Dynasties: Kwa miaka zaidi ya 60, familia hizi zimekuwa zikiitawala Kenya kisiasa na kiuchumi

Dynasties: Kwa miaka zaidi ya 60, familia hizi zimekuwa zikiitawala Kenya kisiasa na kiuchumi

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
Kwa miaka zaidi ya 60 (miongo 6/6 decades) familia hizi zimekuwa zikiitawala Kenya Kisiasa na Kiuchumi!

Hawa wote kazi yao ni moja tu, kuiba mali za Wakenya na kucontrol Serikali ili kuhakikisha kuwa mali hizo za wizi wanazoiba zinalindwa!

Jaramogi alikuwa Muasisi wa KANU, Jomo alikuwa Kiongozi wa KANU, Daniel Moi alikuwa Kiongozi wa KANU, Uhuru ni Kiongozi wa KANU, Raila ni KANU B, na Gideon naye ni Kiongozi wa KANU!

Mbinu yao kuu ya kutawala ni kutumia Ukabila,

Wanaigiza kutetea maslahi ya Kikabila na kutengeneza Viongozi kwenye makabila mengine ili kufanikisha azma yao ya kupata akidi ya kuungwa mkono!

Kwa miaka zaidi ya 60 Wakenya wamekuwa mateka na watumwa wa Siasa hizi za Kikabila pasipo kujua ni akina nani waliowaweka Mateka!

Picha hii inawaonesha watekaji wa Taifa la Kenya, wameteka ardhi ya Kenya, Uchumi wa Kenya na Siasa za Kenya!

Kauli maarufu ya Kenya ni "Bora Uhai*

Yaani Wakenya wanaishi kwa kuvuta pumzi tu, maisha yao ni ya Mateso na wamekosa Matumaini,

Kuna tabaka la watu wachache ambao wao hawajui shida, hawajui kulala njaa, hawajui kulipa rent, hawajui kuhusu kero za Matibabu, Usafiri na kero nyinginezo, hawa wanaishi kama wapo Paradiso!

Tabaka lingine ni la Wakenya Milioni 50 ambao hawa wanaishi wakiwa hawaijui kesho yao, hawana uhakika na matibabu, hawana uhakika na mavazi, hawana uhakika na malazi, wanashindwa kusomesha watoto, wanashindwa kumudu gharama za vyakula, hawa ndio ambao wanaendesha Kampeni ya "Lower food prices"

Wanaishi kwa hustling!

Baada ya miaka 60 anatokea mmoja wao anayejua shida zao (Hustler) kuomba nafasi ya Urais, nao wanamuelewa na kumuunga mkono!

Dynasties baada ya kuona huyu Hustler anataka kuwafungua Wakenya toka kwenye Mateka wa hizi familia chache zinazowakandamiza na kuwanyonya nao wanapambana kuhakikisha kuwa Wakenya wanaendelea kuwa watumwa wao!

Wakati wa MUNGU ukifika hakuna wa kuuzuia!

Saa ya Ukombozi kwa Wakenya ni sasa na mwenye Funguo za kuwafungua Wakenya toka kwenye vifungo vya Ukabila ni Mh. William Samoei Ruto.

Screenshot_20220328-162310.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bahati nzuri ni kwamba sasa hivi utawala na madaraka nchini Kenya hayapo 'concentrated' kwa mtu mmoja. Kama ilivyokuwa hapo awali, ambapo rais alikuwa mungu-mtu, ambaye ameshikilia maendeleo, ndoto na maisha ya wakenya wote mikononi mwake.

Madaraka yalisambazwa kwenye mihimili na taasisi huru za kiserikali(ambazo hadi sasa hivi zinazidi kuimarika kwa kasi) na pia upinzani. Chini ya katiba mpya ya Kenya 2010. Matokeo yake ni kwamba shughuli nchini zinaendeshwa kisheria, kupitia mihimili yote mitatu. Hata pale ambapo hayaendani na hulka za rais ambaye yupo usukani.

Madaraka ambayo rais alibaki nayo ni 'ceremonial', kwa kiasi kikubwa. Kumaanisha kwamba rais sanasana ni kama nembo tu ya taifa na sura ya nchi kimataifa. Tena linapofika kwenye suala la maendeleo, madaraka yakasambazwa zaidi, chini ya mfumo mpya wa ugatuzi. Kumaanisha gatuzi zote 47 zina uhuru wa kujiamulia mkondo wanaotaka kuufata na kujipangia maendeleo wanayoyataka. Kupitia bunge za 'kaunti'(county assemblies), wizara zao na viongozi wao mashinani.

