Sera/Ilani inaweza kuwa mawasiliano, na katika hilo mkazo unaweza kuwekwa katika eneo fulani kama ujenzi wa barabara au reli.
Kama ulivyosema, huwezi kuwa na ilani/sera zinazozungumzia barabara, reli, boti nameli kwa wakati mmoja.
Lazima kuwe na kipaumbele ambacho ni sera/ilani. Kipaumbele hicho kijibu hali ya wakati na matarajio ya siku za mbeleni
Kwa mfano,ukisema reli katika std, hapa ielezwe, reli hiyo imelenga nini kwanini na kwa matokeo gani.
Kuiongelea reli tu bila kueleza hayo, ni sawa na kuongelea majukumu na wajibu wa serikali wa kila siku kama sera/ilani, Kosa!
Sasa ndugu Nguruvi3 naona unaingilia mtiririko wa mawazo yangu in advance, na sidhani kama nina electrons kichwani zinazotuma mawazo yangu kwenye cyberspace!
Jioni hiii nilidhamiria kuja na kuongelea suala la Barabara kama sera, lakini si shida nitaendelea na kulipambanua na kuonyesha mafupi ya kuonyeshwa wajibu kuwa Sera au ishara ya ushindi kuleta maendeleo.
Hakuna sera ya barabara, madaraja au reli. Sera inayoweza kuelezeka ni ya miundombinu na mawasiliano.
Ujenzi wa barabara ni sehemu ya uimarishaji wa miundo mbinu, ni sehemu ya bajeti ya serikali katika kuboresha miundombinu.
Lakini si kweli na si ustaarabu kulaghai Taifa kusema mafanikio ya Serikali ni kujenga barabara au kudai ni Serikali ya Chama fulani au Chama fulani ndio imeleta barabara. Huko ni kuwadharau wananchi na kuwatusi na si sera hata kidogo.
Wananchi wametoa zabuni ya kutaka mtu atakayefanya kazi kwa niaba yao kutekeleza matakwa yao, zabuni hii hupitisha kwa mfumo wa uchaguzi mkuu na kura.
Matakwa ya wananchi ni mengi : shughuli za maendeleo na uzalishaji, huduma za jamii (afya, elimu, maji, ajira), kusimamia na kukusanya mapato, kulinda Taifa na kusimamia haki na sheria, na la mwisho ni kuthamini utu na dhamana ya Uzabuni kupitia Katiba na mgawanyo wa kikazi wa Serikali.
Kutokana na matakwa au mahitaji haya, ambayo yanaweza kushabihiana na vision, Vyama vya siasa hupaswa kuunda sera na ilani ili kuweza kufanya kazi kutokana na uzabuni walioshinda.
Sasa wananchi wanataka miundombinu iliyo imara ambayo itaruhusu wao, bidhaa na mazao kuweza kupita kutoka kona moja hadi nyingine.
Sera ya miundo mbinu ingekuwa ni kuangalia ni jinsi gani nchi inaweza kufikika kwa ufanisi kila kona ili kusambaza maendeleo, kupeleka huduma na kuruhusu movement ya watu na bidhaa.
Tulipopata uhuru, tulirithi miundo mbinu iliyojengwa na wakoloni. TUkaendeleza kwa kadiri ya mahitaji yalivyoongezeka na hata kuambatana na kukua kwa idadi ya watu.
Lakini kama tutajisifu leo kwa kujenga barabara (ukweli tumepanua tuu barabara na kuweka lami) lakini hatuoanishi na mahitaji wala kuonyesha ni vipi usimamizi wake haukuwa wa makini.
Mfano, jiji la Dar na njia zinazoingia Dar ni zile zile tangu ukoloni. Magufuli katika hotuba yake moja Bungeni aliongelea vipimo vya upana wa barabara uliofanya na Wakoloni miaka ya 1940s.
Lakini, kushindikana kwa Dar kuwa na mfumo bora wa barabara kwa zaidi ya miaka 30 pamoja na mfumuko wa idadi ya watu kuongezeka, kuongezeka kwa magari na msongamano ambao sasa umeishia kufanya watu watumie takriban masaa 3-5 kutoka nyumbani kwenda kazini na kurudi, haiwezekani tukasifia ma-flyover, DART au lami mpya na kusema tumeleta maendeleo. Tulichofanya ni kuweka viraka katika mfumo ule ule uliozeeka na ni dhahiri ni ukosefu wa Sera.
Nikiendelea tena kuiangalia barabara ya MOrogoro, inashangaza kuwa mpaka leo hii, njia kuu ya kuingia Dar inategemea Daraja la Ruvu, siku daraja likianguka kwa uzee au kusombwa maji ya mafuriko, Dari haitawezekana kuingilika au kutoka, huduma zitasimama na kero zitakuwa nyingi.
