Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
Awali sim za mkononi zilipoingia zilikuwa ghali sana. Si line, si vocha, si handset. Hali hii ilisababisha kuibuka kwa vibanda vya sim. Hivi vilidumu hadi sim ziliposhuka bei vikafa natural death. Tukiangalia upande wa pili, tuna kompyta. Hizi nazo kutokana na uchache na gharama zake, baadhi ya wajasiriamali wakaanzisha internet ili kuwasaidia wale wasiomudu kumiliki kompyuta. Pamoja na kompyuta kuwako kwa muda wa kutosha, bado cafe zinashamiri. Swali langu, itafika wakati nazo zitakufa kifo cha kawaida bila kuhujumiwa?