Gatuzi zote zina rais(gavana) makamu wake(naibu gavana), seneta ambaye anawakilisha gatuzi husika kwenye serikali kuu, ndani ya bunge la seneti(upper house). Alafu pia kuna wawakilishi wa kila wodi(wards) kwenye bunge za gatuzi, yaani MCAs(madiwani).

Tofauti na nchi nyingi barani Afrika. Urais au kiti cha urais, siasa na mazagazaga yote yanayoendana na nafasi hiyo, sio mwisho au mwanzo wa yote yanayoendelea ndani ya taifa la Kenya.

Alafu sijaelewa kwanini hujataja yanayomhusu rais mstaafu Mwai Kibaki. Wala hujasema pia kwamba rais wa sasa Uhuru Muigai Kenyatta alikuwa upinzani kwa mihula miwili ya utawala wake. Au kwamba rais Daniel Arap Moi aliupata urais, bila kunuia wala kupanga, sawa tu na rais wa sasa nchini Tz. Baada ya kifo cha ghafla cha aliyemtangulia, Mzee Jomo Kenyatta.
 
Bahati nzuri ni kwamba sasa hivi utawala na madaraka nchini Kenya hayapo 'concentrated' kwa mtu mmoja. Kama ilivyokuwa hapo awali, ambapo rais alikuwa mungu-mtu, ambaye ameshikilia maendeleo, ndoto na maisha ya wakenya wote mikononi mwake.

Madaraka yalisambazwa kwenye mihimili na taasisi huru za kiserikali(ambazo hadi sasa hivi zinazidi kuimarika kwa kasi) na pia upinzani. Chini ya katiba mpya ya Kenya 2010. Matokeo yake ni kwamba shughuli nchini zinaendeshwa kisheria, kupitia mihimili yote mitatu. Hata pale ambapo hayaendani na hulka za rais ambaye yupo usukani.

Madaraka ambayo rais alibaki nayo ni 'ceremonial', kwa kiasi kikubwa. Kumaanisha kwamba rais sanasana ni kama nembo tu ya taifa na sura ya nchi kimataifa. Tena linapofika kwenye suala la maendeleo, madaraka yakasambazwa zaidi, chini ya mfumo mpya wa ugatuzi. Kumaanisha gatuzi zote 47 zina uhuru wa kujiamulia mkondo wanaotaka kuufata na kujipangia maendeleo wanayoyataka. Kupitia bunge za 'kaunti', wizara zao na viongozi wao mashinani.

Gatuzi zote zina rais(gavana) makamu wake(naibu gavana), seneta ambaye anawakilisha gatuzi husika kwenye serikali kuu, ndani ya bunge la seneti(upper house). Alafu pia wana wawakilishi wa kila wodi(wards) kwenye bunge za gatuzi, yaani MCAs(madiwani).

Tofauti na nchi nyingi barani Afrika. Urais au kiti cha urais, siasa na mazagazaga yote yanayoendana na nafasi hiyo sio mwisho au mwanzo wa yote yanayoendelea ndani ya taifa la Kenya.

Alafu sijaelewa kwanini hujataja yanayomhusu rais mstaafu Mwai Kibaki. Wala hujasema pia kwamba rais wa sasa Uhuru Muigai Kenyatta alikuwa upinzani kwa mihula miwili ya utawala wake. Au kwamba rais Daniel Arap Moi aliupata urais, bila kunuia wala kupanga, sawa tu na rais wa sasa nchini Tz. Baada ya kifo cha ghafla cha aliyemtangulia, Mzee Jomo Kenyatta.
Iyo katiba yenu nzuri sana...hapa tz Raisi ndio kila kitu...mambo ya kale sana haya
 
Kwa miaka zaidi ya 60 (miongo 6/6 decades) familia hizi zimekuwa zikiitawala Kenya Kisiasa na Kiuchumi!

Hawa wote kazi yao ni moja tu, kuiba mali za Wakenya na kucontrol Serikali ili kuhakikisha kuwa mali hizo za wizi wanazoiba zinalindwa!

Jaramogi alikuwa Muasisi wa KANU, Jomo alikuwa Kiongozi wa KANU, Daniel Moi alikuwa Kiongozi wa KANU, Uhuru ni Kiongozi wa KANU, Raila ni KANU B, na Gideon naye ni Kiongozi wa KANU!

Mbinu yao kuu ya kutawala ni kutumia Ukabila,

Wanaigiza kutetea maslahi ya Kikabila na kutengeneza Viongozi kwenye makabila mengine ili kufanikisha azma yao ya kupata akidi ya kuungwa mkono!

Kwa miaka zaidi ya 60 Wakenya wamekuwa mateka na watumwa wa Siasa hizi za Kikabila pasipo kujua ni akina nani waliowaweka Mateka!

