Duru za siasa: Mtazamo, chaguzi za serikali za mitaa

Duru za siasa: Mtazamo, chaguzi za serikali za mitaa

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
15,773
Reaction score
32,431
DURU: TATHMINI YA CHAGUZI ZA SERIKALI ZA MITAA

Uchaguzi wa serikali za mitaa unaendelea kukiwa na marudio, mikanganyiko na kila aina ya vurugu.
Kuna dalili maandalizi hayakuwa mazuri kwa kiwango chochote kinachofikirika

Matokeo hayawezi kutoa kipimo halisi cha hali ya kisiasa kwa uhalisia wake. Hata hivyo, yanaweza kutoa picha isiyo na rangi kamili ya hali halisi katika muda tulio nao

Matokeo yanaweza kutafsiriwa kwa namna nyingi.
Hivi karibuni kulikuwa na utafiti uliotoa matokeo kuhusu vyama vya kisiasa na wagombe wa Urais kwa mwaka 2015

Lakini pia,kumekuwepo na mambo yaliyoligusa taifa.
Suala la katiba, kashfa za Escrow na uendeshwaji wa bunge na serikali kwa ujumla.

Ni wakati ambapo vyama vya upinzani vimejaribu kuwa karibu kuliko wakati mwingine.
Na ni wakati tunaelekea katika uchaguzi wa mwaka 2015

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, chaguzi za serikali za mitaa zimekuwa na mvuto tofauti na siku za nyuma.

Pengine linachagizwa na ukweli kuwa mitaani/vijijini wapo wapiga kura tofauti na dhana ya wapiga kura wa mjini.

Serikali za mitaa imekuwa ni ngome kubwa kwa CCM kwa kutambua kuwa idadi ya watu wasiokitakia chama hicho ‘mema’ wengi wapo mijini,idadi isiyoweza kuathiri chaguzi kama za wabunge na Marais kwa upande wao

Baada ya kujikita katika udiwani, vyama vya upinzani vimeanza kuweka mizizi huko vijijini na mitaani.

Swali, je kuna matokeo yanayoweza kuakisi jitihada zao wakiwa wameungana?

Uchaguzi wa serikali za mitaa kwa Tanzania bara, hauwezi kutathiminiwa bila kufikiria Zanzibar.

Ukweli ni kuwa chaguzi za mitaa ni hatua ya mwanzo inayosimika mizizi kuelekea chaguzi za taifa.

Matokeo ya chaguzi za mitaa yana athari kwa chaguzi za bunge na Rais, hivyo, kuzitathmini kwa kuangalia upande mmoja kunaweza kutoa picha isiyo sahihi.

Ni kwa mtazamo huo, kumekuwepo na shamra shamra na majonzi kwa kila upande.

Ni mapema mno kutoa tahmini ya jumla kwa kuzingatia mazingira ya chaguzi, utata na wingi au ubora wa ushindi

Duru tutajaribu kuangalia kwa namna tofauti na kutafsiri matokeo kwa kiwango kitakachopatatikana au kuelezwa.

Tutakuwa na mabandiko mfululizo yakiangalia na kutahmini mambo yafuatayo kabla ya kutoa hitimisho linaloweza kueleza maana ya chaguzi hizi.

Tutafanya hivyo kwa kuangalia mambo kadha wa kadha;

1.Hali na mazingira ya chauguzi (Free and fair election)
2.Wingi au upungufu wa ‘’viti’(Quantity)
3.Ubora au udhaifu wa ushindi (Quality)
4.Mgawanyo wa wapiga kura (demographic)
5.Nguvu na udhaifu wa vyama (Weakness and strength)
6.Sababu zilizochangia matokeo (contributing factors)
7.Mwenendo mzima wa hali ya kisiasa(political landscape)
8.Nini kinaweza kutokea katika siku, mwezi au mwaka ujao(future)

Yupo mwanasisasa wa Uingereza aliyewahi kusema,siku moja ni muda mrefu sana katika siasa.
Lolote linaweza kutokea na kubadilisha hali ya kisiasa

Wapo wanajamvi wenzetu waliowahi kutoa kauli zinazojadilika kwa hali ya sasa
Pasco aliwahi kusema CCM imechokwa CDM hawajajipanga Mchambuzi akasema, ‘even magician runs out of trick’ hata wanamazingaombwe huishiwa na mbinu
MwanDiwani kasema upinzani ni vyama vya msimu

Hebu tuangalie kwa upana nini kinapatikana kutokana na chaguzi hizi

Itaendelea sehemu ya I
 
Last edited by a moderator:
1. HALI YA MAZINGIRA YA UCHAGUZI
(FREE AND FAIR)


Hakuna shaka maandalizi yameleta kasoro nyingi.
Si mara ya kwanza kufanya Chaguzi za seriklai za mitaa.

Inashangaza kasoro zisiyohitaji fedha wala elimu zimejitokeza na kuleta vurugu.

Wizara husika haiwezi kukwepa lawama.
Inawezekana kabisa hizi ni mbinu za makusudi ili kutoa matokeo yanayokusudiwa

Sehemu nyingi chaguzi zimeahirishwa hadi wiki ijayo. Sababu ni ukosefu wa vifaA ikiwemo wino

Sababu nyingine ni kujiandikisha mara mbili, kupiga kura kabla ya kutokea kituoni, na kila aina ya uzembe na aibu kwa taifa lenye umri wa nusu karne

Haya ni marudio ya mchezo wa mwaka 1995 uliomwingiza Mkapa madarakani.
Marudio ya uchaguzi yalikatisha watu tamaa na CCM kushinda si kwa kura bali kwa hila.

Kwa hali ilivyo, matokeo yanayoendelea kutangazwa yana athari kubwa sana kwa ari''morali' ya wapiga kura wa maeneo yaliyoahirishwa.

Inaweza kuwa positive au negative kutokana na hali ilivyo.

Waziri mkuu alipotangaza uchaguzi, na serikali kuthibitisha uwepo wake katika tarehe
mahususi,hakukuwa na sababu za kizembe kama kuchelewa vifaa kufika.

Katika kituo kimoja, wapiga kura wamejitokeza saa 1 asubuhi, msimami wa uchaguzi akitokea kazini saa 5 asubuhi akiwa hana wino.

Hili halifanyiki bila sababu, kuna hila zimetendeka ili tu kutoa matokeo yanayotakiwa na wahusika.

Chaguzi hizi zimeonyesha watu kuhamisika kwa kiwango kikubwa.
Hili ni tofauti kidogo na huko nyuma ambapo watu walijiandikisha bila kujitokeza kupiga kura.

Ni aibu kubwa kwamba miaka 50 hatujaweza kujiwekea utaratibu mzuri wa kupata viongozi wetu katika mitaa ambako watu wanaweza kuwa 10 au 100 tu.Hicho ni kiwngo cha mtaa, je kiwango cha taifa kitakuwaje

Ndio maana kuna ulazima wa kuwa na tume huru ya uchaguzi kuelekea 2015
Tume iliyopo sasa si huru ni tawi la serikali na chama tawala.

Majuzi tume imeomba jeshi ili kukamilisha daftari la kura.
Si kazi ya tume kuomba askari, kazi yao kuieleza serikali kuhusu ugumu wa zoezi.

