East Africa Fibre Optic Cable: Connectivity, issues & progress

sawa mkuu tuendelee kusubiri tuone kama itakawa hivyo.Kama watashusha itasaidia sana kuwaongezea wateja.Mimi hofu yangu ni kwamba Je ISP wetu wanauwezo wakununu hiyo 155 mbps? kama wapo ni wachache sana.

Mkuu kwa Mujibu wa SEACOM sasa hivi Wateja 8 wameshapatikana. Kwa uzoefu wangu hao wanaweza kuwa:
- TTCL
- SimbaNET
- Six Telcom
- UDSM ( Siyo UCC)
Sina uhakika makampuni ya simu kama:
- VODACOM
- ZANTEL
- CELTEL
- TIGO

Kwa kuwa sioni kama hiyo Internet ya 155 Mbps wataiuza vipi kwa watumiaji wa simu za kiganjani la laptop kupitia katika infrastructure zao ambazo ziko limited kuwapa wateja capacity au bandwidth kubwa kwa gharama nafuu. Of course uwezo wa kununua kutoka SEACOM wanao.
 
Mkuu Allien,

Nashukuru kwa uchambuzi, ila nilivyoanza kusoma uchambuzi wako umeanza kuandika

ISP lazima zinunue SEACOM Minimum ya 1 pair of Fiber ambayo ina Capacity ya 155 Kbps (Full Duplex). ...

Kwa hiyo ISP inahitaji kununua SEACOM 155 Kbps kwa USD 116,250.00...

Pili kuuza capacity yote ya 155 Kbps kwa mwaka si kazi rahisi sana...

HALAFU ukaendelea (conclusion)
Kwa wateja Wakubwa yaani ISP na makampuni ambayo hayawezi kununua 155 Mbps lakini ..


Hii habari kwangu ni mpya, lakini natumaini 155Kbps kwenye paragraph za juu ulimaanisha 155Mbps?
 
ALLIEN,
nakubaliana na maoni yako mengine lakini hili,
"Kama ulikuwa una ISP A yenye mapato ya USD 2 Million kwa Mwaka, itabidi wateja wake waongezeke kwa asilimia 60% ili apate mapato yale yale vinginevyo labda awalazimishe wateja wake wakubali kuongeza BW kuliko kupunguziwa bei kitu ambacho kitategemea mteja na mteja na bajeti zao."
Sidhani kama ni tatizo kwao, naona unaangalia upande mmoja zaidi hebu fikiria kati ya hizo $2 Million dollars ni kiasi gani kinawabakia wakiisha lipa hao jamaa wanao own hizo international gateways.
Halafu kuna mambo umeongelea kuhusu simu za viganjani and Laptop. Hii mambo ipo hivi ISP ikiisha nunua hiyo 155Mbit/sec, hiyo ni Backbone yao kutoka SeaCom kwenda NOC ya ISP. Hivyo basi SEACOM inamhakikishia ISP bandwidth hiyo kwa muda wote, kitu ambacho ni tofauti kabisa na ISP hawawezi kukuhakikishia bandwidth kiasi fulani wakati wote.
 
wazee asanteni kwa mada hii ya manufaa kwetu, lakini naomba mlekebishe hapo naona mnaweza kuwachanganya watu, SEACOM Wanauza 155 kbps au 155 mbps kwa mwaka kwa sh. 116,250.00...? naomba usahihi tafadhali.
 
La muhimu sirikali ianzishe "ka ewura " kengine bei zipangwe, haiwezekani watu wachumie shida za wenzao na unafuu ukija eti mapato yatapungua! Bei ziende chini tuu, hata Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania alilisemea hilo kwenye ufunguzi, bei kwenda chini. Na Waswahili tufaidike sasa!!!
 
wazee asanteni kwa mada hii ya manufaa kwetu, lakini naomba mlekebishe hapo naona mnaweza kuwachanganya watu, SEACOM Wanauza 155 kbps au 155 mbps kwa mwaka kwa sh. 116,250.00...? naomba usahihi tafadhali.
Mkuu SEACOM wanauza kwa 155 mbps na sio 155 kbps.
 
