EAC wajadili mchakato sarafu moja

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
EAC wajadili mchakato sarafu moja Monday, 17 January 2011 20:13

Mussa Juma, Arusha

NCHI za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC), jana zilianza mchakato wa kuanza matumizi ya sarafu moja kwa nchi hizo , ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya jumuiya hiyo.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Balozi Juma Mwapachu, akizungumza katika kikao hicho, alisema wajumbe tisa katika nchi tano za jumuiya hiyo wamechaguliwa kushughulikia suala hilo.

Alisema umoja wa fedha katika nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki utasaidia sana kukuza uchumi na kuimarisha mahusiano katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara.

" Leo tumeanza na kikao cha kwanza cha kuanzisha mchakato wa kuwa na umoja wa fedha, hadi kufikia mwezi Machi nadhani tutakuwa katika hatua nzuri,"alisema Mwapachu.

Alisema hadhani kama kutakuwa na ugumu wa kufikia kuwa na umoja wa fedha kwani tayari itifaki mbalimbali za jumuiya hiyo zimesainiwa na kuwa na mafanikio.

"Tulikuwa na itifaki ya umoja ya forodha , tukaja soko la pamoja sidhani kama hili la umoja wa fedha litakwama"alisema Mwapachu.

Katika majadiliano hayo ya umoja wa fedha, kimsingi jana wawakilishi wa nchi zote wanachama wa jumuiya hiyo, walikubaliana kuanza majadiliano ya kufikia hatua ya kuwa na sarafu moja.

Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki hadi sasa ni Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi ambao ndio wanashikilia nafasi ya Uenyekiti wa jumuiya hiyo.

 
" Leo tumeanza na kikao cha kwanza cha kuanzisha mchakato wa kuwa na umoja wa fedha, hadi kufikia mwezi Machi nadhani tutakuwa katika hatua nzuri,"alisema Mwapachu.

Hivi kinachoanza ni benki kuu moja au sarafu moja? Are we not placing a cart before horses..................
 
wakiweka bank kuu moja tunataka ikae Arusha, na si Nairobi kama kipindi kile, kwasababu wakenya walituonea sana ile bank ya kipindi kile. tuwe macho sana kwa sasaivi.
 
wakiweka bank kuu moja tunataka ikae Arusha, na si Nairobi kama kipindi kile, kwasababu wakenya walituonea sana ile bank ya kipindi kile. tuwe macho sana kwa sasaivi.
Labda Mafisadi wawe wameshatwaliwa na Bwana ndio pesa zitakuwa Salama
 
Hii kitu ni bad idea especially in light ya matatizo tunayoyaona katika Euro zone. Kwa kile ambacho wakuu wanataka, ile East African Currency Board (EACB) ndiyo inayoweza kurudi kuzireplace member states Central Banks. Tatizo kubwa la Monetary Union au muungano wowote ule ni uachiaji wa nguvu za kutunga sera na kuzisimamia mamlaka nyingine. Hii monetary union inamaanisha BoT watasalimisha uwezo wao wa kutunga na kusimamia monetary policy kwa EACB or whatever the new currency board/regional central bank is going to be called.

Binafsi ningependa kuona Tanzania ikiweka conditionalities za kuingia katika Monetary Union hii kama zile alizoweka Gordon Brown wakati wa mchakato wa Uingereza kuingia katika Eurozone. Na test hizo zilikuwa ni;


Kwa hizo za juu unaweza kusubstitute the UK for Tanzania na Euro for the proposed East African Shilling.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…