Kwavile tume ya uchaguzi ni mkono wa CCM na serikali yake, tume hiyo bila aibu imetumiwa kutoa ombi la wanajeshi kushiriki kuandikisha daftari la kura

Katika hali hiyo, haiwezekani kukawa na mazingira tenganifu katika uchaguzi wa 2015 ukiwa chini ya tume ya uchaguzi CCM

Hili la serikali za mitaa ni somo zuri kwa uchaguzi ujao. Halikuhitaji kikubwa kama tume lakini linaonekana kushindikana!

Wapinzani na wananchi wakizembea , basi hiki tunachokiona sasa kitakaziwa ili kuleta matokeo husika kuelekea 2015

Kushindwa kusimamia mtaa kuchagua kiongozi ni aibu kwa serikali hii, ni aibu kwa taifa hili.

Vurugu zinazojitokeza hadi mabomu na risasi, ni matokeo ya serikali iliyopo madarakani kushindwa kazi.

Katika nchi za wenzetu, waziri mkuu na mawaziri wake, wangekwenda na maji.
Haiingi akilini eti hakuna wino wa kupiga kura ikiwa ilishatangazwa uchaguzi na kila kitu kipo sawa.

Na bila aibu, waziri husika na viongozi wanadai uchaguzi umeenda vema.

Hivi kweli tunajua maana ya vema. Risasi zinapopigwa, au msimamizi kuchukua kichapo cha wananchi n.k. hilo linaweza kuitwa vema.

Hakuna siri, miaka 50 bado tunahitaji wazungu waje kutusaidia kupanga mitaa yetu.

Uchaguzi wa serikali za mitaa uliandaliwa hovyo, na viongozi hovyo kwa mipango hovyo.

Hakuna hoja ya umasikini, ipo hoja ya umasikini wa viongozi wetu kuweza kufikiri na kutenda. Na huo ndio mwanzo wa umasikini wa Watanzania.

Ni aibu wala haina utetezi, ukiona mtu anasimama na kutetea upuuzi wa chaguzi za mitaa kuvurugwa, mtu huyo si tu kuwa hawezi kuongoza, bali anahitaji matibabu

Inaendelea sehemu ya II (Wingi''Quantity)
 
Sehemu ya II,

WINGI WA VITI (QAUANTITY)
Takiwmu zinazotumia wingi zina utata sana katikatafsiri.Inategemea vigezo vingine ili kukamilisha hoja ya wingi

1. Ushindani wakuanzia mwanzo(from 0) wingi wa viti una umuhimu. Vyama vyote vingejinasibukupata alau kiti kimoja

2. Kwa vile CCM ilikuwa inashikilia viti vingi,tafsiri iliyopo ni moja. Katika viti 100, CCM inapaswa kutetea viti hivyo nawapinzani kunyang'anya.

Inapotokea CCM wakapoteza kiti kimoja tu, ushindi wao ni asilimia 99. Hiyo niya leo si 100 ya jana.
Walioshinda kiti kimoja, wana asilimia 1 ya leo na si 0 ya jana


3. Ushindi wa wingi ni wa eneo gani na mgawanyiko upiwa watu
i)Kwa mfano, CCM ina ngome zake kama Tanga,Morogoro, mikoa ya kusini wasikohitaji kampeni.

Wanaposhinda kwa wingi maeneo hayo, wingi hau eleziubora wa ushindi bali udhaifu wa wapinzani wao. Kwa chama kikongwe kama CCM,kushinda kwa kutumia udhaifu hakuoneyshi nguvu yao halisi

ii)Wingi unatokana na kura zipi. CCM wanategemeakura za vijijini
Wanaposhinda eneo X kwa tofauti ya asilimia 10,wingi umesaidia, lakini je wingi huo una mwelekeo mzuri?

Kwa maneno mengine, kama wagombe wa CCM wameshindakwa tofauti ya asilimia 5, bado wameshinda kwa wingi wa viti, lakini wingi waushindi wa asilimia 25 dhidi ya wapinzani kwa kipindi kilichotanguliaumeathirika.
iii) Kama ilivyosemwa , endapo CCM imepoteza vingikuliko ilivyovitetea au kuvirudisha kutoka upinzanini wameshindwa

Wingi wa viti kwa silimia yoyote si kigezo kizurihasa kwa CCM.
Ikumbukwe wameingia katika ushindani wakiwa na mtaji wa viti.

Siku zijazo kutakuwa na propaganda zinazotumiatakwimu za wingi ili pengine kuwafariji wanachama wa CCM.
Ni vema Zaidi wapinzani na CCM wakaangalia vigezo vingine ili kufanya tathminiya uhakika na wala si suala la asilimia kadhaa bila kuanisha. Kwa upande waupinzani , wingi wa vitialivyoongeza ni zaidi ya namba pia


Itaendelea…..

Tuangalie ubora

 
Sehemu ya III

UBORANA UDHAIFU WA MATOKEO (QUALITY)

Uboraunaozungumziwa ni maeneo ya ushindi na kushindwa. CCM kwa miaka mingi inangome zisizohitaji kampeni. Morogoro ,Tanga, Mtwara, Dar es Slaam, Tabora, Sumbawanga, Pwani, Dodoma, Singida

Wapinzani wametwanyika katika mikoa michache. Mfano,Arusha si yote, huko Monduli na kwingineko ni CCM. Mbeya si yote, wala Mara siyote ukiacha Tarime
Eneowalilokuwa na uhakika ni mkoa wa Kigoma.

Matokeo ya serikali za mitaa yanaonyesha hali kwanjia mbili

CCM: Ubora wao ni kutetea mikoa kama Tanga,Ruvumana Pwani

Udhaifu: CCM imepoteza ngome ya kusini, wapinzaniwameingia mikoa mitiifu ya Morogoro, Dar es Salaam, Shinyanga na Singida.

Na CCM imepoteza sehemu kubwa ya mikoa iliyokuwa naushindani kama Mbeya, Mwanza, Arusha na Mara.

Upinzani: Ubora wao ni kujipenya ngome za CCM. Kule kulikosemekanahakuwezekani kwa mfano wa Morogoro, wameweza kuokoteza.
Kubwa zaidi wameiteka ngome ya kusini na kuiwekaCCM mguu sawa.

Udhaifu: Haieleweki ni vipi wapinzani wanawezakukosa mgombea katika wilaya, tarafa au kata nzima. Kuna tatizo katika kufikiamaeneo hayo

Je ushindi wa wapinzani unatokana na jitihada zaokule walikofika au ni wananchi wamepata mwamko mwingine na kutafuta mbadala?

Ukitaka kuangalia ubora kwa pande zote, tazama mkoawa Shinyanga.
Huu ni mkoa mtiifu sana kwa CCM, hakuna aliyewazakama kungetokea kingine.
Hukowapinzani wamepenya na CCM inapoteza ushawishi.

CCM inapopoteza mkoa wa Shinyanga na Morogoro kwamaana ya kuruhusu mchezo wa upinzani uchezwe kwenye viwanja hivyo,

huku tayari ikiwaimepoteza Lindi na Mtwara, ni jambo linaloshtua na kuonyesha udhaifu

CCM imebaki na mikoa 3' loyal', Tanga, Pwani naRuvuma.
Mkoa wa Pwani, CCM hawapo salama.

