KISASI cha miaka ishirini iliyopita kimelipwa Ijumaa usiku katika Uwanja wa Mohamed V, pale Casablanca.
Kisasi cha watu wa Afrika Kaskazini dhidi ya Simba. Maumivu yalikuwa makubwa wakati Simba walipoitoa Zamalek kwa penalti katika uwanja wa Taifa wa Misri miaka ishirini iliyopita pale Cairo.
Halikuwa pambano la robo fainali lakini mazingira mengi yamefanana. Lilikuwa pambano la mtoano kama hili na Simba walikwenda katika hatua ya matuta wakaibuka mashujaa. Wengi tunaikumbuka penalti ya mwisho ya Mchaga Christopher Alex Massawe.
Juzi lilikuwa pambano la robo fainali. Pambano muhimu kuliko lile. Mwaka 2003 Simba walishinda 1-0 pale Temeke na katika pambano la marudiano wakachapwa 1-0 pale Cairo. Mechi ikaenda katika dakika 30 halafu tukaenda katika matuta. Hakuna mchezaji wa Simba aliyekosa penalti kama ambavyo hakuna mchezaji wa Wydad Casablanca aliyekosa penalti juzi usiku.
Hatimaye Shomari Kapombe na Clatous Chotta Chama wakakosa penalti zao juzi. Waarabu wakashangilia. Kisasi pekee ambacho Simba walilipa katika pambano la juzi ni hawakunyanyaswa na Waarabu kama ambavyo walinyanyaswa na Zamalek pale Cairo katika usiku ule wa machozi, jasho na damu.
Haikutazamiwa Simba wangecheza katika kiwango walichocheza. Mara nyingi Waarabu wanaficha makucha yao ugenini na kuyakunjua nyumbani. Ukiangalia mwenendo wao ndivyo ilivyo. Wanapigwa moja au mbili wakiwa ugenini kisha wanashinda sita wakiwa nyumbani. Wengi tulitazamia Simba wangekuwa katika bonde la mauti pale Casablanca. Haikuwa hivyo.
Walitulia wakawamudu Wydad. Walitulia na kupasiana pindi walipokuwa na mpira mguuni. Ni tofauti na miaka ishirini iliyopita, walishindwa kupiga hata pasi sita katika ardhi ya Kaskazini.
Juzi waliwapa mechi Wydad kiasi, ulikuwa ukitazama sura za mashabiki wa Wydad unaona hofu katika mioyo yao. Tatizo kubwa la Simba lilikuwa katika eneo la mwisho. Hawakuwa na mipango. Hawakuonyesha ubora. Labda ndiyo ilikuwa tofauti kubwa ya uwezo na uwekezaji katika vikosi viwili.
Kama tunataka kwenda fainali tunahitaji kuwa bora katika kila eneo la uwanja pindi tunapokuwa nyumbani na kisha ugenini. Pambano la Temeke Simba walipoteza nafasi. Walifika katika lango la wapinzani wao mara kadhaa. Pambano hili la Casablanca walikuwa hawafiki. Wakienda katika takwimu watagundua walikuwa na takwimu mbovu katika eneo la mwisho la uwanja. Kwa wakubwa wenzao wanaoshiriki michuano hii kucheza ugenini huwa haiwi sababu ya kutoshambulia ugenini.
Tatizo jingine la Simba likawa kipa Ally Salim. Subiri kwanza. Ni shujaa wa Simba katika mechi zote ambazo amecheza tangu Aishi Manula aanze kutazama mechi za Simba akiwa sebuleni hivi karibuni. Hata hivyo, Ijumaa usiku alipaswa kuwa bora katika mpira wa kichwa wa mshambuliaji Msenegali wa Wydad, Junior Sambou.
Hauwezi kuruhusu bao rahisi kama lile katika hatua hizi.
Kama Aishi angekuwepo naye angeweza kufungwa kama kipa mwingine yeyote yule lakini siyo kwa namna ile. Lilikuwa bao rahisi. Angeweza kuwa bora zaidi. Ana ushujaa, anajiamini lakini mikono yake inakosa ubora.
