Eddie Hall: Mnyanyua vitu vizito anayelazimika kula mara 10 ya mtu wa kawaida

Zurie

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2014
Posts
2,012
Reaction score
5,571


Edward 'Eddie' Hall(30) ni mshindi wa shindano la World's Strongest Man kwa mwaka 2017. Mbali na kupata ushindi katika mashindano hayo, aliweka rekodi ya dunia kwa kuweza kunyanyua Kilogramu 500(Nusu tani) na kuvunja rekodi aliyoiweka yeye mwenyewe mapema siku hiyo ya kunyanyua Kilogramu 465.

Eddie anaelezea tukio hilo kuwa ni la kipekee katika historia ya binadamu na moja ya vitu vya hatari zaidi alivyowahi kufanya. Kunyanyua uzito huo kulipeleka apoteze fahamu.

Eddie anaeleza kuwa kuwa na uwezo alionao kunahitaji kujitoa kwa hali ya juu kwani ni kazi ya muda wote na si tu wakati wa mashindano.

Utaratibu wake wa mazoezi wa kila siku unahusisha saa 1 na nusu ya mazoezi ya misuli, saa 1 na nusu ya mazoezi ya joto na baridi(hot/cold treatment), saa 1 na nusu ya kujinyoosha, saa 3 hadi 4 za kunyanyua vitu vizito na saa 1 ya mazoezi ya kuimarisha moyo(cardio).

Eddie pia analazimika kula takribani kalori 12,500 kwa siku anapokaribia kushiriki shindano, kiasi ambacho ni mara 10 ya kinachopendekezwa kwa mtu mmoja kwa siku. Ili kufanikisha hili inambidi kula kila baada ya saa 2, hata nyakati za usiku.

Ratiba yake ya mlo huwa hivi;
3am: Raw steaks and protein shakes
7am: Full English breakfast
10am: Second breakfast – fruit, beef jerky
Midday snacks: 150 g cashew nuts, litres of cranberry juice, milk, protein shakes
Lunch: Steak and chips, salmon and pasta or chicken and pasta/rice
Dessert: Half a family cheesecake
Second lunch 3pm: Tuna sandwiches, flapjacks, five or six portions of fruit, Lucozade, cranberry juice
During training: Cranberry juice, litre protein shakes with full fat milk, coconut water
Dinner: Curry, spaghetti bolognese or steak and chips
Dessert: The other half of the cheesecake
Snacks: Protein bar, beef jerky
In bed: Protein bars, beef jerky, raw steak



Hivi sasa Eddie ameshafikia malengo yake ka kuingia kwenye kitabu cha Guiness na kushinda World's Strongest Man hivyo anapanga kuacha mashindano ya unyanyuaji vitu vizito kwa kuhofia afya yake.

Uzito wake ni mkubwa sana unaomfanya ashindwe kutosha kwenye magari na kupata ugumu wa kutoka kitandani.

Anafikiria kuhamia kwenye tasnia ya filamu.
 
huto tu vyakula twepeeeesi hata mimi naweza kutumaliza sema tu labda kwakuwa tunafuatana baada ya muda mfupi
Mwenyewe nimeshangaa. Huto tuvyakula ni twa kuchangamshia kinywa wakati msosi og unasubiriwa[emoji4] [emoji4] . Wazungu bana! Wanaleta utani na kula[emoji124] [emoji124] [emoji124]
huto tu vyakula twepeeeesi hata mimi naweza kutumaliza sema tu labda kwakuwa tunafuatana baada ya muda mfupi
 
Sisi twendelee kula dona mpaka mishipa inasimama ***** πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Huyu kugegeda hawezi,tena ukifanya mazoez ya hv unakuwa na kibamia
 
Dah mpeni nguna ya donna mara tatu tu kwa siku akilumangia na ngisi mbona atanyanyua hata tani moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…