Wameshatoa fursa ya upinzani kutoka Morogoro, Dares Salaam na Lindi ni suala la muda tu, Pwani nayo itafuata mkondo.
Ndivyo Shinyanga ilivyopotea kutokana na msukumokutoka Mwanza na Arusha.

Katika sehemu ya II tumeeleza kuhusu wingi(quantity).
Wingi wa viti unapaswa kuangaliwa kwa ubora(quality).

Ukiangalia ubora wa ushindi kwa CCM, ni wazi unatiashaka wingi wa viti watakavyopata.
Kuangalia matokeo kwa asilimia au idadi ya viti nikuumbaza macho. Kuna zaidi ya hapo.

Tuangalie mgawanyikosehemu inayofuata.
 

Sehemu ya IV

MGAWANYO WA WAPIGA KURA

Kuna sababu za kuamini kuwa katika miji na majiji, wapinzani wanaungwa mkono zaidi ya CCM.
Na zipo sababu za kuamini huko vijijini CCM inapoteza ushawishi.



Ushawishi wa CCM kwa makundi yaliyokuwa tiifu umepungua.
Mfano, inapotokea katika jkijiji CCM wanashinda kwa chini ya asilimia 5 ya wapinzani, maana yake ni kuwa kundi tiifu la akina mama limegawanyika.



CCM imepoteza ushawsishi mijini. Hata sehemu walizoshinda, ni dhahiri walikumbana na upinzani mkubwa.
Kigezo kikubwa ni kupoteza ushawishi katika majiji, Mwanza, Arusha, Dar es Salaam.
Pia miji kama Kigoma, Lindi na Mtwara.



CCM inaungwa mkono na kundi la umri uliosogea.
Umri wa kati na vijana wameitosa.
Wale waliopo CCM ni kwa masilahi na si dhamira ya kweli .

Hili linaeleza kupungua kwa kura na namna wapinzani wanavyojipenyeza katika maeneo yao.


Vijana na kundi kubwa la watu wenye elimu ya waledi wa kati na juu, limeshaipa CCM mkono.
Ukitaka kuliona vema, angalia mkoa wa Dar es Slaam.

CCM wameshinda kule kwenye maeneo yao. Eneo la Kigamboni lilikuwa ngome ya CCM. Ujenzi unaoendelea na kuhamia wakazi wa kiwango cha kati, Kigamboni si salama kwa CCM


Kama lipo eneo wapinzani wanaweza kushinda kwa urahisi, Kigamboni ni la kwanza.
Idadi ya wakazi wa asili inapungua, wahamiaji wa kiwango cha kati wanaongezaeka.
Kundi hili lina vijana wenye ugomvi na CCM.



Disadvantage waliyo nayo CCM kuyhusu vijana ni kuwa, kundi hilo lina wasichana pia.

Hivyo uwezekano wa CCM kuongeza kundi la akina mama ambo ni wapiga kura wao wakubwa unapungua kila siku, kwamba hakuna replacement.



Ukiangalia hoja 1 had III , ukachanganya na hii ya IV, tunarudi kule kule kuwa wingi wa viti haujaeleza mafanikio.
Ubora, na mgawanyiko wa wapiga kura ni vitu vya kuangaa kwa ukaribu.

Kama CCM ahijaingiwa na kiwewe basi kuna tatzo wanapoathmini.



Tutazame sababu zilichangia hali inayoonekana

Inaendelea…..


 
Sehemu ya V


SABABU ZILIZOCHANGIA MATOKEO YANAYOONEKANA

Hakuna shaka matokeo yaliyopo yameitia CCM kiwewe.
katibu mwenezi ametoka na kutoa maelezo yanayochanganya ikiwa ni dalili ya kuweweseka

Katibu Nape anasema, katika siasa za vyama vingi lazima kuwepo na kupungua kwa kura.
Well, labda angejiuliza kwanini zisipungue kwa wapinzani zipungue kwa CCM

Pili, anasema waliporuhusu mfumo wa vyama vingi waliliona hilo. Nape amechanganyikiwa kwa kudhani nchi hii ni ya CCM.
Mfumo wa vyama vingi ni haki ya wananchi na wala si suala la CCM kuamua.

Mfumo huo ulirudi wakati Nyerere akiwa hai, hakuweza kuzuia, ni aghalabu kuna mtu anaweza kusema CCM ya sasa iliyowekwa mfukoni na wahalifu inaweza kuzuia.

Na mwisho amepongeza wapinzani kwa sehemu walizoshinda akisema CCM itawasikiliza wananchi.
Amekubali ukweli kuwa wapinzani wameshinda maeneo yanayotia wasi wasi. Hilo lilikuwa ni kukiri.

Kama tulivyosema hapo awali, Nape ametumia takwimu za asilimia 80 kuonyesha ushindi.
Tulisema wapo watakaopotosha kwa kuacha vigezo vingi.

Nape amesimama katika quantity, hakujali kuongelea quality au mgawanyo wa watu na ushindi.
Huu ni uzumbu kuku kwasababu, ni kwa kutumia njia hizo leo wanalinda goli badala ya kushambulia.

CCM inaporudi nyuma kulinda goli badala ya kusahmbulia, ni ajabu viongozi wake wakisema ni ushindi mnono wa asilimia 80

Nape anakumbu kumbu nzuri,akishirikiana na Kinana, wametumia pesa za umma ziara zao mikoani kupitia wakuu wa wilaya.Msaada wao katika kampeni si kutoka katika CCM, bali serikali kwa ujumla.

Pamoja na jitihada hizo, CCM wamepoteza ushawishi maeneo mengi. Kwa umri wa CCM hiyo ni felia wanayotakiwa kuifikiria. Hatutegemei wanaweza kufikiria kwasababu CCM inamilikiwa na wahuni na wahalifu waliochukua chama mateka.

Ndio maana CCM imeshindwa kuchukua hatua na kujikuta katika wakati mgumu kama iliyo nao.
Kuna sababu nyingi zilizochagiza wananchi kukubali mabadiliko hata kama ni kidogo.

1. CCM imepoteza ushawishi kwa wanachama, na chama sasa kipo mikononi mwa wahalifu wenye mabilioni.

2. CCM imeacha misingi yake kama chama cha wakulima na wafanyakazi, sasa ni chama cha wafanya biashara iwe za bidhaa , kisiasa au ulaghai. Hapo ndipo wanachama walipoachwa nje katika kusikilizwa.
a) Wananchi hawakusikilizwa kuhusu tatizo la Mtwara. CCM imelipa gharama kubwa kwa kupoteza mwana mtiifu.

b) Wananchi wana hasira kutokana na mchakato wa katiba
i) Mapendekezo yao kutupwa na genge la wahuni na wahalifu wazoefu kuandika katiba ya mitaani kwa dharau
ii) Uhuni uliofanywa ili kupitisha katiba ya Chenge, ambao hata wanachama wa CCM wamesema wazi haukubaliki.

c)Wizi wa mali na rasilimali za umma
Kashfa za Escrow na kutokuwa na majibu ya viporo yanawatia wananchi hasira.
Pia, wananchi wanakereka wahalifu wanapopewa nafasi ya kupumzika bila hatua za kisheria dhidi ya wahalifu
d) Chama kimekosa uongozi, serikali imekuwa dhaifu na wazee wa chama kutosikilizwa kwasababu uongozi hauna nguvu tena, chama kipo mateka.