Reli, bandari, usafiri wa ndege na maji, mifereji, madaraja nayo inafanywa kama ni sera, lakini ni wajibu wa Serikali kuhakikisha miundo mbinu inafanya kazi na kama ni sera, ni heri Sera ya miundo mbinu ingelenga hatua za kuhakikisha huduma za usafirishaji na uchukuzi zinafanyika kwa ufanisi mkubwa, kubunguza misongamano na ucheleweshaji wa usafirishaji, kutumia mbinu bora na zenye gharama bora na nafuu kusafirisha mizigo (reli ya kati, Tanga na Tazara zimeachwa zioze na tunakimbilia malori kwa kuwa ni miradi ya watu binafsi na hata viongozi), bomba la mafuta la Tazama liko chali na hatukuona umuhimu kujenga bomba la kutoka Dar mpaka Mwanza (Elisante Muro alikuja na wazo na kupeleka Serikalini akanyang'anywa na kupewa yule Mu-Omani mwenye Nat Oil na leo ni mwaka wa 25 hatujajenga bomba la mafuta kutoka Dar hadi Mwanza kitu ambacho kingepunguza uagizaji wa malori ya mafuta na kuharibu barabara kutokana na udhaifu na uimara wa hati hati wa barabara).
Tukija kwenye ndege an vivuko vya majini, kwa miaka 25 tumekuwa tunafanya majaribio ya kuendesha shirika la ndege, meli na hata pantoni.
Sera inayoeleweka ingekuwa ni serikali kuweka mazingira mazuri na kuachia sekta binafsi imiliki na kuendesha shughuli za usafirishaji, serikali ibakie kuwa mmiliki wa Mataruma ya reli, viwanja vya ndege, bandari na kusimamia sheria na kanuni za mfumo wa uchukuzi huku yenyewe ikikusanya kodi (road toll na fuel taxes to be added) ya mauzo na matumizi ya barabara, reli, viwanja vya ndege na bandari.
Kwa kuwa viongozi na vyama havina vision kubwa na pana ya Uchukuzi na Miundombinu, tunaishia kurukaruka kama panzi kutoka project moja moaka nyingine, tunataka kumwaga lami kila kona na kukwepa kuchonga njia mpya ili kupanua mfumo wa barabara na kusambaza huduma mbali zaidi.
Kumalizia suala la Sera ya Uchukuzi, miaka 20 iliyopita niliuliza ni kwa nini Chalinze haikufikiriak kuwa inland port na kufanywa kuwa loading and unloading dry dock ya mizigo kwenda bandarini KUrasini?
Wazo lilinijia kuona kwa wenzetu kuwa pale Chalinze kuwa kwa kuwa ni njia panda ya kwenda kusini, kati na kaskazini, mizigo yote ingefika Chalinze, ikawa processed kutokana na kanuniza freighting na forwading ikapandishwa kwenye makontena (pia ujenzi wa Container warehouse) na kuwekwa kwenye treni kwenda bandarini. Hapo Chalinze TRA na Customs wangeweka kituo kikubwa cha ukaguzi wa mizigo inayoondoka Tanzania na hata ile ambayo si ya kuja Dar bali kwenda mikoani na nchi majirani, zingeshushwa kutoka kwenye meli na kuwekwa kwenye treni mpaka Chalinze.
Sasa tafakari ni jinsi gani uchukuzi huu na kufikiria hivyo ambako kungesambaza maendeleo pale Chalinze kuwa mji mkubwa wa kibiashara na hata viwanda, kupunguza msongamano wa watu na magari Dar na kupanua maendeleo mbali na Dar pekee.
Kwangu sera inayoeleweka ya uchukuzi ingesema kuwa kuna lengo la kuhakikisha kuwa muda wa usafiri kati ya Dar na Mwanza kwa gari unakuwa masaa 8 au 10, kwa treni unakuwa masaa 9 au 12, kwamba barabara zinahifadhiwa na kufanyiwa marekebisho kila mwaka, madaraja kupimwa uwezo wake wa kuhimili kila baada ya miaka mitano, kuwa badala ya kujenga daraja la kutoka Bahari beach mpaka KIvukoni, tungeweka feri za mwendo kasi za kutosha miaka 15 iliyopita kutoka Bagamoyo, Bahari beach, Kawe na Ferry, kupunguza msongamano, kivuko cha kigamboni kisingekuwa kitendawili tangu enzi za Nalaila Kiula.
Ni faraja kuona barabara za lami kila kona, lakini pia proper maintenance inahitajika kuhakikisha mifereji ya kando ni imara na imefunikwa na haigeuki kuwa dampo la takataka. Ama enforcement ya safety driving iwe ya hali ya juu kudhibiti madereva wanaoendesha reckless bila kufuata kanuni na wala kusiwe an haja ya kuweka matuta ya viazi barabarani kupunguza kasi.
La zaidi pamoja na major roadways ni kuwepo kwa barabara za watu wa miguu, baiskeli na hata madaraja ya juu kuvuka barabara (kama la Manzese) na service roads sambamba na barabara kuu.
Lengo liwe kurahisisha uchukuzi, ili kukuza uchumi, kuongeza ufanisi na kusambaza maendeleo. Naam hapo ndipo sera inaweza eleweka, wananchi watafurahia matunda ya Mzabuni kwa mapana na si kusomewa urefu wa barabara.