Mkuu Allien,

Nashukuru kwa uchambuzi, ila nilivyoanza kusoma uchambuzi wako umeanza kuandika







HALAFU ukaendelea (conclusion)



Hii habari kwangu ni mpya, lakini natumaini 155Kbps kwenye paragraph za juu ulimaanisha 155Mbps?

Asante sana Mkuu;

Hakika nilikuwa nina maana ya 155 Mbps. Niwieni radhi kwa kosa hilo.
 

Mkuu Jua Kali;

Maoni yangu binafsi bado yako palepale na naamini TIME WILL TELL.

Actually katika mfano wangu huo nilioutoa USD 2 Million inaweza kuwa gross income kabla hujatoa running/operating costs zingine zikiwemo za support, maintenance, mishahara nk.

Pili katika zama hizi kama ISP i ukinunua 155 Mbps kisha isimuuzie mteja BW ya kweli, itakuwa kwa manufaa ya nani? Maana hiyo 155 Mbps kuiuza si mchezo ni BW kubwa sana unless kama watumiaji wataongezeka kwa kiasi kikubwa sana.

Hata sasa, si ISP zote zenye hako kamchezo kaahidi BW kiasi fulani kisha wakakubania.

Napenda pia kutoa ushauri kwa wateja wote kuwa kama unahisi kuna ISP inakufanyia mchezo huo, dawa ni kuinstall Network Management Tool/System au Device ambayo itakusaidia kwa uhakika kujua BW ya kweli unayopata pamoja na mambo mengine.
 
wazee asanteni kwa mada hii ya manufaa kwetu, lakini naomba mlekebishe hapo naona mnaweza kuwachanganya watu, SEACOM Wanauza 155 kbps au 155 mbps kwa mwaka kwa sh. 116,250.00...? naomba usahihi tafadhali.

Mzee wa Castle;

Nashukuru sana, nimeshafanya marekebisho. SEACOM wanauza a minimum ya 1 pair yenye Capacity ya 155 Mbps.
 

Mkuu;

Bei zitapungua bila shaka kama nilivyogusia. In fact kama uko DSM najua kuna ISP 2 tayari wameshaunganisha SEACOM na watakuwa LIVE kwa wateja wao kwa bei zitakazofanana na hizo.

Of course EWURA ipo na ni TCRA. Ila wao wanaregulate bei ya SEACOM kwa ISP ziwe standard lakini si retail prices. At the end of the day itakuwa kama zilivyo bei za aitime kwa simu nikiwa na maana kila ISP itapanga bei zake.
 
tatizo langu ni hii serikali yetu yaani hadi Gharama zije kulingana na ghaama za sasa itapita miaka miwili au zaidi! Yaani hadi bei zishuke ni hadi pale hawa ISP watakaposema tumesharudisha gharama za vifaa vyetu vya HUAWEI tulivyonunua. Juzijuzi tu jamaa wa VODA walizindua huduma ya wireless ya 32KB??? yaani unafungua page moja unaenda dukani kunywa soda ukirudi unakuta text tu picha bado na unalipa 40000 less kima cha chini kwa mwezi.
 

Haa haaa;

Mkuu, nimeiona comment hii kule kwa Mkuu wa Wilaya . . . .

Kuna kitu ambacho kinaendelea sasa ambacho wengi hawajui. TEAMS Submarine Cable inategemea pia kuvuta toka Mombasa before end of this year. EASSY cable nayo iko njiani. Bila shaka bei za SEACOM zitashuka zaidi Fiber nyingine zitakapokuja.

Mpaka sasa sina uhakika kama infrastructure za Cellular Networks zina uwezo wa kutoa dedicated BW kubwa kwa bei ya chini. Nyingi zinauza kwa mgao wa GB kutokana na limitation.

