kuunda tume(zaidi ya 8) ni nyingi sana bila mafanikio ya utekelezaji.
Gharama zinazotumika sasa hivi ni za Tanganyika ambayo kutokana na kufichwa kwake inatumiwa kudanganya Tanzania.

Lengo kuu la kuleta mkataba wa muungano limetokana na mambo mawili.
1. Shinikizo la uhalali wa muungano, wengi wakiamini haukuwepo kutokana na usiri uliokuwepo
2. Kujenga uhalali wa muungano wa mwaka 1964, katiba ya 1977 haina uhalali hata mbele yao.

CCM wanatumia mkataba wa mwaka 1964 wakichagua vipengele ili kuonyesha msingi wa muungano ulikuwa serikali 2

Kwa mfano, wanasema Tanganyika ilitoa mamlaka yake kwa JMT na znz ika retain baadhi.
Hadi hapo wanajenga hoja huo ndio msingi.
Kwavile wengi hawasomi mambo kwa weledi, wanaishia kuamini hivyo.

Wasichosema ni kuwa mkataba ulikuwa wa nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar na kulikuwa na kipindi cha katiba ya muda, katiba ya mpito n.k. ambavyo vilipaswa kujadili kwa undani mkataba huo. Hawakumbuki kuwa Tanganyika ilifutwa kwa amri ya Rais na si mamlaka ya wananchi na kwamba hilo halikuridhiwa na upande mwingine.

Mwaka 1977 wakaamua kuandika katiba wakati huo kukiwa na mchanganyiko wa mambo na kufanya wananchi na wajumbe wasahau kuwa kuna mkataba wa muungano. Mawazo ya wengi yalikuwa kuungana kwa TANU na ASP

Lakini pia wanataka kutumia mkataba kuonyesha kuwa Warioba na tume wamechakachua kwa kuwabambikizia mambo.

Wanachotaka kufanya ni kurekebisha katiba ya mwaka 1977.
Samwel Sitta kwa kutumiwa na CCM makusudi meanza na kifungu cha 1 na 6 ili kufumua mfumo uliopendekezwa.

Laiti vifungu vingekuwa na hoja ya serikali 2 tumeshapata katiba ya CCM wanayoitaka.

Tatizo ambalo Sitta amekosa busara nalo kwa unafiki ni kuwa rasimu yote imeandikwa kwa kutumia mfumo wa serikali 3.

Ili iwezekane kufanya hivyo ni lazima rasimu yote iliyotumia mabilioni ya pesa ifutwe kwanza na katiba ya CCM ya mafichoni iingizwe.
Hakuna namna itakayowezesha hilo lutokea kwa muda mfupi.

Kwa mantiki ya muda kuwa mfupi, Samwel Sitta ameomba kuongezewa muda.
Hii ni kutambua ukweli kuwa lazima rasimu yote ya Warioba itafumuliwa.
Hilo hawalioni kama gharama, wanaona gharama za serikali 3 bila kutuonyesha ni zipi.

Leo wanaomba gharama wakati Mwigulu Nchemba ametumia muda wake kutoa matusi, hilo hawalioni kama gharama.Leo tunalipa deni la Dowans CCM haioni kama ni gharama hata kama hatutumii umeme.

Nimemsikia mama Anna Tibaijuka ambaye ni member mwenzetu akisema serikali 3 zitakuwa na tatizo la kuendesha serikali kuu kwavile haina chanzo cha uhakika cha mapato.
Nimemuuliza mama Tibaijuka, hivi kwa sasa chanzo cha uhakika ni kipi?

Je, mama Tibaijuka, kukubalia gharama za muungano azibebe mtoto, mfanyakazi na mkulima wa Tanganyika ndiko kupunguza gharama za muungano?

Mama Tibaijuka, gharama za muungano si kero muhimu kwa upande wetu Tanganyika? Mbona hilo hamuliongelei?

Mama Tibaijuka, kwa uwepo wa katiba ya znz ya mwaka 2010 mnawezaje kuwa na serikali 2 mkaondoa mkanganyiko uliopo?

Mama, hivi inawezakanaje kuwa na serikali 2 mkaondoa ubaguzi unaoonyeshwa na wznz?
Leo mumetoa ajira asilimia 21 kwao, mtoto wa kitanzania ataweza kupata kule kwao?
Wao wanapokuja bara wanakuja Tanzania, Mtanganyika akienda kwao ni Mtanganyika.
Ninyi wa serikali 2 mumejipanga vipi kukabliana na ubaguzi huo?

