Edo Kumwembe: Mayele ana majivuno

Edo Kumwembe: Mayele ana majivuno

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
22,719
Reaction score
40,739
Tatizo la Mayele ni majivuno fulani ambayo anayo. Anafahamu kauli yake itazua taharuki nchini kwa sababu bado ni maarufu hapa nchini.

Angeweza kukaa kimya tu na kufanya mipango yake kuliko kujali sana masuala ya mitandao ya kijamii. Haimsaidii.

Wachezaji wa kulipwa kazi yao ni kucheza soka na kupuuza kelele za mashabiki. Mashabiki kazi yao kubwa pia ni kukutoa mchezoni.

Kukabiliana na changamoto za wachezaji wa timu pinzani, pia mashabiki wa timu pinzani pamoja na wale mashabiki wako ni kazi ya mwanasoka wa kulipwa.

Kuelekea pambano la Pyramids na Mamelodi pale Afrika Kusini, Mayele alikuwa amenyimwa viza ya kuingia Afrika Kusini. Akaenda katika mtandao wake na kuandika kwamba huo ulikuwa mpango tu wa Mamelodi kuhakikisha hachezi pambano hilo.

Kocha wa Mamelodi, Rhulani Mokwena akamjibu Mayele aachane na mambo ya mitandao.” - [emoji2788]Edo Kumwembe.
 
Angalau Makala ya Edo isaidie kupunguza upepo mchafu
 
Hizi tuhuma angezitoa mchezaji wa ndani ningeweza kumuelewa kwamba ni mswahili mwenzetu asiye na upeo.
Ila kwa mchezaji wa kulipwa inashangaza na kiukweli Mayele kazingua na heshima yake imeshuka.
 
Katika watu mapoyoyo basi ni huyo chapombe hana akili na simsikilizagi,kiufupi muache kurushiana majini pumbav zenu
 
Hizi tuhuma angezitoa mchezaji wa ndani ningeweza kumuelewa kwamba ni mswahili mwenzetu asiye na upeo.
Ila kwa mchezaji wa kulipwa inashangaza na kiukweli Mayele kazingua na heshima yake imeshuka.
Kwanini mumtupie majini mkongomani wa watu?
 
alichofanya mayele sijakipenda yaani sio kuidharirisha yanga tu ni taifa zima tunaonekana sisi wachawi yaani katuacha uchi.
 
Hizi tuhuma angezitoa mchezaji wa ndani ningeweza kumuelewa kwamba ni mswahili mwenzetu asiye na upeo.
Ila kwa mchezaji wa kulipwa inashangaza na kiukweli Mayele kazingua na heshima yake imeshuka.
Kiukweli hata mimi nimemshusha sana. Maana huwezi kuwa mchezaji wa kulipwa, halafu muda wote uko kwenye mitandao kujibizana na watu.
 
Back
Top Bottom