Wanaolipa gharama za hayo ni wananchi wa kawaida wasio na hatia wala kunufaika na uhalifu wa aina yoyote unaofanywa ndani ya CCM kwa mgongo wa serikali na kodi zao

e) Serikali kushindwa kufanya kazi. Hili ni kushindwa kwa operesheni kama tokomeza, kusimamia haki za wananchi na mali zao. Bado wanakumbu kumbu ya wezi wa mifugo uwanja wa KIA,serikali inatoa fursa kwa majangili kuendelea na uhalifu.

Huko kwenye madini hali inasikitisha. Wananchi wanabaki na makorongo, thamani zikienda nchi za nje.
Hilo linafanyika kwa ushirikiano wa CCM na wahalifu ima wa ndani au wa nje.

Mambo hayo yanafanyika na wananchi wanayaona. Tatizo la CCM ni kutokubali ukweli kuwa Tanzania ya leo si ya jana.

Wananchi wanakereka lakini hawana njia. Kwa bahati mbaya wananchi wa Tanzania hawakuelewa kuwa wao ndio nchi na ndio wajiri wa hawa viongozi.

Chachu hiyo imeanza kuingia na kinachoendelea ni matokeo ya awali ya wananchi kuamka.

Kuamka kwa wananchi ni pamoja na kubaini mbinu chafu na kuwa tayari kukabiliana na wizi kama wa kura.

Nguvu hiyo imesaidia sana wananchi kutambua kuwa wakiamua wanaweza na wao ndio wenye mpini na si CCM

CCM inaanza kuishiwa na mbinu kama alivyowahi kusema mwanajmvi mwenzetu ''Even magician runs out of trick''

Hoja ya, tuchagueni tuwaletee maendeleo haina mashiko.
Wananchi wanajiuliza kuna tofauti gani kati ya jimbo la Mkinga Muheza na jimbo lingine kule Dodoma au Kigoma?

Pia wanajiuliza je, maendeleo ni haya ya wizi wa mabilioni ya kodi, bill zake akizebeba anayeishi kwa dola 1 kwa siku?
Taratibu wanafunguka akili.

Mbinu za wizi na udanganyifu katika masanduku ya kura nazo zinaonekana kukwama.
Itachukua muda kumaliza tatizo hilo, lakini wananchi wakiamua linaweza kuisha kwa usiku mmoja.

Tumalizie sehemu kwa kusema, matokeo haya yanayoonekana ni ujumbe kwa CCM kuwa wananchi wamechoka kama alivyowahi kusema mwanajmvi Pasco. Kinachoonekana ni kuongezeka kwa chuki kati ya wananchi na CCM.

CCM ina mitihani mikubwa mitatu
1. Kujisafisha, jambo lisilowezekana kwa sasa
2. Kurudisha imani, jambo linalohitaji uthubutu na lenye gharama likifanywa hovyo
3. Kuwasikiliza wananchi, jambo lislokubaliwa na wahuni na wahalifu walioteka chama
4. Kukabiliana na chuki inayojengeka, jambo gumu kutokana na mabadiliko ya kizazi.

Inaendelea....
 
Last edited by a moderator:
Sehemu ya VI

MWENENDO MZIMA WA HALI YA KISIASA

Hali na mwenendo mzima wa kisiasa unaonyesha CCM kupoteza ushawishi wa kisiasa.

CCM inapoteza ushawishi kwa mtazamo wowote,kutoka kwa wasomi, vijana, akina mama na makundi ya jamii

Upinzani una matatizo. Inapotokea hakuna mgombea katika eneo fulani, maana yake ni kuwa eneo halijafikiwa na wapinzani, na kama limefikiwa hakuna nguvu ya ushawishi iliyowavuta wananchi wa eneo husika.

Muungano wa UKAWA, bado umebaki kitaifa. Katika ngazi za chini hainoekani kama kuna kuelewa nini UKAWA wanakusudia.

Kitendo cha kugawana kura katika baadhi ya maeno ni udhaifu mkubwa.Hali hiyo ikiachiwa kuendelea bila viongozi kuchukua hatua za makusudi, uwezekano wa UKAWA kuvurugika utaanzia ngazi za chini.

Pamoja na udhaifu wa UKAWA na upinzani kwa ujumla, wananchi wameona ipo haja ya kufikiria mabadiliko.

Hili ndilo la kuwatia kiwewe CCM. Mambo yanapokwenda bila msukumo mkubwa, yakipata msukumo halisi itakuwa ni ngumu sana.

Jambo moja linalojitokeza ni balance of power katika siku za usoni. Na pengine mabadiliko kabisa.

Mwenendo kama huu ulianza kwa KANU na UNIP na mwisho wa siku zikarudi maktaba.

KANU ya Moi ilitegemea mkono wa chuma. Nayo kama CCM ilitumia maguvu kukabiliana na wapenda mabadiliko ndani ya chama.

Mkono wa Polisi na vyombo vya usalama vilitumika.Tume ya uchaguzi ilihakikisha KANU inatawala.

Wananchi walipoamua kwa dhati yao, KANU imetoweka. Hakuna tofauti na hali tunayoiona nchini.

Tena mazingira yanashabihiana hasa suala la katiba. KANU ilifanya ukaidi wa kutosikiliza wananchi.

Wapinzani wakatumia karata hiyo na umoja wao wa Rainbow kuzungumzia agenda ya katiba iliyowagusa wananchi.
KANU iliondoka madarakani bila kupenda wala kutarajia.

Hata kama CCM itabaki madarakani kwa halali au kwa hila, nguvu ya utawala itapungua sana.

Wabunge wengi wa CCM watapoteza majimbo yao.Bunge linaweza kuwa mikononi mwa chama cha upinzani.

Na kama haitatokea basi ule ubwete wa wingi wa CCM *(2/3) itakuwa umekwisha. JK hana cha kupoteza kama alivyokuwa Rais Moi.

Kama wapo wabunge wa CCM wanaolala usingizi kwa hali ilivyo, basi huyo ajiandae kwa kipindi kigumu sana mbeleni.

Muda wa kurekebisha makosa umepita. Mfano, wabunge wa CCM watarudi vipi kwa wananchi kuwaeleza kuhusu katiba?

Kibaya au kizuri zaidi ni pale CCM watakapolazimisha kura ya maoni ya katiba yao.

Kura hiyo ndio itajenga mazingira tengefu kwa CCM kuondoka madarakani.

Inaweza kuwa kura ya chuki ya kukataa katiba. Hilo litatoa nguvu kwa wananchi kwamba wanaweza.

Inaweza kuwa ushindi wa CCM wa wizi, huo nao utakabiliana na upinzani OcTober wakati wa uchaguzi.

