DSN
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 2,837
- 1,679
Leo nilikuwa nasikiliza kipindi East Africa Radio ambacho kinaendeshwa na Misago,alikuwa anafanya mahojiano na Msanii maaarufu kanda za kaskazini JCB,kuwa anaionaje hali ya Arusha na maswala mazima ya uchaguzi na maendeleo yake.Katika kuonyesha kweli tulipofika ni zama nyingine JCB alisema hali ni shwari baada ya uchaguzi na kuwa wanampongeza Msela [akimaanisha Joshua Nasari].
Hakika nilichokiona ni picha tofauti sana ambayo imezaa kuwa tuko zama za kizazi kipya na kina lugha yake ambayo Joshua Nasari anaijua na kuiongea yeye na vijana wenzie yani mpaka JCB anajisahau huyo anamwita MSELA [ni mheshimiwa mtarajiwa]. Ama kweli hizi ni zama nyingine kabisa na kila zama na vitabu vyake.