Muwe na shukrani japo kidogo, Sarpong kawapa point 3 mechi nyingi tu za ligi. Ikiwemo ya Ruvu Shooting ya Masao Bwile.
Mchezaji hawezi kuwa fiti mechi zote.
Kumsema vibaya ni kumvunja moyo.
Kama kukosa goli mechi ya jana kumbukeni hakuna mshambuliaji wa Yanga aliyeifunga Simba katika ligi ya mwaka huu kwa goli la move.
Sapong aliifunga Simba mechi ya kwanza ya ligi kwa mkwaju wa penati ya Kisinda.
Jana tena Yanga imeshinda kwa penati.
Sasa mbona hao washambuliaji wengine wameshindwa kuifunga Simba magoli ya move pia.
Sapong ni mshambuliaji anayejituma sana na anaweza kuwa mkali zaidi kama atapata walishaji wazuri.
Kumbukeni Simba ndio timu iliyoruhusu magoli machache ya kufungwa hadi sasa kutokana na ubora wa beki zao.
Kazi ya Onyango inaonekana wazi kabisa.
Hebu mheshimuni Sapong