Hatimaye Mkonga wa Chini ya Bahari wa SEACOM Uko LIVE.
Sasa ni nini kinafuata? Unaweza kupata huduma kwa sasa kupitia Local ISP ambazo tayari zimeshajiunga.
Tusahau Siasa zote tulizosikia juu ya bei nk. Je, Bei halisi zikoje?
- ISP lazima zinunue SEACOM Minimum ya 1 pair of Fiber ambayo ina Capacity ya 155 Mbps (Full Duplex). SEACOM wanauza 1 Mbps Full Duplex (1024 Kbps) kwa USD 750.00 Kwa Mwezi Full Duplex au $ 375 Kwa Half Duplex ambayo SEACOM Hawauzi. Originally bei ya 1 Mbps full duplex kupitia VSAT (Best Price Wholesale from Satellite Operators) ilikuwa ni USD 5120.
- Kwa hiyo ISP inahitaji kununua SEACOM 155 Mbps kwa USD 116,250.00. Mkataba wa chini ni Mwaka Moja. So, total amount ni USD 1,395,000/=, Bila ya shaka hiki ni kiasi kikubwa sana kuwekeza kwa mara moja. Hii ni mbali ya gharama za Inland Fiber utakayotumia kuunganisha SEACOM Hub Station na Network Operating Centre (NOC) yako pamoja na Equipment zingine.
- So, what next?
- ISP nyingi sasa zina woga wa kujua watafanya vipi biashara kwa kuwa mara moja mapato yao yatapungua sana kutokana na bei kushuka sana kwa kama asilimia 60%. Pili kuuza capacity yote ya 155 Mbps kwa mwaka si kazi rahisi sana.
- Biggest ISP kwa sasa kwa miaka yote at best inaweza kuwa imeuza si zidi ya 100 Mbps.
- Sasa je ISP ziwauzie wateja kiasi gani?
- Na wafanye nini ili wasiingie katika loss na waendelee kutoa huduma na kuwalipa wafanyakazi wao vizuri?
- Je wataweza kuuza volume kubwa na kwa wateja wengi ili warudishe gharama zao na faida?
Kwa uzoefu na maoni yangu, huenda bei ikawa kama ifuatavyo:
- Kwa wateja Wakubwa yaani ISP na makampuni ambayo hayawezi kununua 155 Mbps lakini wanaweza kununua zaidi ya 50 Mbps bei kwa 1 Mbps huenda ikawa $ 850 kwa mwezi. Je wao watauza Retail kwa kiasi gani?
- Kama Watanunua pungufu ya 50 Mbps bei kwa 1 Mbps huenda itakuwa $ 950. Je wao watuza retail kwa kiasi gani?
- Bei hizo ni mbali ya mteja kuunganishwa kutoa NOC kwenda kwa huyo Mteja mkubwa. Say Installation itakuwa $ 5000 kwa Cable ya Fibre na Backup Link yake. Maintenance itakuwa $ 1000 kwa mwezi. Je bei za rejareja zitakuwaje?
- Bei za Rejareja bila ya shaka zinaweza kufanana na hizi hapa chni baada ya kuzingatia Investment pamoja na mambo yote niliyoyataja hapo juu (Bandwidth zote ni full Duplex):
- 128 Kbps - $ 230 Per Month - Bei ya sasa $ 640 Per Month (Best Price)
- 256 Kbps - $ 460 PM - Bei ya sasa $ 1280 pm
- 512 kbps - $ 920 pm - bei ya sasa $ 2560 pm
- 1024 kbps (1 Mbps) - $ 1840 - bei ya sasa $ 5120
- Bei hizo ni mbali na Equipment na Installation ambazo gharama zake zinaweza kuwa kati ya $ 1000 hadi $ 3000.
Hii ina maana bei halisi ya Bandwidth kwa ulinganifu wa Full Duplex itapungua kwa karibu asilimia 60%. Lakini je ISP zitakubali kushusha bei au kuwaongezea wateja wao Bandwidth ili mapato yao yasianguke?