Dylan Kerr: Sina wasiwasi wowote na Tanzania Prisons

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Kocha mwenye leseni ya juu kabisa ya ufundishaji toka UEFA [leseni yake haina tofauti na zile za kina Brendan Rodgers, Mourinho n.k], Dylan Kerr ambae anaifundisha Simba S.C ametoa maneno mazito kuelekea mechi ya kesho dhidi ya Tanzania Prisons.

Akihojiwa na waandishi mbalimbali wa habari, amedai hana wasiwasi hata chembe juu ya kuchota point 3 toka Tanzania Prisons.. namnukuu...
“Nimeambiwa Prisons ni timu ngumu kwa Simba, lakini sina wasiwasi wowote, timu yangu ipo fiti na wachezaji wanaonyesha kuzoeana na tumeshazoea mazingira ya Mbeya”.

Pia akagusia, ubora wa uwanja wa Sokoine.. namnukuu..
"Ukizungumzia viwanja bora ni mmoja tu uliopo Dar es Salaam ule wa Taifa lakini viwanja vya mikoani si vizuri ila naamini mpaka Jumatano tutakuwa tumeuzoea zaidi uwanja huu na tutafanya vizuri" alisema Kerr.

Ikumbukwe, mara ya mwisho Simba S.C kukutana na Tanzania Prisons ilikua ni 28.02.2015.. Mnyama akiibuka na ushindi wa goli 5-0, huku Ibrahimu Ajibu akiweka rekodi ya kipekee ya kuwa;
1. Mchezaji mwenye umri mdogo kabisa kufunga magoli matatu katika mechi 1.
2. Mchezaji aliyefunga hat trick katika mda mfupi zaidi.. Alitumia Dk. 25 tu [magoli alifunga katika Dk. za 16, 21 na 41].

Kesho Ibrahimu Ajibu anaenda kuongoza maangamizi mazito Sokoine Stadium.. Na hii ni kutokana na Kiiza kutokua bado fiti.
Namuona Ibrahimu Ajibu akienda kuzivunja vunja rekodi zake.. na kuweka mpya.. Huku Simba S.C tukiwapatia dozi Nene zaidi Prisons.
 
sembo una maneno mengi...

Haya hebu lete visingizio kwa nini mmetiwa adabu huko Mbeya?

Mkuu hakuna la ziada.. Hawa Maafande wa Magereza leo wametuzidi ujanja tu.. Tunarudi Dar kujipanga vyema kwa akili ya mechi ijayo.
 
Last edited by a moderator:
Safi sana kwa kuwa muwazi...

Mkuu hakuna la ziada.. Hawa Maafande wa Magereza leo wametuzidi ujanja tu.. Tunarudi Dar kujipanga vyema kwa akili ya mechi ijayo.
 
Usitupe mawe wakati nyumba yako ni ya kioo
 

Trend ya makocha kuondoka inaelekea Simba SC baada ya Ruvu JKT (Minziro) na Coastal Union (Mayanja). Dalili za Kerr kutupiwa virago zimeanza kujitokeza.

Mungu mnusuru Kerr.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…