Nikamuuliza tena, vipi wanaweza kuwa na mambo ya muungano na yasiyo ya muungano kwa mfumo wa serikali 2 ulipo?

Mama Tibaijuka, kwavile ni mwenzetu na sisi tupo njia panda tnakuomba uje hapa utusaidie ili tuelewe tusipopaelewa.

Yes, watafanya kila mbinu na watafanikiwa. Jambo wasilolijua ni kuwa 'beyond yield point' kitu kinavunnjika.

Ipo siku ambayo si mbali wananchi watachukua hatima ya nchi yao.
Watachukua kwa njia zipi linabaki kuwa ni kitendawili.
Kwasasa wananchi wamechoshwa na uhuni, kizazi hiki si cha mwaka 1950,1960 hiki ni millennial generation. Hatima ya taifa ni haki ya kila mmoja

Anna Tibaijuka HKGwangalla Dr.F. Ndugulile Zitto Kabwe John Mnyika Mwigulu Nchemba
 
Last edited by a moderator:
........ Mkuu Mchambuzi , CCM haina maadili ya kiroho ya kuzungumzia gharama.

Kilicho dhahiri sasa ni kwamba kinachoendelea Dodoma na kitakachofanyika hadi mwisho itakuwa ni marekebisho na maboresho ya Katiba ya JMT (1977), sio utungaji wa katiba mpya. Mwanzo mjadala ulianza kwa ccm kulazimisha kwamba kazi ya bunge la katiba ni pamoja na kuondoa au kufuta vifungu vya kwenye rasimu. Na hicho ndicho kinaendelea, na kama ulivyosema, wameanza na sura za kwanza na sita za rasimu kwa lengo la kuondoa yote yaliyomo. Msingi wa rasimu ni hiz sura mbili, na msingi wa katiba ya JMT (1977), ukiondoa chama kimoja cha siasa, ni serikali mbili. Usanii unakuja hivi:

*Kitendo cha ccm kulazimisha na kuhodhi BLK maana yake ni kurudisha nchi kwenye katiba yenye mtazamo wa chama kimoja. Hii ilikuwa nguzo ya kwanza kati ya mbili za katiba ya JMT (1977).

*Kitendo cha Ccm kulazimisha serikali mbili ziendelee, ni kuua kabisa rasimu hivyo kushindilia nguzo ya pili ya katiba ya JMT (serikali mbili) kwa zege .

Na haya yalikuwa dhahiri pale JK nadhani alipokuwa Mbeya alipotamka kwamba katiba iliyopo itaendelea kutumika iwapo BLK halitafikia muafaka. Sasa tunabaki kujiuliza - kwanini fedha za walipa kodi zimepotea kuendesha bunge kwa mtindo wa maboresho badala ya kazi hiyo kufanywa tu na bunge la JMT? Nia ilikuwa nini hapa? Zaidi ya bilioni nane zimeenda katika kurekebisha ukumbi wa bunge, ili wabunge waje kufanya kazi ya bunge la Jamhuri ya Muungano (mabadiliko ya katiba) na sio kazi ya bunge la katiba (kuandika katiba mpya)? Hii ni ajali au ilikusudiwa? Ndio swali lako Nguruvi3 kuhoji moral authority ya CCM kujali gharama linapokuwa na uzito.

Wajumbe wa BLK wamekaa zaidi ya siku sitini kwa ajili ya maboresho?? Siku sitini mara laki tatu (posho) ni milioni kumi na nane wa kila mjumbe. Ukizidisha mara wajumbe mia sita, ni shilingi Trilioni MOJA. Na hapo kazi haijaisha. Halafu watu wanajifanya kupata maumivu na gharama. Hatua ya Mwigulu Nchemba kuzuia posho za ukawa haina maana kwamba ana uchungu na fedha za walipa kodi bali anataka warudi kufanya kazi ambayo sio yao bali ya bunge la JMT (marekebisho ya katiba iliyopo). Itakuwa ni ajabu sana iwapo ukawa watarudi mle kichwa kichwa.

Mama Anna Tibaijuka ni mchumi mzuri, lakini katika hili, ameamua kujiingiza katika political mobilization badala ya economic rationalization. Hivi mama yetu haoni kwamba gharama kubwa za kuendesha serikali zinasababishwa na wao kukumbatia ufisadi na wizi wa mali ya umma? Hivi haoni kwamba mfumo wa serikali tatu msingi wake ni kupunguza gharama? Haoni kwamba kwa sasa baraza la mawaziri lina watu 61, wabunge 450? Haoni jinsi gani idadi hii itapunguzwa na serikali mbili?

