Duuuh! Hivi huu ushirikiana hadi ulaya upo kweli maana sasa sielewi.

Mr the dragon

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2017
Posts
1,937
Reaction score
3,718
Wadau JF mimi ni kijana mpambanaji katika harakati zangu nimekuwa inspired na waliofanikiwa wengi Tanzania mpaka ulaya.Kuna mzee mmoja hapa kitaa mwanza enzi tunakua alikuwa na pesa sana ila kwa sasa amefilisika kidogo japo bado pesa anazo.Huyu mzee huwa namfanyia kazi za malipo sometimes namsaidia tu kazi ndogo ndogo naishi karibu nae hivyo tumezoena sana.

Jana nikiwa napiga nae story tukawa tunaongelea masuala ya utajiri.Sasa Yule mzee akanambia kuhusu utajiri wa jamaa fulani ambae ni maarufu sana bongo ambaye huwa anani insipire sana na anawa inspire watanzania wengi kwamba siri ya huyo jamaa kufanikiwa alienda kwa mganga akanitajia hadi eneo.Kilichonifanya niamini ni jinsi Yule mzee alivyoongea simple kana kwamba ni kitu cha kawaida kabisa sasa mzee akanisoma saikolojia akaona kama nimeduwaa akanipa story za matajiri wengi zaidi maarufu hapa mwanza na utajiri wao wa kishirikina na akanipa hadi story yake na chanzo chake cha kufilisika ni huo huo ushirikina.kiukweli nilishangaa sana maana Yule tajiri maarufu bongo nzima namkubali sana na jamaa huwa anatueleza jinsi alivyopambana mpaka kufika alipo na anadai ni mcha Mungu sana na Si mimi tu ni watanzania wengi wanamkubali.huyu mzee amenifanya niwaone matajiri wote kuna ushirikina nyuma yao.

Mimi naamini katika Mungu sana nimeamua kuachana na hawa matajiri wetu wa bongo niwe inspired na waliofanikiwa huko nchi za wenzetu sasa nachojiuliza kwani na huko nako haya masuala ya ushirikina yapo ili kama ni hivyo nipambane na hali yangu tu.
 
Naungana na ww mkuu..
Mm nayajua hayo sanaa masuala ya Ndagu za utajili mm hua nawaangalia tu..
 
Si ujaribu kidogo kwenda kwa mganga uone kama hela zako zitaongezeka alafu ukisha-prove ndo unaacha kuwa inspired na matajiri wa kibongo,,,za kuambiwa inabidi uchanganye na zako
 
Si ujaribu kidogo kwenda kwa mganga uone kama hela zako zitaongezeka alafu ukisha-prove ndo unaacha kuwa inspired na matajiri wa kibongo,,,za kuambiwa inabidi uchanganye na zako
No hiyo ya kwenda kwa mganga hapana mkuu
 
Mtoa mada kuwa muwazi tu hapa anaongelewa ERICK JAMES SHIGONGO.
 
Hakuna uchawi, ulozi, wanga wala ushirikina. Ni story za kusadikika wajinga wanadanganyana na kuamini
 
Unamzungumzia nani? Shigongo au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…