Economic Hitmen

Economic Hitmen

Mu-sir

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Posts
3,621
Reaction score
1,636
Ni kitabu kinaitwa CONFESSION OF AN ECONOMIC HITMAN.

Iko hivi:

Kabla nchi zetu maskini kukopeshwa zinafanyiwa study ya nguvu na wataalam wa uchumi kutoka IMF, WORLD BANK and the so wakopeshaji wakubwa. Lengo lao hasa ni kujua unexplored resources zilizopo.

1. Sasa hayo mataifa makubwa yanatoa the so called MIKOPO au MISAADA ya ujenzi ai Ufadhili wa Mradi fulani lakini sharti kubwa ni kuwa main contractor anatoka kwao. Lets say anayoa pesa ni IMF au world bank so most likely contractor atakuwa kampuni ya kimarekani.(Yaani pesa inakuwa transfered huko huko) Anakuja contractor anapiga kazi analipwa huko huko kwao ila nyie mnabeba deni tu. Yaani mnaishia kuona barabara au daraja au umeme au chochote lakini pesa hampewi na deni linakuwa la taifa. (Hapa local contractors hawapati hizi tender kubwa)

2. sasa wakisha wakopesha sana then the next move ni kuomba Access kwenye natural resource mlizonazo kama nchi. Kwa sababu mnadaiwa na hawa jamaa inawawia vigumu kuwanyima fursa hiyo adimu na adhim. (Mfano hai upo hapa kwetu..wakopeshaji wetu wapo kwenye madini na gesi yetu. Hata wachina nao wametumia same technic na wapo)


3. mkiwakatalia Access ya natural resource zenu kisa deni wanalilowakopesha next move ni ku create propaganda. Kumbuka hata hapa Tanzania ile issue ya mikataba ya madini ya URANI mkuju river project kupewa kampuni za urusi (NMZ) kulianza kuzuka propaganda eti inatumiwa na Magaidi. Sijui wakubwa wetu walili solve vipi. Niliishia kusikia kampuni husika iliuza hisa zake ulaya.

4.Next move ni kutumia "The Jackals" ku create movement within a country ya kuleta "ukombozi" kwa wananchi...hii hujumuisha kuzuka ghafla kwa kikundi cha waasi wenye silaha kali wanaopigana na serikali ili kuitoa madarakani....hupewa support ya fedha na silaha na hao hao jamaa. Hapa ghafla huzuka vita ya wenyewe kwa wenyewe...Refer Syria, Libya, Congo etc. kwa mifano hai.


5.Hiyo hapo juu ikishindikana ndiyo propaganda inazidishwa na kuonesha nchi fulani inahatarisha "Amani" ya dunia hivyo kuleta ulazima wa kushambuliwa na mataifa makubwa ili kuondoa utawala Hatari kwao. Hapo utaona majeshi yao yakika kupigana na nchi husika kwa kisingizio hicho na Finally wanashinda. Refer Laurent Gbagbo wa Ivory coast (pamoja na kuwa alishinda uchaguzi kihalali), Saddam Hussein, etc.

NB:
nimejitahid kueleza kwa kifupi kitabu hicho. Wengine wataongezea.
 
Back
Top Bottom