Tetesi: Ed Sheeran Atangaza Kupumzika Muziki

Tetesi: Ed Sheeran Atangaza Kupumzika Muziki

Joined
Aug 23, 2019
Posts
22
Reaction score
19
Image result for ed sheeran


MWANAMUZIKI maarufu duniani, Mwingereza, Edward Christopher Sheeran, maarufu kama Ed Sheeran ametangaza kuwa atapumzika kazi hiyo baada ya kuifanya kwa muda mrefu.

Ametoa kauli hiyo alipokuwa anafanya hitimisho la ziara yake ya ‘Divide World Tour’ mjini Ipswich, Uingereza, baada ya miaka miwili ya kuzunguka na ziara yake hiyo yenye mafanikio zaidi kwa muda wote .

image-1.jpg


“Nimependa uwepo wenu hapa na tumemaliza ziara yetu mjini Ipswich. Hili ni tamasha langu la mwisho kwa takribani miezi 18,” alisema.

Hii ni baada ya watu zaidi ya milioni tisa kuhudhuria kwenye tamasha lake la ‘Divide World Tour’ lililoanza mwezi Machi mwaka 2017 ambapo ndani ya siku 893 amezunguka mataifa 46 kwenye miji 175 na kufanya shoo 260, akiwa na crew ya watu 268 na kutembea kilometa 311,029 zilizomwingizia kiasi cha Sh. trilioni 1.9 za Tanzania.

 
Huyu jamaa kuna ngoma yake latest kaitoa nimeshangaa kuona ana rap
 
Hili goma lake na Bieber liko poa sana
 
Back
Top Bottom