Edo Kumwembe: Mayele ana majivuno

Kiukweli hata mimi nimemshusha sana. Maana huwezi kuwa mchezaji wa kulipwa, halafu muda wote uko kwenye mitandao kujibizana na watu.
Halafu anajibizana nini? Mambo ya kipumbavu kabisa. Professional player unaongelea mambo ya majini? Tena unalalamika kurogwa?
 
Anatamani mno zile shobo zingeendelea hadi kule aliko ila kashangaa wabongo wamemsahau mapema sana
Nakumbuka kwenye afcon baada ya kuisha mechi ya Tanzania na Congo akaandikA kwenye page yake Instagram kuwa mbali ya kuchezesha mabeki wanne ila hawakufuzu na wabongo bila kujali timu zao walimuogesha matusi mno
 
Mayele yupo Egypt lakini ki uhalisia Bado yupo Tanzania, Mayele mafanikio na Heshima kubwa katika soka la ndani na nje ya Nchi ameyapata Tanzania.

Kule Drc Mayele alikua maarufu lakini Kwa level yake pale Drc wapo wengi na wamepita wengi katika ligi ya Drc kwaiyo alikua wakawaida Sana.

Mayele amejenga jina akiwa Tanzania uku akimfunika mkongo man Mwenzake Makambo ,Mayele alijituma Sana yeye na wenzake wakafanya mambo makubwa Yanga yeye akiwa kinara.

Kwa ujumla Yanga ya kimataifa ili Bebwa na Mayele na umaarufu wake uka (backfire) mpaka timu ya Taifa ya Congo na kwa wakongomani wote.

Bahati mbaya Amekwenda nchi ambayo lugha haziendani, tamaduni mpya na timu ambayo Haina umaarufu ya pyramid.
Kule watu hawaishi kama Bongo, mdawote mko Avic na washikaji/wachezji wenzako, kule mkitoka mazoezini kilamtu ki vyake kama Ulaya, Sasa Mayele anakua mpweke kwakua muda mwingi ata( chill)na familia yake tu.

Kwaiyo anarudi mtandaoni na kupiga stori na watu wake wa karibu ambao wengi ni wa Tanzania, kwakua anaongea na kuelewa kiswahili, ameshindwa kuwa na washikaji wengi kule misri kwakua tamaduni ziko tofauti Bora ya Drc na TZ zina fanana.

Anafuatilia mambo ya Tz na Drc na hasa ya Tz kwakua anafahamu vingi na anafahamiana na wengi.

Muda mwingi akiwa amepumzika anafuatilia au kuwasiliana na watu wa Tz kwasababu ya upweke, mazingira, tamaduni n.k
Mpaka atakapo weza kuwa na washikaji wapya na kuzoea mazingira mapya ya ugeni ndipo atapunguza kufuatilia ya Tz.

Kwaiyo kama mshikajiwake ni Feisal na inasemekana Kuna Kiongozi wa Azam aliongea na Kiongozi wa Yanga siku Azam inacheza na Dodoma jiji na inasemekana uyo Kiongozi wa Yanga Ali mpiga majungu Mayele wakati akiongea na uyo Kiongozi wa Azam.

Kwakua uyo Kiongozi wa Azam friji haligandishi akampa maneno labda Bangala au Feisal ambao Wana ukaribu na Mayele, Mayele bila kufikiri position yake aliyo iacha Yanga na mashabiki wake aka kurupuka kuongea alicho ongea uku akitambua au kutotambua Yanga inahusisha nchi Nzima isipokua kikundi kidogo Cha uhasi kinacho itwa Simba.

Mayele ame (provoc) nchi ya Wananchi
Ame unyea mkono ulio mlea, Kama Wazazi Yanga naomba wamsamehe.

Kwasasa Mayele yupo Sana mitandaoni kwakua Bado hajapata kampani na kuzoea mazingira mapya.
Kwasasa Mayele anachezea timu ambayo ni kama Azam Haina wafuasi wengi ila ni timu Tajiri pale Egypt ukiondoa Ahly, Zamaleki na Future.

Mayele anatakiwa aongeze juhudi na kuwafunga Ahly, Zamaleki na Future timu vigogo ili aweze kupenya ki umaarufu na kujenga ufalme mpya kule Egypt.