Kama lipo jambo CCM wanapaswa kuliepuka, ni kuingia katika mzozo na wananchi kwa kutumia nguvu au wingi wao.

Uchaguzi wa serikali za mitaa umewajenga wananchi kuchukua mamlaka, umejenga ari kwa wapinzani na umekidhoofisha CCM kwa kigezo chochote.

Itaendelea…..
 
HALI YA SIKU ZA USONI

Upinzani ulipoanza sehemu za manzese zilitoa diwani. Kilichofuata ni majimbo kama Tarime na Karatu kutoa wabunge.

Mwendo huo umeendelea na chaguzi zilizofuata wabunge wametoka baadhi ya maeneo yasiyotarajiwa.
CCM ielewe kuwa ile ngome yao ya vijijini sasa inabomoka.
Mikoa salama imepungua. Kwa mfano, CCM ni salama Dodoma, Ruvuma, Tabora,Tanga na Pwani.

Ngome za CCM zilizoanguka ni Morogoro, Shinyanga, Mtwara na Lindi.
Mikoa isiayo salama kwa CCM ni pamoja na Iringa, Dar, Bukoba, Arusha, Mwanza, Kigoma.
uwezekano kwa wapinzani wa kutoa wabunge sawa au zaidi ya CCM ni mkubwa

Mikoa iliyobaki ni ‘toss up' kwamba lolote linawezekana.
Kwa hali hiyo CCM ijiandae kisaikolojia hasa wabunge wake

UPINZANI
Ushindi walioupata katika baadhi ya maeneo hauelezi kwa uhalisia nguvu ya UKAWA au hoja wanazojenga.
Pengine ni kutokana na hoja zinazojitokeza bungeni zinazowaamsha wananchi bila nguvu ya upinzani.

Kukosekana kwa wagombe kwa baadhi ya maeneo hakutoi nafasi kwa wapinzani kushinda uchaguzi.
Ni lazima wahakikishe kila eneo, mtaa na kijiji wana uwakilishi.

Upinzani hauwezi kuchukua dola ikiwa baadhi ya maeneo hakuna upinzani. Itawezekana vipi kugawana kura mahali wasipokuwa na mgombea?

Hili la kupita bila kupingwa lazima liangaliwe. Kuna suala la pingamizi, hilo ni tofauti na kushinda bila mpinzani.

Ingawa inaonekana upinzani kukua kwa kasi, katika miaka zaidi ya 20 bado wanahitaji kukimbia na si kutembea kwa kasi

Wapinzani wajiulize, kipi kimeweza kuwaamsha watu wa Kigoma na Singida ambacho hakiwezekani Tanga na Pwani?

WABUNGE
Kwa upande wa CCM, uhalifu, kashfa na ufujaji unahusishwa moja kwa moja na CCM.
Hata kama wanaofanya ni wachache, wananchi wameshatoa ujumbe kuwa hali inakoelekea itawaelemea.
Leo mbunge wa CCM ataeleza nini aeleweke?

Kiburi cha kutowasikiliza wananchi katika mambo muhimu kama katiba kwa mgongo wa chama, ni mzigo mzito kwa wabunge wa CCM.

Hivi wanaendaje kunadi rasimu ya Chenge katika mazingira yaliyojitokeza sasa hivi?
Wabunge watakaolipa gharama za uhuni wa kundi la wana CCM ni wa CCM, ni suala la muda. Muda wa kurekebisha makosa haupo,ukimya au undumila kuwili au upiga debe itakuwa ni chachu ya hasira za wananchi dhidi yao.

Wabunge watasimama na CCM na kundi lao ili wateuliwa. Nguvu iliyokuwepo ya kuwaweka madarakani sasa haipo, nguvu iliyopo ni ya wananchi. Mbunge makini wa CCM afikirie hilo kwa makini.

Inaendelea......
 
Sehemu ya mwisho

NINI KINATOKEA


Asilimia yoyote ya viti kwa CCM inaeleza kupungua kwa ushawishi wa kisiasa. Ongezeko lolote la viti linaonyesha kumarika kwa upinzani.
Kwa matokeo yaliyopo katika vurugu na hujuma, wapinzani wanaonekana kuungwa mkono na jamii

Mwamko wa kujiandikisha na kupiga kura unatueleza jambo moja. Wananchi huhamasika lakini ipo njia inayotumika ya kuwazuia kupiga kura. Haiwezekani katika chaguzi hasa ndogo, wananchi wajiandikishe asilimia 80, wapige kura asilimia 30. Mbona hayakutokea kipindi hiki?


Je, ni mwamko wa wananchi? Ni kujulikana kwa mbinu za kihalifu? Ni kuchokwa kwa CCM? Ni kukubalika kwa hoja za wapinzani?
Je, ni kutokana na ongezeko la kashfa na utendaji mbovu wa serikali ya CCM? Je, ni hasira za wananchi kutosikilizwa na kudharauliw

Changamoto kwa wapinzani ni kuhakikisha mwendo ulioonekana unaendelea. Wanatakiwa watoe matokeo chanya ili kuzidi kujenga Imani.
Matokeo hasi yatawaathiri nap engine kuondoa tumaini waanaloonyesha wananchi

Ni kutokana na mabadiliko yanayojitokeza, ubabe wa aina yoyote wa CCM ni kuendelea kujichimbia kaburi. Zama za kutawala na si kuongoza zinafikia ukingoni. KANU na UNIP walipitia CCM ilipo sasa hivi.

Kiwewe cha chaguzi za serikali za mitaa kinatoa mwelekeo mpya katika duru za siasa nchini. Ujumbe wa wananchi kwa serikali ya CCM ni clear.
Ima CCM iwasikilize au iendelee na ubabe ikielekea kule ilipo KANU.

Kiwewe kinamlazimisha mwenyekiti wa CCM aliye Rais kuja na mikakati mingine. Ijumaa Rais atahutubia taifa.

Wengi wanataraji Rais kuongelea kashfa za Escrow. Ukweli ni kuwa, Rais anataka kutumia jukwaa la kisiasa kuongea na wananchi kwasababu kadhaa

  1. Kutafuta kuungwa mkono baada ya serikali kupoteza ushawishi
  2. Kusahaulisha wananchi kilichotokea ili kupunguza msisimko walio nao wananchi kuelekea kuiondoa ccm
  3. Kutumia jukwaa hilo kusukuma agenda zinazoonekana kukwama.

    Kesho asubuhi kabla ya hotuba ya Rais, tutajadili mwelekeo wa hotuba yake, nini kinatarajiwa kusemwa na kwasababu gani.

    Kwa haraka tunaweza kusema, hotuba yake ni matokeo ya kiwewe cha chaguzi za serikali za mitaa na itajikita huko kwa njia ya kujificha.

    Tusemezane
 
HOTUBA YA JK
Intarajiwa Rais ataongea nawazee wa Dar es Salaam na taifa kwa ujumla.
Utaratibu wa Rais umekuwakuongea na taifa siku za mwisho wa mwezi.

Na mwezi ukiwa wa mwisho kwamwaka, pengine alikuwa na mengi ya kuzungumza
Katika haliya kushtua, Raisataongea na wazee.
Utamaduni uliopo ni kuwatumia wazee kupata huruma ya jamboFulani.
Suala la wazee limepoteza maana.