Habari njema ni kuwa wakati SEACOM wanatest LIVE, Dodoma nayo ilikuwa imeunganishwa tayari na TTCL kupitia TANESCO Fiber. So Waheshimiwa, PMO na UDOM soon watakuwa LIVE.
 
hayo makampuni baadhi ya mafisadi ni wakurugenzi na wenyeviti wa boards tuwe makini wanaweza kufanya njama SEACOM ife
 
Jambo la muhimu tu subiri tuone hizo gharama zitashuka kwa % ngapi.nimesoma gazeti la mwanachi leo wanadai kuwa mbps itauza kwa $ 100,na kwa wanafunzi watakao kuwa na simu ambazo zina Internet watalipia kwa mwezi $ 20
 
Jambo la muhimu tu subiri tuone hizo gharama zitashuka kwa % ngapi.nimesoma gazeti la mwanachi leo wanadai kuwa mbps itauza kwa $ 100,na kwa wanafunzi watakao kuwa na simu ambazo zina Internet watalipia kwa mwezi $ 20
Hii itakuwa ni habari nyema sana kwetu.1 mbps kwa $ 100 sio mbaya naona itatufaa wengi!
 

Mkokotoo mzuri mwana.

Ila usiwe na wasiwasi sana, kwa kutumia data zako hapo naweza kujipa moyo hivi:

- Kuhusu ugumu wa kuuza 155Mbps: kumbuka kwamba walikuwa hawauzi nyingi kwa sababu bei zipo juu, na hivyo demand inakuwa chini.

- Kama kuna mtu alikuwa ananunua 1Mbps kwa $5,120, na kama sasa hivi SEACOM wanauza 1Mbps kwa 750, maana yake ni kwamba huyu mtu anauwezo wa kupata bandwidth zaidi ya x6 at the same price. Kwa hiyo pengine ISP aliyekuwa anauza at least 30Mbps itaweza ku-switch to SEACOM kwa kuwaongezea tu bandwidth wateja wake na kuashawishi wabaki naye. Wateja wakiondoka ujue kuna ISP mwingine has a better idea, which is good for all of us anyway. Swala pengine litabaki za wapi anazitoa hizo upfront fees anazolipa SEACOM. Na sidhani kwamba ni kweli watashindwa kuzipata. Kumbuka SEACOM hawana interest ya kumuuzia kila tom-dick-and-hurry. Kwa hiyo pengine wewe na mimi binafsi ambao tunaona hiyo pesa ni nyingi hatutaweza kuunganishwa moja kwa SEACOM

- Kwa sababu cost za entry ziko juu kidogo, pengine kitakachotokea ni kwamba ISP watapendelea ku-push more bandwidth zaidi ya kushusha prices sana. Halafu baadaye wateja wanavyoongezeka ndivyo bei itakavyozidi kushuka. ISP wachache watakaotaka ku-disrupt market (I am thinking Zantel, Tigo) wanaweza wakaingia na lower prices moja kwa moja, watakubali ku-absorb loses mwanzoni lakini watumiaji wa mtandao wao wataongezeka sana kwa sababu ya lower prices, na in no time they will be making a killing.

- Kumbuka kama ISP wakigoma kushusha prices ili wale wao tu faida ya SEACOM kuingia mjini, basi ujue watakuwa wanakula pengine zaidi ya profits walizokuwa wanakula mwanzoni. More profits zita attract wajasiriamali kuingia huko wanaotaka nao some piece of the tasty cake. More wajasiriamali means more competition na prices zitashuka tu. Hivyo ndivyo free market inavyofanya kazi. Ili kuwepo na free market inabidi kusiwe na mizengwe kwenye kuuziwa bandwidth na SEACOM as long as mtu ana hela yake ya kutosha.

- Kwa upande wa bei, sinauhakika nimekuelewa umehitimisha vipi lakini nachukulia uko sawa. I assume ume-assume a 1:1 contention ratio (bandwidth is dedicated). Lakini mara nyingi ISP huwa wana-oversale, waroho wengine wanaweza fika hata 50:1 (watu 50 wanashare 1 unit of bandwidth). With a reasonably healthy contention ratio ya 10:1, prices zako zanaweza kushuka to a 10th. Kwa mfano 256Kbp inaweza ikauzwa kwa $46.
 
Last edited:
Wajameni, hivi ni ISP yupi ameshajiconnect kwenye hii fiber ili tumkimbilie tuanze kudauniload vitu!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…