ECCAS yataka kuwepo mazungumzo ya makundi yote nchini Chad

ECCAS yataka kuwepo mazungumzo ya makundi yote nchini Chad

jollyman91

Member
Joined
Sep 21, 2021
Posts
69
Reaction score
29
Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Katikati mwa Afrika (ECCAS) imetoa wito wa kuitishwa amazungumzo yatakayoshirikisha makundi yote nchini Chad.

Rais Denis Sassou Nguesso wa Jamhuri ya Kongo ambaye ni Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Katikati mwa Afrika (ECCAS) amezitolea wito pande za kisiasa nchini Chad kushiriki katika mazungumzo shirikishi ya baadaye nchini humo. Denis Sassou Nguesso amekariri uungaji mkono wa jumuiya hiyo kwa kipindi cha mpito huko Chad.

Vilevile amempongeza Mahamat Idriss Derby kwa hatua zilizopigwa na serikali ya mpito ya Chad kwa ajili ya kuanzisha mazungumzo shirikishi na ya amani. Pongezi hizo za Rais Nguesso zimesomwa kwa niaba na Denis Christel Sassou Nguesso Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Kongo.

Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Katikati mwa Afrika pia imekaribisha nia ya serikali ya mpito ya Chad ya kukubali kuyashirikisha makundi mbalimbali yanayobeba silaha katika mchakato wa maridhiano ya kitaifa.

Mkuu wa serikali ya Chad Mahamat Idriss Deby Itno Ijumaa iliyopita alitangaza majina ya wawakilishi 93 wa bunge jipya la mpito la nchi hiyo, miezi mitano baada ya kujitangaza kuwa kiongozi wa nchi kufuatia kifo cha baba yake, Idriss Deby Itno.

4bmy9f6aba91b8scrc_800C450.jpg
Mwendazake, Rais wa zamani wa Chad, Idriss Deby

Baada ya mauaji ya aliyekuwa rais wa Chad, Idriss Deby, jeshi la nchi hiyo lilitangaza kuwa limeunda baraza la mpito litakaloiongoza nchi katika kipindi cha mpito cha miezi 18 na kuanzisha taasisi za kidemokrasi ikiwa ni pamoja na kusimamia uchaguzi huru baada ha kipindi hicho.

Deby aliuawa akiwa katika maeneo ya vita baina ya jeshi la taifa na makundi ya waasi baada ya kuiongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 30.
 
Huyu sassou Nguesso mwenyewe aliingia kwa wizi mkubwa wa kura, nguvu ya kuitisha mazungumzo sijui anatoa wapi.
 
Back
Top Bottom