Halafu akaenda kukosa ubora katika mikwaju ya penalti. Sawa unaweza kumfunga Manuel Neuer mikwaju mitano ya penalti lakini atakuonyesha ubora wake wa kukaribia kupangua mikwaju kadhaa. Labda mipira itakuwa na nguvu zaidi lakini ataiona. Ally hakukaribia kudaka penalti. Waarabu walikuwa wanamtupa mbali kadri walivyojisikia.Aishi asingetupwa vile. Angefanya jambo. Labda angeweza kufidia penalti ambazo Shomari na Chama walikosa.
Hata hivyo, hauwezi kumlaumu sana Ally. Katika mechi za viwango kama hizi ameonyesha ushujaa mkubwa. Anaweza asiwe kipa mzuri sana lakini ana ushujaa moyoni. Ukimtazama hana hata wasiwasi. Ilikuwa hivyo hivyo, katika mechi alizokaa katika lango la Simba tangu Aishi atoweke.
Baada ya kutolewa unatazama nyuma na kugundua Simba na Yanga hazipo mbali sana kufikia nchi ya ahadi kama wakubwa watakuwa wanazichukulia poa. Wydad hawakucheza kama mabingwa watetezi na wangeweza kutolewa na Simba. Kufikia hatua ya mikwaju ukiwa nyumbani ni hatari kubwa na lolote lingeweza kutokea.
Simba wasikate tamaa. Kitu muhimu ni kwamba wameanza kuigeuza hatua ya robo fainali kuwa mazoea.
Hauwezi kuwaza nusu fainali au fainali kama hauifanyi hatua ya robo fainali kuwa mazoea. Ukifanikiwa kuigeuza hatua ya robo fainali kuwa mazoea unaweza kuanza kuiwaza nusu fainali.
Ni kichekesho hiki hiki kinaangukia kwa timu yetu ya taifa. Unawazaje kuwaza kombe la dunia kama haujaifanya Afcon kuwa mazoea? Wanachofanya Simba kwa sasa ni kitu sahihi.
Wanaweza kuimarika zaidi msimu ujao na kwenda mbali zaidi kama wakiamua kuwekeza zaidi katika kikosi chao.
Wakati mwingine soka ni mchezo wa kushangaza. Naamini Simba hii sio bora kuliko ile ya kina Louis Miquissone na wale kina Rally Bwalya lakini ndio walikaribia zaidi kwenda nusu fainali kuliko wale. Fikiria wametolewa kwa matuta na wakati ule hawakufikia hatua ya matuta, tena hawakucheza na Mwarabu. Nadhani wanahitajika kuwa bora zaidi na kujiandaa kwa kila vita.
Kitu ambacho sishangai kuwahi kusema ni afadhali Simba ingekutana na Waarabu hawa kuliko Mamelodi. Nadhani Mamelodi ni ndoto inayotisha kwa sasa. Kuna Waarabu walijipendekeza kwao katika hatua robo fainali na wamefungwa 4-1 kwao halafu juzi wamebabuliwa 2-1 pale Pretoria. Sikutaka jambo hili liwakute Simba.
Mpaka wakati ujao lakini kwa sasa Simba wanaweza kutembea vifua mbele. Inabidi wachukue wachezaji wa maana. Kuna madirisha hapa katikati wamekosea na ndio maana first eleven yao unaweza kuikariri tofauti na ya mtani wao pale Jangwani.
Wanapaswa kurudi imara kwa kuchukua wachezaji wa maana ambao wataanza kubadilishana nafasi na kina Chama uwanjani. Kutoka hatua ya robo fainali kwenda fainali kuna daraja la matumizi ya pesa ambayo klabu inabidi ivuke. Ni nadra sana timu ya kawaida kufika nusu fainali.
Unaweza kupambana na kupata bahati katika hatua ya makundi hadi robo lakini nusu fainali unakutana na wanaume waliowekeza. Haishangazi kuona mabingwa wa Afrika mara nyingi wanakuwa wale wale tu. Hauwezi kukuta timu kutoka Chad, Tanzania, Benin inaibuka na kuwa bingwa mbele ya kina Al Ahly.
MWANASPOTI