EDF na insurance- matumizi ya EDF kwa insurance brokers

crabat

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2012
Posts
4,323
Reaction score
2,207
EDF NA INSURANCE
MATUMIZI YA EDF KWA INSURANCE BROKERS
Mamlaka ya mapato Tanzania imeanzisha matumizi ya machine za ki electroniki za kutolea risiti kwa manunuzi yoyote yanayofanywa. Awali walianza na wale wote walisajiliwa kama walipaji VAT. Wafanya biashara hawa wengi hawakupinga utmiaji wa mashine hizi kwani lengo lake kwao ni ulipaji wa VAT kama mauzo yanavo fanyika.
Ikaja awamu ya kundi la pili nalo ni la wafanyabishara ambao si walipaji VAT lakini turnover yao ni zaidi ya Shilling 14m/ kwa mwaka.
Hili kundi la pili kumekuwa na upinzani mkubwa kutoka kwa wafanya biashara,
Kumefanyika maandamano na migomo kama kule mwanza , kariakoo na iringa.
Wafanya biashara hawa wametoa wasi wasi wao kuwa TRA haikufanya utafiti wa kutosha juu ya vipi watatumia mauzo ya kila siku ya wafanya biashara hawa katika kupata makisio ya kodi ya kulipa.inavo onekana yale mauzo ya wafanya biashara ndio kigezo kinachotumiwa na TRA kujua provisional TAX ya kulipa. Bila ya kuzingatia mambo ya msingi katika biashara kama
bei ya kununulia mali,
faida au hasara
gharama za uendeshaji n.k
TRA wamekua wabishi na wanajifanya kama hawasikii hiki wa kile wao maadam kimeamuliwa basi ni lazima kifanyike na kwa kutumia vitishio . Baya zaidi ni kwa TRA kutokua na uwezo wa kitaalam kujibu malalamiko ya wafanya biashara. Inaonekana kama vile TRA haina wasomi ambao wanaweza kujibu hoja za wafanya biashara…wao wanatumia zaidi nguvu kuliko busara na elimu ya taxation. Naamini kama TRA watawaeleza wafanya biashara njia gani zitatumika katika kukadiria kodi kutokana na data za wafanya biashara basi kusingekua na migomo na maandamano. Lakini hawako wa wazi na kama wanafanya kazi kwa hadaa …yote haya yanafanywa ili mfanya biashara asijue kodi yake ni ngapi ili kuweka mwanya ya kuja kutoa rushwa.
Sasa tuje kwenye suala la EDF na insurance brokers.
Tra wamewataka mawakala wa bima yaani brokers watumie machine hizi. Na Brokers kupitia chama chao wamewaandikia TRA kutaka kujadiliana ili kupata njia muwafaka ya kutumia machine hizi ili hesabu sahihi zipatikane.
Kisheria risiti za bima zinatakiwa ziwe na maelezo maalum yahusuyo bima na mkata bima na kampuni ya bima. Sote tunajua bima ni mkataba ambao unahusisha watu wawili na ulipaju wa consideration ambayo tunaita premium. Hivyo risiti ni sehemu muhimu ya mkataba na ina affect madai ya mwenye bima. Risiti za bima zinatakiwa ziwe na
Jina la Insurer
Cover note na tarehe yake ya kutolewa
Aina ya bima
Namba ya gari kama ni bima ya gari
Jina la mwenye bima.
Sasa hizi risiti za EFD hazina uwezo wa kutoa data hizi hivyo zenyewe zinaenda kinyume na sheria ya bima kuhusu risiti.
Pili mawakala wa bima wao wanapokea malipo ya bima kwa niaba ya makampuni ya bima hivyo sio sahihi wao kutoa risiti kwa jina lao kwa full amount wanayo pokea….kwani hapa data zitazokwenda TRA ni kuwa wakala ameingiza amount kama inavonesha kwenye risiti hivyo bila ya shaka wataitumia hiyo kuamua turnover ya wakala na ulipaji wa provisional Tax..!!!
Hii si sahihi mawakala wao wanapata only commision kutokana na malipo ya bima kutoka kwa wateja wao.
Jambo la pili ni kuwa mawakala wanatakiwa kupeleka malipo kila baada ya siku 15 kwa kampuni za bima yaani principals…na huwa wanapeleka malipo kasoro ile commission yao..hapa napo kampuni ile inatakiwa kutoa risiti hii ya EFD …Sasa utaona namna gani dublication ya data na kuharibu kabisa mapato kamili ya biashara ya bima !
Brokers watakua wame ripoti full amount wanayopokea na Insurers wao wanaripoti full amount less commision. Hivyo TRA watakua hawajui kabisa turnover halisi ya biashara ya bima kwa kutumia mfumo huu ambao wanaulazimisha,
Chama cha mawakala kiliwaandikia TRA lakini cha kustaajabisha hata kuijibu barua yetu wameshindwa kabisa..hawakujiabu…na bado wanaendelea na msimamo wao wa kulazimisha kutumia mashine hizi ..
Hili linastaajabisha sana kwani tumeandika ili kupatia ufumbuzi mambo hayo na mengine ili TRA wapate njia nzuri ya kupata kodi zao lakini wao inaonekana wanakimbia majadiliano yoyote hata kama ya msingi. Sasa sijui ni kwa sababu hawana uwezo wa kielimu kujadili mambo kisomi na wanapenda kutumia zaidi nguvu! Hili hakika wao watalijibu…

