Duuh! Amepigwa kipigo cha mbwa koko!

Duuh! Amepigwa kipigo cha mbwa koko!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
1,679
Reaction score
2,123
Majigambo yake yameisha. Amepigwa kipigo cha mbwa koko! Amepigwa na Bwana Mkubwa!

Loo, aibu yake! Alivyoona amefaulu kuwaingiza mtegoni ndugu zetu, kwa hila zake, alifikiri atadumu kuwa mwerevu. Sasa ameshushwa chini kabisa. Kila mtu anamzomea, hata watoto wadogo wanambeza!

Alijiinua juu kwa majivuno, akiamini kwamba utukufu wake ungeendelea milele, lakini sasa amelala chali matopeni. Alijiona mshindi wa zama zote; sasa amebainika ni muongo, mwenye ghiliba, na udanganyifu wa kupindukia.

Aliwavuta wengi kwa ahadi zisizo na mashiko, akawashawishi kugeuka na kufuata njia zake. Lakini sasa, wale waliomfuata wameshtuka. Wanamtazama kwa macho yaliyofunguka, wakitambua kuwa waliuziwa mbuzi ndani ya gunia. Hakuna tena anayemsikiliza; hakuna anayemheshimu.

Aliwaza kuwa na enzi isiyoshindwa, lakini kumbe hakuona mwisho wake. Waliokuwa wanamtetemekea, sasa wanamkanyaga kwa miguu yao.

Alikuwa na sauti ya ngurumo sasa anaomboleza kwa kilio cha kimya, kilio cha waliokata tamaa. Hakuna tena mshirika wa kumtetea; wale aliowahadaa wameshtuka, wamerudi nyuma, wanasema, “Hatu-danga-nyiki! Tulipotea kwa kufuata ahadi zake hewa.” Waliomtumikia kwa bidii, wakidhani watanufaika, sasa wanamtupia lawama.

Miguu yake, iliyokimbilia maangamizi ya wengine, sasa imelegea. Hatetemeshi watu tena; badala yake anatetemeka mwenyewe kwa hofu.

Enzi zake zilikuwa za mbwembwe na kelele. Aliwaahidi wafuasi wake utukufu usio na mwisho, akisema, “Nitawapa kile mnachotaka, mkinifuata.” Lakini sasa, aliowalaghai wanamuuliza, “Yako wapi yale uliyotuahidi? Yako wapi yale uliyosema yatadumu milele?” Hana jibu. Hana la kusema.

Aliyejivuna, aliyedhani atakaa juu milele, sasa ameanguka. Amevunjika. Ameharibika. Na dunia inashangilia kwa sababu nguvu zake zimefika mwisho.

Lakini cha ajabu ni kwamba, ingawa amepigwa “knock out” na kuanguka chali, bado anawaza njama. Bado anatafuta jinsi ya kuinuka tena, jinsi ya kurubuni tena. Bado anatafuta nafasi ya mwisho ya kuwahadaa wasiokuwa macho. Bado anatafuta upenyo. Anafikiri, anapanga, anawaza—labda bado anaweza kudanganya tena, labda anaweza kujipenyeza na kujifanya mwenye haki kwa mara nyingine.

Lakini hapana! Mlango umeishafungwa. Hukumu yake imeshatolewa, na uamuzi hauwezi kubadilishwa.

Huyo si mwingine. Ni shetani a.k.a. Ibilisi. Kwa habari zaidi za anguko lake soma: Isaya 14:12-15; Ezekieli 28:12-19; Luka 10:18; Ufunuo 12:7-9; Ufunuo 20:10. Usimuogope tena shetani kuanzia leo. Ameishashindwa na kulegea kwa Jina la Yesu Kristo.
 
Hehehe
 
Back
Top Bottom