Ed Sheeran kacopy wimbo, adaiwa Bilioni 225

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564

STAA wa R&B, Ed Sheeran yamemkuta! Unaweza sema hivyo kwa maana nyingine baada ya familia ya aliyekuwa mkali wa muziki huo, marehemu Marvin Gaye kutaka ilipwe dola milioni 100 (zaidi ya bilioni 225 za Kibongo) kwa kosa la kuibiwa wimbo.

Kwa mujibu wa Kampuni ya Structured Asset Sales, inamdai Ed kiasi hicho cha pesa kutokana na kuiba Wimbo wa Let’s Get It On na kuubadili baadhi ya vitu kisha kuuita Thinking Out Loud. Ed anadaiwa kukopi midundo, melodi, sauti pamoja na kiitikio cha mbali kutoka katika wimbo huo uliowahi kuimbwa mwaka 1973.

Mtoto wa Marvin Gaye, Ed Townsend Jr kwa kushirikiana na Structured wameshafikia pazuri ambapo wamewalalamikia makampuni ya Sony/ATV Music, Atlantic Records na mwandishi ambaye ni Ed.Hata hivyo, bado Ed hajatoa ufafanuzi wowote juu ya madai hayo ya kuiba wimbo.

Wimbo wa Thinking Out Loud wa Ed uliachiwa Novemba, 2014 na kuwa namba moja katika chati kubwa duniani za Billboard.
 
Walikuwa wapi muda wote hyo, watafte hela sio kutajirikia kosa LA mtu
 
Mtoa mada tafadhali tuekee nyimbo ya Marvin Gaye na ya Ed sheeran tulinganishe kama hayo Madai yana ukweli wowote
 
Hata haifanani sana[emoji58]
 
Mahakama ndio itajudge huyo aliyeweka hizo hela kwamba alipwe anaweza kulipwa au asilipwe kwahio tusubili..

Lakino tukiwa yunasubiri hebu kasikilize ngoma ya happier ya ed sheeran upate ladha ya mziki adimu kabisa duniani.
 
Hii familia ya marvin gaye sio mara ya kwanaza na kesi za namna walishawahai mshtaki pharrel Williams na wakashinda kesi naona hii ndio imekuwa staili ya kujipatia kipato.
 
Nimeisikiliza hio ngoma mara ya 3 haifanani hata kidogo na think out loud..
Hao jamaa wanataka unaarufu kupitia kwa ed sheeran
 
Walikuwa wapi muda wote hyo, watafte hela sio kutajirikia kosa LA mtu


Mambo haya sio kama kupeleka kesi kwa mjumbe wa kijiji huko kwenu. Unapohusisha kitu kama $100M lazima jopo la wanasheria wapitie kesi kabla ya kufikishwa mahakamani. Halafu unaposema kutajirika kutokana kosa la mtu sikuelewi.
 
Hii familia ya mavin gaye iache njaa.. walishawahi fungua madai dhidi ya farell williams kutokana na wimbo wa happy sijui yaliishia wapi..naona wamekuja na jipya..!
 
Kakopi wimbo ama kacopy melody??
Tuanzie APA kwanza
 
Hao jamaa nyimbo zao zote nazikubali,ila kiukweli hazifanani kabisa.
 
Hii familia ya mavin gaye iache njaa.. walishawahi fungua madai dhidi ya farell williams kutokana na wimbo wa happy sijui yaliishia wapi..naona wamekuja na jipya..!


Sio njaa. Haki ya mtu aiendi bure tu. Kesi ya Darrel walipiga pesa nyingi, na hii kuna dalili zote ya kupata haki zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…