Edo Kumwembe: Tuwatafakari kwa kina Sawadogo na Mudathir

Edo Kumwembe: Tuwatafakari kwa kina Sawadogo na Mudathir

Oldmantz

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2023
Posts
704
Reaction score
1,457
SIMBA walipomsajili kiungo anayeitwa Ismael Sawadogo nilikuwa na uhakika walikuwa wanajua jambo wanalofanya. Hapa katikati kulikuwa na malalamiko mengi kwamba Simba walikuwa hawajafanya vyema katika madirisha ya usajili ya hivi karibuni.

Mwanzoni tu mwa msimu aliyekuwa kocha mpya wa Simba, Zoran Mark ambaye alikwenda na timu Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya alikuwa analalamika kwamba wachezaji wengi wapya walikuwa hawana hadhi au uwezo wa kuichezea Simba.

Hii ilikuwa nafasi nyingine kwao kujirekebisha. Niliamini alikuwa mchezaji mzuri. Sio tu kwa sababu alikuwa anatokea Burkina Faso, lakini tazama timu mbili alizopitia. Alikuwa amepitia klabu ya ENPPI ya Misri pamoja na Difaa El Jadida ya Morocco ambayo staa wetu, Simon Msuva alipita.

Hauwezi kucheza Misri na Morocco kama hauna kitu mguuni. Tatizo ni kwamba baada ya kuondoka Jadida haionekani ni wapi Sawadogo alikwenda. Inaonekana kama vile hakucheza soka tena kwa muda mrefu. Kwanini? Alikuwa ameumia au? Hatujui.

Mchezaji wa kiwango chake aliyetoka Misri kisha Morocco anashindwa walau kucheza katika timu ya Ligi Kuu ya Burkina Faso kwa ajili ya kujiweka fiti na kucheza tena nje ya nchi yake? Hapa wengi hatuna majibu kwanini hakucheza muda mrefu.

Tunachofahamu ni kwamba mchezaji anayekuja katika dirisha la katikati ya msimu anapaswa kuongeza kitu katika timu yake. Anakuja kwa ajili ya kucheza na kutia nguvu katika upungufu ambao umeonekana baada ya msimu kuanza.Jonas Mkude anaonekana hayupo sawa.

Nassor Kapama na Victor Akpan walionekana kutokuwa vizuri kucheza Simba. Hii inawaacha viungo wachache pale Simba. Viungo wanaoaminika wanabakia kuwa Sadio Kanoute na Muzamiru Yassin. Hao ni katika eneo la chini ambalo ni muhimu achilia mbali viungo washambuliaji kina Clatous Chama.

Kwa nilivyomtazama Sawadogo hawezi kuwasaidia Simba msimu huu. Ni mzito na amejikuta katika ligi iliyochangamka kuliko yeye alivyochangamka. Bado sijauona ubora wake katika maeneo yoyote yale. Sio katika kupiga pasi, kukaba wala kuunganisha timu.

Nilipomtazama Mudathir Yahya katika pambano lake la kwanza la Yanga mchuano wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Singida Big Stars nilikumbuka kitu. kwanini Simba hawakumsajili Mudathir? Walifanya makosa mawili au matatu kwa mpigo.

Mudathir ingawa hakuwa na pumzi kubwa kwa sababu na yeye kama ilivyo kwa Sawadogo alikuwa hajacheza soka la ushindani kwa muda mrefu, lakini alionekana kuwa kiungo bora zaidi uwanjani kutokana na ubora wake katika kukaba na kugawa mipira.

Ingawa wote wawili hawakuwa uwanjani kwa muda mrefu, lakini Mudathir ni bora kuliko Sawadogo na angeingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza cha Simba kuliko ilivyo kwa Sawadogo. Labda katika vipindi ambavyo wote walikuwa nje Mudathir alikuwa na mazoezi zaidi. Au labda tuseme kwamba Sawadogo alikuwa na majeraha na alituficha.

Vyovyote ilivyo, Simba kama wangemsajili Mudathir wasingejuta kwa sababu moja kwa moja angeenda kuwa bora kuliko viungo ambao wapo nao kwa sasa. Wakati ule Mudathir na Sure Boy wamepata matatizo pale Azam ilikuwa inaonekana kama vile Mudathir angekwenda Simba na Sure Boy angekwenda Yanga. Wote wangekuwa wamepata viungo wazuri.Matokeo yake wote wamekwenda upande mmoja. Nasikia Simba walipuuza kumsajili Mudathir.

