Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
juzi nilimpatia dengu na choroko, lakini anaonekana kupendelea zaidi uji wa mtama!
[/CENTER]
...Mwite "Fisadi" maana anaonesha anapenda kujinafasi bila kutoka jasho cheki hata alivyokaa hapo..Sura yake inafanana na Fisadi mmoja al-maarufu sana anaitwa..... Muangalie vizuri utagundua tu.![]()
(Epa - picha ya hivi karibuni)
Napenda kuwapa-update tu kuwa yule mnyama niliyetumiwa kwenye posta bado yu mwenye afya njema. Sikuweza kupata msaada kutoka idara ya wanyamapori, najitahidi kumudu hivyo hivo Ila anakula sana siku hizi. Ameanza kupendelea matopetope na mbegu za maboga kwa sana, kama kuna mtu analima maboga naomba anitaarifu nitafute njia ya kusafirisha.
By the way, tumeshampatia jina. tunamwita Epa, jina bado hajalizoea sana, kama kuna mtu mwenye pendekezo la jina jingine naomba anipatie.
Wkend njema.
![]()
Tafadhali sana, naomba msaada kumpeleka idara ya wanyamapori... bado anapumua, juzi nilimpatia dengu na choroko, lakini anaonekana kupendelea zaidi uji wa mtama!
wkend njema 😀
mmmh hii sio kweli ni story kama za SHY ............. ni udaku tu huu.
![]()
Napenda kuwahabarisha tu kuwa Epa yu mwenye afya. Sema tu wiki chache zilizopita alipatwa na viroboto... tulinunua dip na kumwogesha kwenye beseni. Sasa hivi yuko fiti tu na kwa kweli kawa mtundu sana.
Juzi kuna mbwa wa jirani alikuja maeneo ya karibu na dirisha kwenye mti anaopenda kukaa, acha atuchekeshe. Alimtolea ulimi na kuanza ku-blow rasberries (zile sauti za kumstitua mtu mwenye busha). Mbwa alivyojiondokea... akaacha. 🙂 🙂
Weekend njema!!