Ebu tutoe ushauri kwa huyu jamaa ambaye mke wake ni mjamzito!

Ebu tutoe ushauri kwa huyu jamaa ambaye mke wake ni mjamzito!

Fimbo ya Musa

Member
Joined
Jul 21, 2012
Posts
94
Reaction score
13
Kuna jamaa mmoja alikuwa akitusimulia yanayomsibu katika ndoa yake, ati mkewe ni mja mzito kwa mara ya kwanza na wanaishi wawili katika nyumba ya kupanga. Jamaa anahuzunishwa na tabia ya mkewe kwan mkewe anadai hawezi kazi yoyote ila rafiki zake wakija anawachangamkia! Halafu anawambia haumwi! Ila mmewe anamwambia ati anaumwa! Bac jamb anaomba ushauri kwenu wana JF Kwani kazi zimemzidi na hana uwezo wa kumuajiri house girl. Nawasilisha...
 
Mkuu hapo hakuna ushauri toka kwa regular people kama sisi labda wataalamu wa kisaikolojia. Kwa sababu jamaa anataka mtoto na mtoto hapatikani kirahisi basi afanye tu hayo majukumu kwa miezi hiyo tisa
 
Ameshakuona wewe bonge la Bushoke, Inabidi ukomae mdogo wangu, vinginevyo utaosha sana sufuria.
 
Analo..mpaka baada ya miezi 9!! Tena afadhali huyo kuna mwingine alikuwa akiingia ndani mke anamwambia ananuka!
 
huyo mwanamke ni mzembe na mnafiki na siku akipata tatizo la kweli ndiyo ataisoma namba
 
mwambie rafiki yako akue kama mwanaume na atake responsibility, anajua kadhia ya mimba?????

Hivi anataka mkewe aeleze shida zake zooooooooote kwa marafiki zake???

Mkewe anajua kuwa mambo ya ndani ya ndoa yanawahusu wao wawili...... Ndo maana anaficha maumivu yake na kujichangamsha......... Sasa mwambie 'rafikio' nae awe mtu mzima aweke tabasamu usoni....akaugulie kwa mkewe mara baada ya marafiki kuondoka....

Kuhusu kazi, kazi huwa haziishi.... Kama alivyopata muda wa kumdunga mkewe mimba, a-adjust muda wake akamsaidia mkewe kazi........
 
Kuna jamaa mmoja alikuwa akitusimulia yanayomsibu katika ndoa yake, ati mkewe ni mja mzito kwa mara ya kwanza na wanaishi wawili katika nyumba ya kupanga. Jamaa anahuzunishwa na tabia ya mkewe kwan mkewe anadai hawezi kazi yoyote ila rafiki zake wakija anawachangamkia! Halafu anawambia haumwi! Ila mmewe anamwambia ati anaumwa! Bac jamb anaomba ushauri kwenu wana JF Kwani kazi zimemzidi na hana uwezo wa kumuajiri house girl. Nawasilisha...

asiajiri house girl kwanza, amwache (ampe talaka) mke wake, akimwacha manake hatakuwa nae hapo nyumbani, so rafiki zake wakija "atawachangamkia" yeye mwenyewe, na wakati huo hata kuwa na mawazo kuwa mkewe hasaidiii kwani alisha achana nae. naamini wakati huo atapata kujua kama ni bora kuwa na mke anaechangamikia marafiki ila akiwa nae pekee anasema anaumwa , au kukosa kabisa mke. akisha jua tofauti ya mawili haya , hata weka visingizio kwenye mimba ya mkewe
 
hata na mimi ningedeka.maybe huyo mke anaona chance ndio hiyo hiyo,wanawake wengi wanafanya hivyo.ila mengine huzidiana tu
 
Back
Top Bottom