Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MHE. EDWARD LEKAITA, Mbunge wa Jimbo la Kiteto Afanya Ziara Kata ya Kibaya na Lengatei
Mbunge wa Jimbo la Kiteto Mkoa wa Manyara, Mhe. Edward Ole Lekaita amefanya ziara katika Kata ya Kibaya na Lengatei na kukutana na Makundi mbalimbali ikiwemo Maafisa Usafirishaji (Bodaboda) wa MaishaPlus, Wazee wa Kibaya Mjini na Soko la Kibaya.
Vilevile, Mhe. Edward Ole Lekaita amefika katika familia mojawapo iliyopatwa na msiba ili kutoa pole lakini pia na kushiriki dua ya 40 ya msiba ikiwa ni arobaini ya msiba wa mwananchi wake uliotokea Kibaya ambapo aliwasihi wananchi wote kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kijamii.
Aidha, Mhe. Edward Ole Lekaita alifika Kata ya Lengatei ambapo alishiriki Maadhimisho ya wiki ya Wazazi Mkoa wa Manyara yaliyofanyika katika Kata ya Lengatei na kuongozwa na mgeni rasmi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara, Mhe. Peter Toima.
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-04-29 at 05.58.41.jpeg648.7 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2024-04-29 at 05.58.40.jpeg593.7 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-04-29 at 05.58.39.jpeg112.2 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-04-29 at 05.58.38(1).jpeg114.2 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-04-29 at 05.58.38.jpeg109.5 KB · Views: 3