Dynamic technology

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,478
Reaction score
3,659
Awali sim za mkononi zilipoingia zilikuwa ghali sana. Si line, si vocha, si handset. Hali hii ilisababisha kuibuka kwa vibanda vya sim. Hivi vilidumu hadi sim ziliposhuka bei vikafa natural death. Tukiangalia upande wa pili, tuna kompyta. Hizi nazo kutokana na uchache na gharama zake, baadhi ya wajasiriamali wakaanzisha internet ili kuwasaidia wale wasiomudu kumiliki kompyuta. Pamoja na kompyuta kuwako kwa muda wa kutosha, bado cafe zinashamiri. Swali langu, itafika wakati nazo zitakufa kifo cha kawaida bila kuhujumiwa?
 
Yawezekana, lakini hapa kitakachochelewesha ni miundo mbinu ya connectivity. Hili litakuja haraka pale tu wireless zitakapokuwa na gharama nafuu na kuwa na speed kubwa.
Likiangaliwa kibiashara inabidi hizo "internet cafes" zijibadili kulingana na mazingira ili ziendelee kufanya biashara, mfano pamoja na kuwepo na videos/tv World Cinema wamejipanga tofauti na wapo wanaendelea.
Hili la internet linahitaji miundo mbinu iliyo kaa vizuri na gharama nafuu.
 
Ughaibuni ninapoishi internet cafe ni chache sana, na zile zilizopo zinaendesha biashara zingine ili zijimudu. Karibu kila nyumba kuna internet access ya broadband na ni rahisi tu kupata hotspots. Vilevile mobile internet imetiliwa mkazo, hivyo unaweza kuwa na internet kwenye simu au laptop yako popote uendapo. Bei zake ni nafuu.
 
Ila kwa nchi nyingi za kiafrika itachukua muda sana kwa cafe kulegalega. Net ipo zaidi mijini, na pale wireless ikisambaa basi wenye cafe watajisogeza kwenye miji midogo. Ila biashara ni uwe na KSFs (key success factors) utadumu. Ninachoamini kuhusu cafe kwa Africa ni biashara ya kudumu
 
Hapana Hazitokufa kama unavyofikiri.......kwani people like me na wengine kama majasusi hawapendi kutumia net mahome as wanakuwa vulnarable kuwa traced back.......simu ni rahisi mtu kuitupa endapo wanausalama watakufuatilia ila computa service yake tu kwanza lazima ujulikane...... so any stupid professional who wants to shake other professionals will always want to stay in the darkness where no where to be found.....but computer might be replaced with smartphones in the near future...kama mimi i am using one.
 
Mziwanda,

Kama ulivyoashiria kwenye mambo ya simu na vibanda; ni kweli viliongezeka na sasa vimepungua kwa kasi kubwa. Ongezeko la watumiaji, ushindani kibiashara na mabadiliko ya teknolojia na kiuchumi zote ni moja ya sababu. Internet cafes nazo zitapungua kama vilivyo vibanda vya simu. Ongezeko la mitandao ya wireless na kupungua kwa bei za computer kutafanya hata vijijini ambako tungetegemea kuwe na cafes nyingi zaidi pale zinapopungua mijini kusiwe, kutokana na mjumuiko wa haya mawili, - wireless networks and hardware affordability.

Hapo awali cafes zilikuwa nyingi hata mijini kutokana na hali halisi kwamba wireless technology ilikuwa bado ndiyo inazindukazinduka. Sometimes teknolojia na matumizi yake huruka vihunzi. Tunakumbuka jinsi vile ilivyokuwa taabu kupata simu za ndani hapa kwetu Bongo, wakati nchi nyingine simu za ndani ndizo zilikuwa asilimia kubwa. Ghafla hizo tuliziruka na kuingia katika simu za mikononi. The natural trend ya ku-acquire teknolojia haikufata mtiririko, na hili la internet cafe laweza kuwa mojawapo.

SteveD.
 

yah, tunaimbiwa deile kuwa wakati wenzetu wanatembea sie tukimbie hadi tunapoteza step. Ni mengi tunaruka, mathalan modes of production from ujima na kuendelea. Hopefully cafes r here to stay kwani haitatokea watu karibu wote kuwa na access ya wireless
 

u mtu wa sistim ww
 

Kama huwezi kutumia computer yako na kujificha, hata ukitumia ya cafe watakudaka tu mwanawane ....

Heshima mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…