Hawa ndio walioomba nafasi za kujiunga na shule yetu na hatuna utaratibu wa kukataa mwanafunzi kwa case ya ukabila wangekuja kina shehoza pia tunge wa enroll. MKUU WA SHULE =sisi kwa sisi secondary school. SLP- KIBOSHO. MOSHI
Tunashukuru kwa ufafanuzi ticha, ila dah hoja hapa nadhani sio kukashif, bali kupima ama kutafuta kiini cha kiwango kikubwa cha matokeo mabovu katika shule zetu za kata,..
Pengine kuna suluhu, nitolee mfano shule niliyosoma mimi,kaloleni sec school na kumaliza mwaka 2001, ilikuwa ni shule ya kata lakini iliyokuwa ya utofauti kwenye matokeo ya kidato cha nne ikiwa ni mara yake ya kwanza kwa wanafunzi kuhitim kidato cha nne.
Tulio hitim tulitoka sehemu mbalimbali za mikoa ya tz akiwemo mtangazaji mmoja wa clouds fm na matokeo yalikuwa ni kama ifuatavyo, div 1=11 div 2=18 div 3,4 & 0 sikumbuki idadi yake japo jumla ya wahitim tulikuwa 67.
Kwa upande wangu nikilunganisha na shule nyingine za kata haya yalikuwa ni matokeo mazuri ambayo yamekuwa na graph inayopanda kila mwaka. Na hivi Leo ni shule ya 12 kimkoa kati ya shule 137.
Kwa hali hii haya ni mafanikio ya kuigwa na shule nyingine za kata. Nigusie kidogo kiini cha haya mafanikio kwa mtizamo wangu ni uongozi mzuri uliofanikiwa kudumisha nidhamu ya wanafunzi na walimu, lakini zaidi ya hapo naona imechangiwa pia na umakini katika uchaguzi wa wanafunzi wanaojiunga, mchanganyo wa wanafunza toka sehemu mbalimbali na mengineyo ambayo pengine wahusika wanajua zaidi.
Kuna haja ya hizi shule kutizamwa kivingine kwani tatizo linaweza lisiwe kwa walimu na vitabu pekee