Kitu kingine kwa nini biashara ya bima haistahili ni kwamba bima sio VAT regisered business na hii sheria ni sheria iliyopo kwenye VAT Taxable business.
Na pia Bima na premium are not taxable consideration in Tanzania hivyo kuilazimisha ni sawa na kuwalazimisha Banki kutoa risiti ya EFD unapoweka pesa zako.
Tunawaomba TRA wawe wakweli wajibu barua za wadau na pia wajibu hoja za wafanya biashara kwa ustadi na sio kwa nguvu.
Kama watashikilia brokers watumie utaratibu huu basi wajue watasababisha kodi za uongo na zisizo na mshiko..na kesi katika mabaraza ya kodi yatakua nyingi sana..tushirikiane kujenga nchi yetu.


:embarassed2::embarassed2:
 
Hili swala lina mgogoro hata kwenye Insurance Company zenyewe na mwisho nasikia kuna uwezekano wa kuangalia namna ya kuwa na machine aina tofauti itayokidhi mahitaji ya financial institution kama Bima.

EFD zililenga VAT registered na baadae wakaamua kuleta za unregistered ili kuweza kufatilia mauzo na hii ingewasaidia kujua nani amefikia level ya mauzo yanayohitaji kuwa VAT registered ili walipe kodi lakini wakaamua lengo liwe zaidi ya hilo ili waweze kupata revenue records ya kila kampuni yenye vigezo fulani walivyoweka.

TRA wanajaribu kutafuta namna ya kuweza kupata reliable records kwa kila mlipa kodi ambacho ni kitu kizuri lakini wanahitaji kufanya utafiti wa kutosha kabla ya kulazimisha mambo yaliyofanyiwa utafiti finyu.Wanapaswa kutafiti kila sector na changamoto zake ili waweze kuweka utaratibu tofauti utakaowapa reliable records.

Kampuni za Bima zinapokusanya premium zile ni collection ambazo mwisho wa siku inakuwa income baada ya ile risk period kupita na pia ile collection si yote inachukuliwa na kampuni husika ya Bima maana Reinsurer anachukua percentage yake, lakini pia Kampuni za Bima zenyewe zinagawana risk na kupelekea kugawana hiyo premium iliyokusanywa hivyo kuna changamoto za kufanyia utafiti kabla ya kuibua tu machine na kulazimisha watu kuzitumia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…