E-Fm mnaboa

Simara

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2014
Posts
7,512
Reaction score
23,925
Sijaona mahali nitakapotolea malalamiko yangu zaidi ya JF, kiukweli E-Fm sijajua mnalenga nini utakuta mtu unasikiliza kipindi cha maana kabisa asubuhi mara inapigwa singeri!!! Huwa mnatutoa kwenye mood kabisa!! mfano mwingne unakuta mnaweka bongo fleva....mara nyimbo za zamani za dansi mkitoa mnaweka singeri!! yaan hamfanyi vitu kimpangilio...tengeni muda wa singeri ni singeri....bongo fleva ni bongo fleva...singeri asubuhi asubuhi anasikiliza nani?!!!
 

Kwa maelezo hayo bila shaka humo studioni kuna vichaa tena vichaaa haswa
 
Inaboa sana unasikiliza taarifa za maana mara wanaeka nyimbo sijui 'tekenya tekenya' wawe wanaangalia na muda wa kupiga hizo nyimbo.
Sasa ww ulitaka hzo taarifa unazoita za maana zisindikizwe na nyimbo gani labda......???
 
Ungewapigia simu ukawaambia ingekua ni busara zaidi!
 
Umelazimishwa kusikiliza hizo singeli? E.fm inaendeshwa na singeli soko lao ndipo lilipo ukiona singeli inakuboa ujue wewe efm siyo type yako
 
Kuna huyu aliyepewa kipindi cha kigenge ananiboa sana tena sana.Kicheko alikuwa anakinogesha kuliko huyu anayepiga kelele kama kakabwa koo.Kila neno analoliongea anaweka neno lake la looooooo! Mpaka nakereka.Kipindi cha kigenge kimepoteza mvuto.
 
Mimi nilishaacha kusikiliza maredio toka miaka ya 2002,tangu hapo Mimi nanunua TV tu wala sijawahi kusikiliza matangazo ya radio tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…