Amtafute nahoza wa zamani wa Azam Himid Mao amwelekeze namna ya kuishi Egypt kwakua tayari ana ukaribu na Sure boy ambaye ata muunganisha na Himid.

Pole Mayele pole Yanga, ivyo ni vitu vidogo tu focus kwenye mechi zijazo tu twae ubingwa aya mengine yanapita.
 
Jini katika moja na mbili..
 
Hizi tuhuma angezitoa mchezaji wa ndani ningeweza kumuelewa kwamba ni mswahili mwenzetu asiye na upeo.
Ila kwa mchezaji wa kulipwa inashangaza na kiukweli Mayele kazingua na heshima yake imeshuka.
Wachezaji wote ni wa kulipwa.Au una maana wachezaji wa kigeni?Hamna mchezaji amatuer kwenye ligi kuu wote ajira yao ni kucheza mpira.
Mayele ameomba muache kumtumia majini mkiacha atakuwa hana la kusema.Uswahili mmemfundisha wenyewe. Rudisheni majini kwenye chupa atanyamaza.
 
Hahahahaaahhahahaa hebu ncheke..😂😂😂😂😂😂😂majini yanafurushwa mpk kaka wa watu anaona nyota nyota...
 
Anatamani mno zile shobo zingeendelea hadi kule aliko ila kashangaa wabongo wamemsahau mapema sana
Mshamba sana nafikiri anatatizo kichwani..heshima hutafutwa kwa tabu sana lakin kuivunja ni sekunde tu.
 
Mayele ni mpuuzi tu. Kuna siku nilifuatilia kwenye page ya Pyramids aseeh ndio nikagundua wabongo wanampenda sana jamaa, nimeshangaa jinsi anavyowalipa kwa style hii
 
alichofanya mayele sijakipenda yaani sio kuidharirisha yanga tu ni taifa zima tunaonekana sisi wachawi yaani katuacha uchi.
hivi yanga mkifanyiwa kitu kwanini muhusishe na Taifa zima, Eymael alipowatukana mkakimbilia kusema ametukana taifa zima. Alichosema Mayele yanga mmemutupia majini wala sio watanzania.
 
Binafsi nimemdharau sana mayele..
Jirani na aliekuwa mwanaparokia mwezangu mt petro oysterbay
 
Hizi tuhuma angezitoa mchezaji wa ndani ningeweza kumuelewa kwamba ni mswahili mwenzetu asiye na upeo.
Ila kwa mchezaji wa kulipwa inashangaza na kiukweli Mayele kazingua na heshima yake imeshuka.
We siku zote unadhani wachezaji Wana upeo!?..wachache Sana!!..kule ulaya Kuna mbulula nyingi tu
 
Hizi tuhuma angezitoa mchezaji wa ndani ningeweza kumuelewa kwamba ni mswahili mwenzetu asiye na upeo.
Ila kwa mchezaji wa kulipwa inashangaza na kiukweli Mayele kazingua na heshima yake imeshuka.
Sio kwamba kwakuwa zimetolewa na mchezaji wa nje ambaye ana heshima nje na ndani ya uwanja huenda tuhuma hizo zikawa zina ukweli ndani yake tofauti labda zingetolewa na Mkude au Ajib ambaye wengi tungehisi ni uswahili tu
 
Sio kwamba kwakuwa zimetolewa na mchezaji wa nje ambaye ana heshima nje na ndani ya uwanja huenda tuhuma hizo zikawa zina ukweli ndani yake tofauti labda zingetolewa na Mkude au Ajib ambaye wengi tungehisi ni uswahili tu
Mkuu, kwamba tuhuma za uchawi na majini zina ukweli? Kwamba unaamini katika hayo?
Yeyote anayeamini katika uchawi, hasa mambo technical kama mpira huwa namdharau sana.

Kwa maana hiyo unaamini kushindwa kufanya vizuri kwa Mayele kunatokana na sisi Yanga kumtupia majini?
Nimesikitika sana.
 
Mayele Amejichanganya Kiukweli Wana Dar Young Africans Tulimkubali Sana Ila Alichofanya Atajionea Mwenyewe.


Kila La Kheri Dar Young Africans Kwa Ushindi Mwingine Wa Ligi Kuu NBC 2023/2024
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…