Marahaba! Unajua
Star TV tanzania wako nyuma sana kuanzia mpangilio wa vipindi hadi aina ya watangazaji wanao hitajika kwenye vipindi vya burudani.
Mimi Huyo jamaa sijawai kumuona wala kuona hicho kipindi Lakini sina doubt na yanayo semwa maana Star tv wanajulikana wako nyuma sana.
Tatizo wamejaza wazee kila kipindi wakati kuna vipindi vingine vina hitaji vijana wabichi.
Kuna tangazo lao mmoja ni la mashindano ya kudance sasa linatangazwa kama Habari za kitaifa vile kumbe burudani na lina tangazwa na watu walio zoea kutangaza habari za kisiasa halafu wazee daaa huwa nikiliona nacheka sana daaaaa .......
Star tv wana tatizo kwenye aina ya watu wa kuajiri, Wao wana fikiri kila mtangazaji ana faa kwenye kila idara na cha kushangaza muda wote huo hawajifunzI kwa wenzao EATV.