Poleni ila Watanzania sidhani kama mpo tayari kwa siasa za upinzani au demokrasia, wananchi wenyewe washajichokea, kama hamkuwatoa CCM kwa mzuka mliokua nawo 2015 sioni tena, ingekua mnachagua kwa kuzingatia hoja, nahisi hii awamu ingeshindwa pakubwa maana had sasa hawana kitu hata kimoja hivi wamekamilisha kikaonekana, SGR yenyewe iliyokua ianze kutumika mwaka jana, nimesoma sehemu waziri mkuu anasema ndio sasa imefikia 77%
Aisei mnalo, poleni lakini, sema tu hili la corona duh! Yaani hamna jitihada zozote, tushukuru Mungu hiki kirusi kimehurumia Afrika kiaina maana kwa jinsi Tz imejichokea na kukata tamaa kwenye hili la corona, watu wangepukutika sana.