Mwigulu, Yeye, JK na wengine wanapata wapi hoja kwamba serikali ya muungano haitakuwa na mapato ya kujiendesha wakati wataalam wa kodi toka TRA wameainisha mapato ya Muungano, mapato ya Tanganyia na mapato ya Zanzibar?

Sijui ni kwa sababu gani wenzetu hawa wanashindwa elewa kwamba hatuwezi kuwa na muungano na kuwa na nchi moja wakati zanzibar inajitambua kikatiba kama "nchi". Muungano utakuwepo iwapo Zanzibar itarudi ilipotoka au Tanganyika itazinduliwa. Zanzibar kurudi ilipotoka kwa kulazimishwa na CCM ni gharama kubwa kuliko Kuizindua Tanganyika.

Mama Anna Tibaijuka, Mwigulu Nchemba, Nape Nnauye, na hata JK, nje ya kurudi ilipotoka au kuzindua Tanganyika, msubiri tu kutafunwa na dhambi ya kuvunja muungano. Tutawakumbusha.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Ndugu wanajamvi

Tumeeleza mara nyingi jinsi CCM inavyojitahidi kuingiza rasimu yake kwa hila.
Tumeeleza sana kuwa kinachojadiliwa sasa ni namna ya kuwapendeza wznz kwa gharama za Mtanganyika.

Hakuna hata mmoja anayefikiria madhila ya kutokuwepo kwa Tanganyika katika watu wa serikali na bunge.
Na kwavile Tanganyika haipo, hakuna wa kumtetea Mtanganyika. Kinachobaki ni kuwa shamba la bibi.

Leo Hawa Ghasia anasema faida za benki kuu zitaongezwa kwa znz kutoka 4.5 kwenda katika kiwango alichogoma kukisema. Akasema mfuko wa pamoja wa pesa za muungano mchakato wake umeshaanza na kwamba katiba ya CCM inayoandaliwa Dodoma itauweka.

Hii ina maana moja kuwa viongozi wa bara watafanya kila jambo kuhakikisha kuwa wanaiuza Tanganyika simply wanataka madaraka. Mathalan, miaka 50 haikuweza kutatua kero, miaka 8 ya Kikwete haiukuweza kutatua kero. Tume zaidi ya 10 hazikufanyiwa kazi mapendekezo yake.

Leo baada ya Watu kudai haki ya serikali yao ya Tanganyika ili kusimamia masilhi yao ya Tanganyika, serikali imeweza kuondoa kero 50 na kwa mujibu wa Samia na Ghasia sasa zitakuwa zimebaki kero 2.

Hakuna mtu anayezungumzia kero za Tanganyika kama kubaguliwa znz, Kuvunjwa kwa katiba na znz kutochangia muungano, kinyume chake inapitisha madeni yake kwa JMT ili Mtanganyika asiyeijua wa manyoni au Ukiliguru alipe gharama.

Ni kwa kutumia gharama za muungano ambazo mbali ya bajeti kuna fursa na mapesa mengi, Mtanganyika atazidi kuvunja mgongo katika kodi. Kwa mwendo wa zawadi na pipi huenda miaka 2 ijayo wznz hawatahitaji kufanya kazi kwasababu gharama zao zinalipwa na Mtanganyika.

Mkumbuke kuwa ili mznz aweze kukubagua vizuri, ukiwa znz hujulikani kama Mtanzania wanakuita Mtanganyika.

Inavyoonekana baadhi ya Watanganyika hasa wenye nafasi serikalini wameamua kuuza nchi kwa vile wao future ya vizazi vyao imeshakaa sawa.

Wewe unayelipa kodi ambayo hataitumia mtoto wako hata kupata mkopo wa elimu ya juu lazima ujiulize, ni kwanini ulipe kodi kwa ajili ya nchi jirani?

Mtoto wako anapokosa mkopo kwasababu nafasi yake imechukuliwa na mwanafunzi wa nchi jirani ya znz ambaye baba yake hajui kodi, unajisikiaje? Unamtendea haki mwanao?

Katika mambo yote hakuna hata moja kama la kuvunja katiba ambalo limejadiliwa.
Maana yake ni kuwa watu wakae kimya znz ikivunja katiba.
Licha ya zawadi wanazopata kutoka JMT kwa free ride bado hata katiba wanaruhusiwa kuichezea.

Leo wznz wa baraza la wawakilishi wana uwezo wa kuzuia haki zako bila kuulizwa.
Hii Tanganyika lazima ipiganiwe.