Wananchi wamebaini wazee wengini waganga njaa na weledi wao ni hafifu.
Ni watu wanaoweza kupigwa hadithi za Abnuwasi wakaamini ilikuwa kweli.


Wananchi wanataraji kusikia Rais akiongelea suala la Escrow na pengine na majibu yawiki mbilizilizo msubiri

Mtazamo wetukuhusu hotuba yaJK ni kama ifuatavyo

1. AtawashukuruWatanzania kwa salam wakati akiwakatika matubabu.
Atatumia nafasi hiyo kusisitiza kmapeni aliyoanzisha ya tezidume.
Rais atahimiza kucheki afya,hatazungumzia kwanini nchi haina dawa na hasa hospitali kubwa


2. Rais ataongelea suala la Escrow. jJK Ataonyesha hasira wakati huo huo akitumia fursa hiyo kuhakikishawatuhumiwa ''wanatendewa haki'

Kitendo cha mwanasheria mkuu kujiuzulu kimelenga kusema ‘tunafanyia kazi na uchunguzi wa kinaunaendelea, hatua zimeanza kuchukuliwa''
Rais antarajiwa kulirudisha suala hilo serikalini na kufunga mjadala


Kwa namna fulani ataeleza kuhusu mgangono wamihimili uliojitokeza, na kutumia nafasi kuonyesha upo umuhimu wa kupitisha katiba ya Chenge. JK atawatuhumu PAC kwa njia yasiri ili kumlinda PM wake na mawaziri.

3. JK ataongeleauchaguzi wa serikali za mitaa,akionyesha kukerwa na yaliyotokea.
Atatumianafasi hiyo kuonyesha serikali imeanza kuchukua hatua dhidi ya wahusika(wakurugenzi)


4. Kura ya Maoni.Hili hasa ndilo ataliongea kwa undani. Sababu za kufanya hivyo ni nyingi.
Kwanza, kura ya maoni ya katiba yaChenge imesusiwa na wananchi na kukosamsisimko.

Pili, matokeo ya uchaguzi waseri kali za mitaa unaonyesha hasira za wananchi dhidi ya serikali ya Kikwete.
It is unlikely hiyo katiba yaoya mafichoni inaweza hata kukubaliwa kwa kuangalia mwamko wa wananchi.


-JK atatumia nafasi kuhimiza na kuamsha mjadala wa kura ya maoni uliokufa kabla ya kuanza.
Tunakumbuka ofisi ya Rais ilivyohusika na kuhonga waandishi na wasomi na badokatiba imesusiwa.


JK anatarajiwa kutangaza uzinduzi wa kampeni za kura ya maoni ya katiba ya CCM na Chenge ili kuwasahaulisha wananchi machungu yaEscrow, kukosekana dawa hospitali, chaguzimbovu za serikali za mitaa na matokeo mabovu

Pia, anatarajiwa kutangaza jeshi kuanza kuandikisha daftari la wapiga kura.
Hoja hiyo ilitolewa na tume ya uchaguzi ambayo hufanyakazi kwa maagizo kutoka kwa mwenyekiti wa CCM na Rais.


Hotuba ya JK itakuwa yakisiasa ya kampeni za mambo yasiyo na tija na taifa.
JK hatatoa solution ya suala lolote, atakacho kifanyani ku balance kila issue ili aonekane mwema kwakila upande.


Tusemezane








 
Nguruvi umemaliza, sioni jipya atakalokuja nalo jk hasa ukizingatia naye ni miongoni mwa wanakundi waliohusika moja kwa moja kulifikisha taifa hapa lilipo.
 
Nguruvi umemaliza, sioni jipya atakalokuja nalo jk hasa ukizingatia naye ni miongoni mwa wanakundi waliohusika moja kwa moja kulifikisha taifa hapa lilipo.
Update
Mkutanoaliokuwa ameandaa kama ilivyosema mawasiliano Ikuku na ilivyonukuliwa na gazetila Habari leo siku tatu zilizopita umeahirishwa !!


Badala yakemkutano utafanyika tarehe 3 January 2015
http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/33411-mzozo-escrow-kumalizwa-j3

Kinachoendeleani kuchukua muda wa kutahmini matokeo ya serikali za mitaa, namna ya kuwapanafasi watuhumiwa wa escrow wajiuzulu na kuingiza suala la kura za maoni zakatiba ya Chenge.

Tunakumbuka jinsi JK alivyovunja tume ya Warioba siku ilipotimia na kwanyang'anya ofisi,kufunga website n.k.
Swali linakuja, huku kusita sita katika mambo mengine yakitaifa kunatokana na nini.



Kama utasomagazeti la Habari leo, ni wazi jitihada za kumlinda Mhongo zinaendelea kwakutumia vyombo vya habari. Hili ni kutengeneza mazingira mazuri yatakayompanafasi Rais kuwaacha baadhi ya watuhumiwa.
 
Nguruvi3,

Hakika unajitahidi sana kuchambua mambo hususan haya ya siasa za Tgk.

Tatizo lako kubwa katika uchambuzi wako ni USHABIKI. umejikita katika ushabiki wa kisiasa na chuki binafsi na hizo zoote kufanya uchambuzi wako kupoteza haiba kwa wasomaji.

Kumbuka kuwa mchambuzi yoyote siku zote anatakiwa kuifafanulia na kuiilimisha jamii bila kuegemea upande wowote wa shilingi NA HIVYO kutoa nafasi kwa wasomaji wa uchambuzi huo kufanya maamuzi yao kwa mujibu wa maono na uelewa wao.

Ushauri wangu punguza ushabiki na tuliza akili na soma matukio kwa kina na mapana yake ndio uielezee jamii. Kumbuka kuna wengi wanakusoma.

Ahsantum
 
Nguruvi3,

Hakika unajitahidi sana kuchambua mambo hususan haya ya siasa za Tgk.

Tatizo lako kubwa katika uchambuzi wako ni USHABIKI. umejikita katika ushabiki wa kisiasa na chuki binafsi na hizo zoote kufanya uchambuzi wako kupoteza haiba kwa wasomaji.

Kumbuka kuwa mchambuzi yoyote siku zote anatakiwa kuifafanulia na kuiilimisha jamii bila kuegemea upande wowote wa shilingi NA HIVYO kutoa nafasi kwa wasomaji wa uchambuzi huo kufanya maamuzi yao kwa mujibu wa maono na uelewa wao.

Ushauri wangu punguza ushabiki na tuliza akili na soma matukio kwa kina na mapana yake ndio uielezee jamii. Kumbuka kuna wengi wanakusoma.

Ahsantum

Mkuu Barubaru huo ni mtazamo wako, binafsi namuona huyu Bwana Nguruvi kwa picha tofauti na yako,mnamuona kama mchambuzi huru na anaetoa analysis based on facts na avilable data ( both qualitative and quantitative), kwa sisi tusio na vyama na tusioshabikia siasa za majitakaa tubamuona kama jamaa yuko sawa ukiacha makosa madogo ya kibinadamu ambayo hata kwa maprofessor wa Havard au Cambridge utayakuta.