Inadaiwa kwamba kulifan-yika mazungumzo kati ya Simba na mchezaji lakini ni mabosi wa Simba walianza kumpiga chenga mchezaji na kuamini kwamba thamani yake ilikuwa ndogo sokoni.

Mbaya zaidi wakamsahau kwa zaidi ya miezi sita mpaka Yanga walipokuja kumchukua. Kwa Simba kumchukua Sawadogo ina maana kwamba kwanza hawajaimarika, lakini kwa Yanga kumchukua Mudathir inaonekana wameimarika zaidi na kitu kibaya kwa watani wao ni kwamba wameimarika katika eneo ambalo tayari walikuwa imara.

Wakati tukizungumza kuwa katika eneo la kiungo la Simba kuna Kanoute na Mzamiru, tayari eneo la kiungo la Yanga lilikuwa na Khalid Aucho, Aziz Ki, Sure Boy, Yannick Bangala, Fei Toto na Zawadi Mauya. Kwanini uruhusu wamchukue Mudathir?

Katika pambano la Yanga dhidi ya Real Bamako, Yanga walianza na Bangala, Mudathir na Aziz Ki. Juzi nilikuwa nawatazama katika pambano dhidi ya Geita alianza Mudathir tu kati yao. Huo ndio utajiri ambao wamekuwa nao kwa sasa.

Tukiachana na suala la Sawadogo, kuna jambo jingine ambalo limenifikirisha kiasi. Nilikuwa natazama pambano la Dodoma City dhidi ya Polisi Tanzania mara baada ya kumalizika pambano la Yanga na Geita pale Chamazi. Ubora wa wachezaji wetu umepunguza kwa kiasi kikubwa.

Wakati ligi inaendelea na imeshika kasi, ilikuwaje Yanga ikawaza kwenda kumchukua mchezaji ambaye alikuwa nje kwa miezi sita badala ya kutupa jicho lao kwa wachezaji mbalimbali ambao walikuwa wanaendelea kucheza katika ligi yetu?

Hii ina maana wakati Mudathir anafanya biashara zake Zanzibar bado aliendelea kuwa bora kuliko wachezaji wengi wa Ligi Kuu Bara? Kuthibitisha hilo ni kwamba amerudi uwanjani na haonekani kama hakucheza kwa muda mrefu. Au labda kwa sababu anacheza katika timu iliyo na wachezaji bora? Sielewi.

Inavyoonekana hakuna wachezaji wengi wenye ubora nje ya klabu zetu kubwa. Huwa tunazungumza tu kwamba wazawa hawapewi nafasi lakini ukweli ubora wa wachezaji wazawa umepungua tofauti na ilivyokuwa zamani.

Kwa mfano, baadhi ya wachezaji ambao wangeonekana wanafaa kucheza nafasi ile Yanga angekuwa Cleophace Mkandala wa Azam ambaye kabla ya hapo alikuwa Dodoma City na alikuwa anasifika. Lakini leo Mkandala anashindwa kupata nafasi mbele ya kina James Akaminko pale Azam.

Credit: Mwananchi
 
SIMBA walipomsajili kiungo anayeitwa Ismael Sawadogo nilikuwa na uhakika walikuwa wanajua jambo wanalofanya. Hapa katikati kulikuwa na malalamiko mengi kwamba Simba walikuwa hawajafanya vyema katika madirisha ya usajili ya hivi karibuni.
Anajichanganya tu ili kulazimisha point yake.

Sawadogo anakosa tu fitness hasa kwenye pumzi na inawezekana ana majeraha fulani ila ni mchezaji mzuri. Ana uwezo wa kuficha na kutembea na mpira katikati ya wapinzani kwa kujiamini, kitu ambacho midfielders wengi wa Simba na Yanga hata wa kigeni wanashindwa. Kwa kipindi hichi angewafaa zaidi Simba kama angekuwa anaanzia benchi na kuingia kipindi cha pili kuituliza timu pale inapokuwa tayari inaongoza.

Ni kweli hakuna wachezaji wengi wazawa waliojipambanua kwa utofauti wao. Wengi wanacheza mpira unaofanana, wanacheza mpira wa kupokea pasi na kutoa pasi haraka, hawana uwezo wa kumiliki mpira kwa utulivu na kutoa pasi mpenyezo zenye manufaa katika mchezo. Hawana uwezo wa kupress mbele na mpira kwa pasi za haraka lakini zilizo sahihi. Kutoa pasi sahihi lazima wapunguze sana kasi ya kucheza.

