Mengi amezungumza kwa usahihi hasa hili la kero, fujo na utaratibu mbovu wa kuingia na kutoka uwanjani.
Ila haya mengine, kuhusu tamasha, I think ameyazungumza kwa jicho la kimpira zaidi na sio kwa ukubwa wa tamasha husika.
Ni mara nyingi nimejumuika na watu ambao sio watu wa mpira, ila tu wamefuata pale burudani.
Hivi hawa watu wajae namna ile sababu ya:
Yanga vs Red Arrows?
Simba vs APR?
Wengi wanafuata burudani tu, je hizi show zinaanza saa ngapi? unakuta muda ya saa nane tu watu wanaanza show.
Haya matamasha asiangalie tu kwa picha ya mpira, ila achukue kwa ukubwa wa entertainment.
By the way, Tayari amejimilikisha akili kuwa wenye akili wana mawazo kama yake, sisi tutasema nini?
Ila kuhusu utaratibu wa kuingia uwanjani tubadilike, sio lazima tuwe kama ulaya, ila hata wakati wa AFL tulifanya poa. Inawezekana.