Education

funda

Member
Joined
May 9, 2020
Posts
16
Reaction score
5
Hellow wana JF wotee, mm ni kijana wa miaka 20 nipo chuo coz ya clinical medicine mwaka wa 2 , nimetembelea TCU nikaona kuja kusoma degree ya medicine MD mpaka uwe na credit ya chemistry ila mm Nina D yani pass , kwahiyo taishia diploma tuu hata nikifaulu vizuri , nataka niache chuo niende advance nikasome HKL kwan nilifauru vizuri masomo yote ya arts ,, ndoto yangu mm nikupata degree tuu ,, naombeni ushauri wenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
...unataka heshima kwamba tu una degree au unataka kuitumia iyo degree kutoboa maisha

sijui itakuaje
 

Kuna taratibu/miongozo miwili ya TCU,kwa wale wanaotarajia kujiunga na degree (undergraduate)...

Hiyo ulioiangalia ni kwa wale wanaotokea form six,lakini kwenu mnaotokea diploma kuna qualification zenu pia...Miaka ya nyuma ilikuua gpa ya 3.5 kwa miaka hii fuatilia ikoje

Yote ya yote nakushauri endelea na chuo (diploma),kazana upate gpa nzuri,Anza kwa kufanya kazi,baadae baada ya miaka 2 au 3 utajiendeleza degree..(kama vipi pia una gpa nzuri na uko desperate sana na degree utaapply degree)

Sikushauri uende urudi ukasome hkl..sikuizi kuna sekeseke kubwa la mkopo,waweza baadae ukakosa mkopo (kama maisha yako ni ya hhali ya chini),pia kwa masomo ya arts ajira zasumbua
 
Nimefatilia nikakuta kujiunga na MD ni diploma ya co with 3.5 GPA or B+ with two credit of o - level for chemistry and biology ,,, sasa mimi chemistry ina miss

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Karibuu sana JF mjukuu wetu upate kufaidi GT.
 
Maisha jinsi yalivyo magumu kuna watu wanakomaa bado na shule mpaka kupata degree ngoja nimalizie hii k vant nikalale
 
Kikubwa ni kujua elimu uliyonayo itakusaidiaje kupambana na mazingira yako.. huku mtaani kuna ukosefu wa ajira,wanataka experience za miaka n.k sikutishi ila ni taarifa ambayo ama ukiitumia unaweza fanya maamuzi sahihi..
 
Hiyo course unayosoma ni nzuri sana pia hajira ni uhakika katika hiki kipindi cha Jiwe wizara ya Afya ameipa kiumbele na hajira nyongi ni Afya na Polisi
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…