Ukitaka kuona mapungufu hayo, wafanyie zoezi lile la duara la kupasiana uone zitapigwa pasi ngapi kabla ya mtafutaji mpira hajaweza kuugusa.
 
Mo anazingua sana mala ajitoe mala Arudi haeleweki.

Hawa wachezaji wake
WA Buku buku hatuwataki Simba.
Kanute.
Banda.
Okrah.
Ottara.
Onyango.
Sawadogo.

Simba Ina wachezaji wa Tano tu.
MANURA, kapombe, Shabalala, Inonga , chama na Saidoo tu.
Wengine woote ni taka taka.
 
Mo anazingua sana mala ajitoe mala Arudi haeleweki.

Hawa wachezaji wake
WA Buku buku hatuwataki Simba.
Kanute.
Banda.
Okrah.
Ottara.
Onyango.
Sawadogo.

Simba Ina wachezaji wa Tano tu.
MANURA, kapombe, Shabalala, Inonga , chama na Saidoo tu.
Wengine woote ni taka taka.
Kama Mo anazingua wewe hujanyimwa kwenda kupeleka mchezaji wako. Unaweza kumsajili ukampeleka na akapokelewa na ikiwa anakiwango kizuri kuliko waliopo wa Mo basi atacheza.

Simba ina kamati ya usajili. Hao ndio wako responsible na aina ya wachezaji waliosajiliwa/wanaosajiliwa. Sio Mo. Mo anachangia tu pale bajeti inapokomea yeye anaongezea kutoka mfukoni kwake kama ihsani tu. Bajeti ya mwaka huu iliyopitishwa kwenye mkutano mkuu wa wanachama MO atatoa zaidi ya bilioni 3. Kiwango kikubwa kuliko pesa zote Simba inayopata kutoka kwenye viingilio msimu mzima.

Kwenye bajeti hiyo 2.4b zitatumika kwenye usajili. Ni chache kuliko pesa anayotop up Mo. Na ukumbuke Mo hapangi bajeti wala haipitishi yeye.

Mo tayari ameshabeba upande wake wa benchi (kutop up bajeti), uongozi unatakiwa na wenyewe ubebe upande wake kwa kuitumia 'efficiently' hiyo pesa kwa kusajili wachezaji wazuri. Na kila mmoja alaumiwe kama atashindwa kutimiza jukumu lake
 
Anajichanganya tu ili kulazimisha point yake.

Sawadogo anakosa tu fitness hasa kwenye pumzi na inawezekana ana majeraha fulani ila ni mchezaji mzuri. Ana uwezo wa kuficha na kutembea na mpira katikati ya wapinzani kwa kujiamini, kitu ambacho midfielders wengi wa Simba na Yanga hata wa kigeni wanashindwa. Kwa kipindi hichi angewafaa zaidi Simba kama angekuwa anaanzia benchi na kuingia kipindi cha pili kuituliza timu pale inapokuwa tayari inaongoza.

Ni kweli hakuna wachezaji wengi wazawa waliojipambanua kwa utofauti wao. Wengi wanacheza mpira unaofanana, wanacheza mpira wa kupokea pasi na kutoa pasi haraka, hawana uwezo wa kumiliki mpira kwa utulivu na kutoa pasi mpenyezo zenye manufaa katika mchezo. Hawana uwezo wa kupress mbele na mpira kwa pasi za haraka lakini zilizo sahihi. Kutoa pasi sahihi lazima wapunguze sana kasi ya kucheza.

Ukitaka kuona mapungufu hayo, wafanyie zoezi lile la duara la kupasiana uone zitapigwa pasi ngapi kabla ya mtafutaji mpira hajaweza kuugusa.
Kwani kasema Sawadogo hana kitu?
 
Mo anazingua sana mala ajitoe mala Arudi haeleweki.

Hawa wachezaji wake
WA Buku buku hatuwataki Simba.
Kanute.
Banda.
Okrah.
Ottara.
Onyango.
Sawadogo.

Simba Ina wachezaji wa Tano tu.
MANURA, kapombe, Shabalala, Inonga , chama na Saidoo tu.
Wengine woote ni taka taka.
ukiwa na akili timamu na ukiwa huna ujinga Kanoute na Banda huwezi kuwaandika kipuuzi kama hapa. Hata rafiki zangu GENTAMYCINE na @okwbobansunzu hawatakuelewa.
 
Wanamuita Muda, zee rrraa kukaba na kusambaza upendooo
#SemaNn, Sawadogo tumpe Muda
 
Back
Top Bottom