Yani Mwanakijiji, nilikuwa naandika posti yangu ya hapo juu wakati wewe unatuma hii ya kwako. Halafu umesema yale yale ya kutingwa niliyo kuwa naandika wakati wewe unaposti! LOL!
Ha haa laaa!
Kutingwa haku justify kutotimiza ahadi na kunyamaza kimya. Inabidi ufahamishe uliowaahidi kwamba utashindwa kutimiza ahadi, kama ambavyo "ukitingwa" na ugonjwa unamfahamisha bosi kwamba siwezi kuja kazini kama nilivyoahadi kufanya kila asubuhi.
Huyu ambae unasema hatujui kama ametingwa tumawona hapa akishiriki mijadala kila siku tokea ahadi itolewe!
Kuhani.. kuna vitu nimejifunza katika maisha yangu haya mafupi.. la kwanza ni kuwa sayari ya dunia hainizunguki hata kama ningependa sana.
Pili, maisha hayana haki utakuwa unakatishwa tamaa mara nyingi
tatu, usiassume vitu bila kufuatilia, jaribu kufuatilia na tafuta chanzo
nne, kama inabidi kulalamika basi toa nafasi mtu kujieleza na upate kumuelewa kama hutakubali maelezo yake hilo ni jambo jingine..
tano.. usibatize watu majina tu kwa vile havikuendana na unavyotaka.
Katika kuandika kwangu kwingi kuna vitu ambavyo sijavifanya hadi sasa; sijawahi kumuita JK jina lolote ambalo si la kwake au siyo cheo chake; Pamoja na mgongano wangu na Lowassa sikuwahi kumbatisha jina lolote lile ambalo si la kwake.. nikitumia kejeli au kebehi vyote navitumia katika majina yao na vyeo vyao. Nikisema kitu kuhusu jambo fulani najaribu kufuatilia kuna usahihi wake na kupata maelezo zaidi badala ya kuchukulia assumption zangu kuwa ni sahihi..
Na mwisho, nikikosea najirudi kwani huo ndio uungwana na sitarajii kumpendezesha kila mtu. Lakini kama kutingwa watu hutingwa, na naamini ni ubinadamu kuwapa watu nafasi nyingine. Ni kwa sababu hiyo alipojiuzulu Lowassa makala yangu ya kwanza haikuwa ya kushangilia kuanguka kwake kama wengine...
Ndio maana kamwe sitaanzisha mada ya kumgusa mwanachama yoyote hapa kwa namna yoyote ya kumfanya awe duni, sitombatiza mtu jina lolote la kebehi au kejeli, na wala katika kupingana kwangu sitatumia hoja za nguvu. Sasa tuko tofauti naelewa..
so ambao mnajisikia mmesalitiwa, kwamba mioyo yenu imevunjwa kwa sababu "ahadi haikutimizwa" na wale ambao kwa namna moja wanaona kuwa "wameachwa solemba" naomba mgangamale tu mjipe moyo na msikate tamaa. Tumkumbushe ndugu yetu FMES kuhusu ahadi yake hiyo na tusimuone kafail kwa vile we didn't get what we wanted when we wanted tit.....