Picha hii inawaonesha watekaji wa Taifa la Kenya, wameteka ardhi ya Kenya, Uchumi wa Kenya na Siasa za Kenya!

Kauli maarufu ya Kenya ni "Bora Uhai*

Yaani Wakenya wanaishi kwa kuvuta pumzi tu, maisha yao ni ya Mateso na wamekosa Matumaini,

Kuna tabaka la watu wachache ambao wao hawajui shida, hawajui kulala njaa, hawajui kulipa rent, hawajui kuhusu kero za Matibabu, Usafiri na kero nyinginezo, hawa wanaishi kama wapo Paradiso!

Tabaka lingine ni la Wakenya Milioni 50 ambao hawa wanaishi wakiwa hawaijui kesho yao, hawana uhakika na matibabu, hawana uhakika na mavazi, hawana uhakika na malazi, wanashindwa kusomesha watoto, wanashindwa kumudu gharama za vyakula, hawa ndio ambao wanaendesha Kampeni ya "Lower food prices"

Wanaishi kwa hustling!

Baada ya miaka 60 anatokea mmoja wao anayejua shida zao (Hustler) kuomba nafasi ya Urais, nao wanamuelewa na kumuunga mkono!

Dynasties baada ya kuona huyu Hustler anataka kuwafungua Wakenya toka kwenye Mateka wa hizi familia chache zinazowakandamiza na kuwanyonya nao wanapambana kuhakikisha kuwa Wakenya wanaendelea kuwa watumwa wao!

Wakati wa MUNGU ukifika hakuna wa kuuzuia!

Saa ya Ukombozi kwa Wakenya ni sasa na mwenye Funguo za kuwafungua Wakenya toka kwenye vifungo vya Ukabila ni Mh. William Samoei Ruto.

View attachment 2167116

Sent using Jamii Forums mobile app
Leo ndo nimejua Raila ni KANU alooo
 
Hilo la kenya hta hapa Tanzania lipo sana na nilishalizungumzia

Bandiko jenyewe ni hili hapa

elite class ni watu wasiozidi elfu hamsini na ndio wafaidika wakuu wa keki ya taifa

Wameshika nyanja zote za uchumi na kitovu chake kikuu ni kamati kuu ya chama cha mapinduzi.

Wote hawa hawana njaa na hakuna mtoto anaetoka kwenye hii class akasoma kayumba school au akakosa ajira akimaliza chuo na huwezi kukuta wanakaa sehemu ambazo umeme na maji ni changamoto

Na wameweka vikwazo kibao kwa watu wasiotoka kwenye class yao kujikwamua kiuchumi, ndio maana ukianzisha kabiashara kadogo unakutana na lundo la tozo za vibali.

Ndio maana wengine wameamua kuwa chawa tu ilimradi waingie kwenye hiyo class, mfano halisi ni bashite amejipenyeza penyeza mpaka kaingia ndani ya system na leo inamfaidisha kwa kumlinda kwa madudu aliyofanya
 
Wakati Uhuru akitumia ukabila mpaka yeye Ruto kuwa vice akuliona hilo!,mpaka sasa ameona maji yamemfika shingoni.
Kikuyu na Jaluo wameshikana Ruto maji ataita mma.
 
Hawa Watu Shida Sana Yaani Kubandua Wameshindwa Kutumia Lugha Fasaha
Kubandua ni lugha fasaha kabisa kama walivoitumia hapo. Sema labda wewe ndio umejikita kwenye lugha za kihuni, za mitaani. Ambazo ndio huwa zinatumia maneno flani ya lugha vibaya na kupindisha maana halisi ya maneno hayo.
 
MK254 weee unatoka ukoo gani? Au nawe ni pangu pakavu tia mchuzi?

Hehehe!! Nipo kwenye ukoo wa katiba yetu hii nzuri ambayo inatulinda, imemchukua rais Uhuru muda mrefu kuizoea hii katiba, amri zake nyingi nyingi zimekua zikibatilishwa hadi basi, mkiwa na katiba nzuri hautajali nani ataingia ikulu maana atanyooshwa akae, nchi itang'aa, mtapaa kimaendeleo na kuboreka kijamii......
 
Sio sawa wewe nyang'au. Unabandua kitu kilichobandikwa (mathalan kwa gundi), na unaondoa kitu kilichowekwa. Sasa nani "alimbandika" huyo jamaa hadi abanduliwe?
Lugha ya kishairi- inatilia mkazo wa mabadiliko ya uongozi.Sawa na Mwalimu aliposema kung'atuka- kuachia madaraka.
 
Back
Top Bottom