pwilo
JF-Expert Member
- May 27, 2015
- 10,913
- 13,876
Nawasalimu kwa jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania,
Ule msemo wa usikate tamaa kwenye maisha kila kitu kina mda wake ni wa kweli kabisa japo wengi wetu tunakuwa sio wavumilivu na kuona kama tunachelewa hivi wakati mwingine.
Sikia hii kutoka kwa EDUARDO MENDY:
kwa wale msiofuatilia mpira au msio mfahamu huyu ni mlinda mlango namba moja wa timu ya CHELSEA ya nchini uingereza na timu ya taifa ya SENEGAL iliyochukua AFCON usiku wa juzi.
Wakala wake alimkimbia na kumzimia simu akiwa na umri wa miaka 22 akidai hana kipaji cha mpira na akabakia mtaani mwaka mmoja bila timu.
Alicheza msimu mmoja buree ili aonyeshe kiwango chake lakini hakufanikiwa pia wazazi wake wakaamua kumpeleka ufaransa kwenye academy ya mpira ambayo alipitia POGBA,DIARRA,PAYET NA MAHREZ inaitwa le havre academy nchini ufaransa.
Licha ya kuwa mzuri ila hakupata nafasi ya kucheza nchini ufaransa akaamua kwenda daraja la tatu ili apate mda mwingi wa kucheza katika club ya CHERBOURG mwaka 2011 ambapo alianza soka la kulipwa.
Hakufanya vizuri na baada ya miaka mitatu (2014) baada ya kuachwa alijaribu kumtafuta wakala wake ila hakujibu sms wala kupokea simu baada ya mda mrefu alitumiwa sms na wakala wake akimtakia kila la kheri katika maisha yake ya soka.
Alitaka kuacha mpira akarudi mtaani mwaka mmoja bila timu ila wazazi wake wakaendelea kumpa moyo na kumtaka asikate tamaa na ajaribu tena kwa mara nyingine.
Akiwa na miaka 24 alirudi tena le havre academy ya nchini ufaransa na akacheza bure kwa mwaka mmoja kuonyesha tena kipaji chake.
Mwaka 2015 rafiki yake (TED LEVIE)
akamtaarifu kuna nafasi ya mlinda mlango club ya MARSEILLE na kumuomba ajiunge nao alikubali ombi lake la kujiunga nao na akawa mlinda mlango chaguo la nne.
Huko pia mambo yakawa magumu kwani hakupata nafasi akaondoka na kujiunga na club ya RENNES mwaka 2016 kwa ajili ya kupata mechi nyingi za kucheza na mechi yake ya kwanza kuchezea club yake hiyo ilitokea baada ya kipa namba moja kupewa RED CARD dakika ya 5 tu ya mchezo akaweka rekodi ya clean sheet 3 kati ya mechi 7 alizodakia.
Mwaka 2019 RENNES walimaliza ligi wakiwa nafasi ya tatu na kufuzu kucheza ligi ya mabingwa barani ulaya huku yeye akiwa na clean sheet 14 nyingi zaidi akishika nafasi ya tatu kwa wachezaji wenzake waliomtangulia katika nafasi hiyo.
SEPTEMBER 2020 alijiunga na Chelsea ya nchini uingereza akiwa na umri wa miaka 27 na mpaka sasa akiwa ameshinda;
UEFA,
UEFA SUPER CUP,
UEFA GOAL KEEPER OF THE YEAR,
FIFA BEST GOAL KEEPER OF THE YEAR,
AFCON ,
AFCON BEST GOAL KEEPER .
Never give up on your dreams.