Otherwise uwe una chuki nae just kwasababu haendi na muono wako, bt hiyo ni kazi ya analyst sio kila jambo atakupendeza kunawakati atakuchoma misumari, so usimkatishe tamaa wala kumdhihaki mtie moyo aongeze juhudi maana anasaidia wengi.

Mkuu Nguruvi3, binafsi nimekua nikikusoma sana kwa muda mrefu kabla hata sijaanza kuchangia jukwaa hili la GT, nakutia moyo endelea na uchambuzi wako makini, unatusaidia wengi na kwa taarifa tu wengi tunakufuatilia hata kama hatuchangii, usikatishwe tamaa hata tone. Ni yangu haya machache
 
CHAGUZI ZA SERIKALI ZA MITAA NA FUKUTO NDANI YA CCM

WAPINZANI WAKISIMAMA KIDETE, CCM MAJI YA SHINGO

Juzi wakati wa kumkaribisha Rais/Mwenyekiti wa CCM mkuu wa mkoa wa Dar es salaam alitoa takwimu za ushindi wa asilimia 75 kwa mkoa wa Dar es Salaam

Tulieleza jinsi takwimu zinavyotumika vibaya wala si kuzitathminiMkuu wa mkoa hakueleza ubora wa ushindi, hakueleza kwanini kumekuwa na upungufu ,kuyumba kwa ngome za CCM kama ilivyotokea Kigamboni,bali namba kubwa tu

Ikizingatiwa majimbo mawili si ya CCM,asilimia 75 inaeleza lolote?

Rais kawapongeza walioshinda kinyume na tambo za ushindi wa kishindo. Hali hiyo inaeleza utata unaoikumba CCM

Kwanza, kuna hofu miongoni mwa wabunge ya kuwa ‘mbinu za ushindi'' zinadhibitiwa.
Kuna mwamako wa wananchi kutambua umuhimu wa kupiga kura kinyume na ilivyokuwa

Pili, matokeo hayaelezeki kwa uyakinifu kama ni zao la kashfa zinzaozikumba serikali hii

Tatu, matokeo yanaonyesha chuki kutokana na maamuzi ya CCM.
a)Chuki kuhusu masuala ya mikoa ya kusini ambako CCM imetumia maguvu na si busara wala weledi
b)Chuki dhidi ya kudhalilishwa wananchi kwa maoni yao ya katiba
c)Kutumia wingi katika kupitisha mawazo ya CCM kama ilivyo katika katiba

Nne, kuna chuki zilizokuwepo sasa zitaibuka rasmi
a)Ziara za Kinana na Nape hzionekani kuzaa matunda.
Hili litaamsha hoja ya mawaziri mizigo na mafisadi waliopewa muda

Makundi hayo yatatumia matokeo kama fimbo ya kujibu mapigo ya lawama za Nape na Kinana

b) Kuna kundi la CCM wanoona wanaonewa. Hili ni kama la Kagasheki,Tibaijuka na Lowassa.
Kwamba, katika kuwajibishwa wapo mbuzi wa kafara na wanaokingiwa kifua

c) Kuna kundi linalotaka wenzao wawajibishwe ili lipate nguvu za kisiasa kuelekea 2015.
Kwamba hakuna hatua zilizochukuliwa hadi sasa inatia hasira kundi hili.

d) Wapo CCM wanaoona ni waathirika wa uzembe unaoleta tabu. Kundi hili halinufaiki kwa namna yoyote, si kifisadi au madaraka, lakini lipo katika wakati mgumu kutokana hali tete iliyopo

Mwisho wa mwezi, Rais atatoa hotuba ya mwezi.
Rais amelikwepa kama tulivyoeleza kutoshadidia hasira za escrow.
Rais atapigia chapuo katiba ya CCM na Chenge

Katika mtafaruku unaofukuta CCM, kura ya maoni inaweza kufia mikononi mwa Kikwete kutokana na chuki za wananchi

Chuki zizlizopata nguvu kwa kuelewa inawezekana wananchi wakiamua

Kikwete hataungwa mkono kutokana na sababu zilizotajwa hapo juu.

Wabunge wa CCM wana wakati mgumu kuamua

  1. Kusimama na JK asiyepoteza lolote ili wateuliwe kugombea tena
  2. Kususia kura ya maoni ya Chenge ili waungwe mkono na wananchi
  3. Kusimama katika ukweli, lolote na liwe

Kama lipo jambo JK anapaswa kuliepuka ni kura ya maoni. Hii inaweza kulazmishwa kwa kutumia tume ya uchaguzi.
Hata hivyo itakuwa kichochoe kizuri cha kuonyesha hasira za wananchi 2015.

Wananchi na wapinzani, hawatakiwi kujadili suala la kura ya maoni.
Kufanya hivyo ni kuipa uhalali na kupunguza shinikizo kwa wana CCM waliopo njia panda.

Hoja ya wapinzani iwe kuzungumzia mchakato ulivyovurugwa na kwamba wakipewa uwezo wa bunge au serikali, katiba ya Chenge itafutwa

Waunganishe jinsi katiba iliyoandikwa na mafisadi inavyowalinda kama ilivyo kwa escrow na kashfa nyingine.

Wawaulize wananchi, wapi na lini wameshirikishwa kuandika katiba ya mafisadi?
Na kama hukuna, wanapiga kura ya maoni kitu gani wasichokijua?

Huo ndio ujumbe wanaotakiwa wautoe na si kujadili uhalali wa haramu
Haramu ni haramu hakuna afadhali ya kujadili kama haramu ikubaliwe au ikatiliwe

Tusemezane
 
Mkuu Barubaru huo ni mtazamo wako, binafsi namuona huyu Bwana Nguruvi kwa picha tofauti na yako,mnamuona kama mchambuzi huru na anaetoa analysis based on facts na avilable data ( both qualitative and quantitative), kwa sisi tusio na vyama na tusioshabikia siasa za majitakaa tubamuona kama jamaa yuko sawa ukiacha makosa madogo ya kibinadamu ambayo hata kwa maprofessor wa Havard au Cambridge utayakuta.

Otherwise uwe una chuki nae just kwasababu haendi na muono wako, bt hiyo ni kazi ya analyst sio kila jambo atakupendeza kunawakati atakuchoma misumari, so usimkatishe tamaa wala kumdhihaki mtie moyo aongeze juhudi maana anasaidia wengi.

Mkuu Nguruvi3, binafsi nimekua nikikusoma sana kwa muda mrefu kabla hata sijaanza kuchangia jukwaa hili la GT, nakutia moyo endelea na uchambuzi wako makini, unatusaidia wengi na kwa taarifa tu wengi tunakufuatilia hata kama hatuchangii, usikatishwe tamaa hata tone. Ni yangu haya machache

Kama nilivyobainisha kuwa mchambuzi au uchambuzi wowote unakuwa na sehemu mbili yaani kuukubali ima kuupinga na hizo zote zinaongozwa na facts. na huo ndio unaitwa mjadala au demokrasi.

Siwezi kupingana na maono yako lakin kwa maono yangu naona fika amejikita katika ushabiki hususan wa kiasiasa na sehemu nyingine chuki za namna moja au nyingine na hilo lipo wazi labda uwe na makengeza au uvae miwani ya mbao ndio usilione. Lakin kama unamsoma KWA NIA YA KUMUELEWA unaweza kugundua mengi.