Tunarudia ipo siku watu watakaa vibarazani wakicheza bado na wakaleta madai ya kununuliwa chakula na Mtanganyika. Na mtafanya hivyo kwasababu laiti watu wangejua namna gani deni la taifa linavyowaumiza,, namna gani kodi zao zinavyotolewa kama sadaka kule znz, leo tungekuwa na lingine la kuongelea.

Bado duru za siasa tunaonya kuwa nje ya utaratibu, ni sheria za mitaani zitakazotumika.
Kutakuwa hakuna law and order, wananchi wataitaka nchi yao.

Ipo siku watu watachoka na dhalili hii, watachukua hatua mikononi na muungano utaisha kwa fedheha na majonzi makubwa. Hatari hii kwanini watu hawaioni?
 
ILE RASIMU YA CCM YA MAFICHONI SASA HADHARANI
TUKIWATAJA HADI WAHUSIKA, TUKAAMBIWA TUNATUMIA POBABILITY
MAJIBU YAMEPATIKANA, HATUNA HATIA NA KILICHOSEMWA IMETOKA

Katika uzi huu tulieleza uwepo wa rasimu yaCCM ya mafichoni. Tuliwataja akina Chenge, Migiro na wengine kama wahusikawakuu wa rasimu hiyo. Bunge la CCM Dodoma limethibitisha pasi na shaka uhusikawa watu hao

Kwanza, wote walikuwa katika kamati yauandishi wa rasimu. Na kutokana na kuchukua rasimu ya CCM na kuigeuza kama yabunge lao, mwanasheria mkuu wa znz akasusia uwepo ndani ya kamati.

Yaliyomkuta kutoka CCM znz ilikuwa tishiola kibarua chake. Ni kwa uhakika kabisa mwanasheria huyo alijiridhisha kuwakatiba ya CCM inayopendekezwa itakuwa na mgongano mkubwa na ile ya Zanzibar yamwaka 2010

Katiba ya znz inasema ili mabadilikoyafanyike ni lazima kuwepo kwa kura ya maoni. Hilo tu linaonyesha kuwa mgogorowa mgongano wa katiba za JMT nah ii ya CCM ya Sitta na ile ya SMZ utaendeleakuwepo.

Na katika kuonyesha kuwa rasimu ya CCMiliibuliwa na waliotumwa, katika kamati ya maridhiano ya bunge la Sitta, walewale tuliowataja kuwa na rasimu ya mafichoni ndio wahusika tena.

Hii maana yake ni kuwa akina Chenge naMigiro walipewa dhamana ya kuandaa katiba ya mafichoni na ni wao wanaowezakuandika(uandishi) au kuichomoa kutoka Lumumba, na ni wao wanaoweza kuitetea(kamati ya maridhiano)

Tulieleza pia kuhusu zawadi na pipi kwawazanzibar. Hilo ndilo limefanyika kwa kuwawekea vyeo vingi katika JMT. Sitta nawenzake hawawelewi kuwa wingi wav yeo ni kwa baadhi ya wznz, wengi huko mitaanibado wana duku duku lao na hivyo suluhu iliyofanywa na tume iliyoandika rasimuya CCM band aid tu.

Hivi sasa lipo vugu vugu la kura ya maonihuko znz, na kwa upande wa Tanganyika mambo mengi yameibuka yasiyo na majibu

Kwa mfano, Watanganyika wanauliza, asilimia21 za ajira zao walizopewa wazanzibar ni utaratibu gani umetumika kufikia nambahiyo?

Wanuliza tena, kwanini znz wapewe 4.5 yapaoto la Tanganyika tukijua hawana mchango wa ina yoyote. Ni utaratibu ganiumetumika kufika hapo

Watanganyika wanauliza, kama ardhiimefanywa kuwa ya muungano, yale mafuta na gesi yanayosemwa yapo znz nayo ni yamuungano? Mafuta yapo katika ardhi ya muungano, iweje yakitoka yawe ya znz pekeyake?

Na ukisoma rasimu ya CCM ya Sitta, Chengena Asha Migiro utaona sehemu kubwa sana ni kuwafariji wznz na kuwaumizaWatanganyika. Hilo tulilisema na limetokea kwa sasa.

Tutaendelea kuwahabarisha mkakatiunaopangwa wa kutumia makongamano, wasomi ili kutoa uhalali wa rasimu ya Chengena Sitta.

Kwasasa hofu kubwa imeiukumba CCM kwanihakuna kinachojadiliwa katika rasimu yao bali uhuni uliotumika kupata 2/3 kamaushahidi tu kuwa utoto na upuuzi wa wazee wetu akina Samwel, Asha na Andreahauna muda utakwama.

Tusemezane

Back
Top Bottom