Nahishimu sana maono yako lakin nasimamia maono yangu na kusimamia ushauri wangu kwake.kuwa mchambuzi yoyote siku zote anatakiwa kuifafanulia na kuiilimisha jamii bila kuegemea upande wowote wa shilingi NA HIVYO kutoa nafasi kwa wasomaji wa uchambuzi huo kufanya maamuzi yao kwa mujibu wa maono na uelewa wao.





 
King Suleiman nashukuru kwa maoni yako na jinsi unavyotutia moyo.
Kama yapo mapungufukama ulivyosema, hayo ni ya kibinadamu. Hakuna miongoni mwetu aliye mtimilifu.
Ushauri wako nauchukua kwa dhati kabisa, hakika umenitia nguvu


Baru baru ,nawe pia nikushukuru kwa maoni yako.
Hata kama tunatofautiana namna yakufikisha ujumbe bado naamini kuna njia nyingi za mawasiliano

Kuhusu ushabiki,hayo ni maoni yako. Nitakuwa nimekosea nikisema ni sahihi au la.

Jambo lililonisikitisha ni kauli yako ya kueleza jinsi nilivyo na chuki tena ukisema kama watu watasoma kwa kunielewa. Hukuweka facts za ku back up madai yako.
Hayo ni maoni yako.
Si vema maoni yako yasiyo na facts na ambayo ni hisia ukayafanya ni ukweli.


Nikikusoma vema si mara moja au mbili, umetoa madai hayo bila kuonyesha wapi unadhani kunachuki na facts za ku back up. Ni hatari unapofanya hisia zako kuwa ni ukweli.Ni jambo baya unapotia hisia zako ili zitie hisia wengine.

Kwa lugha nyingine unachokifanya, kwavile hakina ukweli kwa kukosa kithibitisho, hiyo ni fitna.
Itabaki kuwa fitna unless uje na kueleza wapi chuki zilipo kwa nani,kundi gani n.k. ili watu waone.
Umesema zipo wazi, kwa wengine wasioona unawajibu wa kuwaelesha ni wapi chuki zilipo.

Lakini pianakuomba utembelee nyuzi zote za duru kuanzia 2010.
Hapo unaweza kusema ninachuki na dunia.
Nimejadili sana yanayotokea duniani, sasa chuki na dunia ninawezaje kuifanya nikiwa mwanadamu?

Siku zote kauli yangu mbiu ni hii ‘Nitasema ninachotaka kueleza na si kile mtu anachotaka kusikia''
 
King Suleiman nashukuru kwa maoni yako na jinsi unavyotutia moyo.
Kama yapo mapungufukama ulivyosema, hayo ni ya kibinadamu. Hakuna miongoni mwetu aliye mtimilifu.
Ushauri wako nauchukua kwa dhati kabisa, hakika umenitia nguvu


Baru baru ,nawe pia nikushukuru kwa maoni yako.
Hata kama tunatofautiana namna yakufikisha ujumbe bado naamini kuna njia nyingi za mawasiliano

Kuhusu ushabiki,hayo ni maoni yako. Nitakuwa nimekosea nikisema ni sahihi au la.

Jambo lililonisikitisha ni kauli yako ya kueleza jinsi nilivyo na chuki tena ukisema kama watu watasoma kwa kunielewa. Hukuweka facts za ku back up madai yako.
Hayo ni maoni yako.
Si vema maoni yako yasiyo na facts na ambayo ni hisia ukayafanya ni ukweli.


Nikikusoma vema si mara moja au mbili, umetoa madai hayo bila kuonyesha wapi unadhani kunachuki na facts za ku back up. Ni hatari unapofanya hisia zako kuwa ni ukweli.Ni jambo baya unapotia hisia zako ili zitie hisia wengine.

Kwa lugha nyingine unachokifanya, kwavile hakina ukweli kwa kukosa kithibitisho, hiyo ni fitna.
Itabaki kuwa fitna unless uje na kueleza wapi chuki zilipo kwa nani,kundi gani n.k. ili watu waone.
Umesema zipo wazi, kwa wengine wasioona unawajibu wa kuwaelesha ni wapi chuki zilipo.

Lakini pianakuomba utembelee nyuzi zote za duru kuanzia 2010.
Hapo unaweza kusema ninachuki na dunia.
Nimejadili sana yanayotokea duniani, sasa chuki na dunia ninawezaje kuifanya nikiwa mwanadamu?

Siku zote kauli yangu mbiu ni hii ‘Nitasema ninachotaka kueleza na si kile mtu anachotaka kusikia''

Nguruvi3.

Nashukuru kwa comment zako.

Mimi naona sio busara nikaweka facts zangu kubainisha USHABIKI NA CHUKI ZAKO katika uzi huu lakin kama kwani naona zitapoteza maudhui ya uzi husika lakin kama utaruhusu nawza poteza muda kupitia post zako na kukuwekea hapa. naomba ruhsa yako kwalo.

Lakin in general katika maandiko yako umejikita katika ushabiki wa kisiasa na chuki kwa Znz na waZnz. hilo lipo wazi. na kama mtu akikusoma kiundani umejidhwihirisha umeshabikia upinzani huko Tanzania na kama utakufuatilia na kukupembua kwa kina atagundua umejikipenda chama kimoja cha upinzani na kuviponda vingine.

Hili la Ushabiki na chuki dhidi ya Znz, hili sifikiri kama utataka ushahihidi zaidi kwani kila unapojaribu kupotosha mambo ya Znz iwe ndani ya znz au katika muungano iwe kiuchumi au kijamii mara zote nakuwa makini kukuweka sawa japo unakuwa unachukia lakin najitahidi.

Kumbuka kuwa mimi ni msomaji mzuri wa JF na napitia karibu topic nyingi sana na post nyingi tu na kuna baadhwi nachangia. Hivyo ukiona na comment kitu jua nimeona kuna upungufu kwani palipo timia natoa hongera tu na kupita.

Kumbuka sumu kubwa ya uchambuzi ni USHABIKI na CHUKI nalo nakuhasa liangalie katika maandiko yako.

Ahsantum

 
Barubaru,ninashangaa unaposema kuingiza hoja zako kutavuruga uzi.
Mbona tayariumeshavuruga?

Hata sionihoja zako zenye tuhuma zinaingiaje katika uzi huu wa serikali za mitaa.

Ningekushauriutoe ushahidi katika uzi unaowezakuanzisha.
Ni haki yakondani ya jamvi isyohitaji ruhusa ya mtu

Ima hili lahisia zako, tuwaachie wasomaji waamue kwa mitazamo yao na si kwa ushawishiunaoufanya

Mwisho,narudia tena kuwa jambo unalohisi ni haki yako
Kama umeshadraw conclusion, ubaki nayo kama haki yako.
Unapoipenyezakwa hila, ni fitna.

''Nitasemaninachokusidia kueleza si kile mtu anachotarajia kusikia''

Kwa wasomajinawaomba radhi kwa kutoka nje ya mada.

 
Back
Top Bottom